Mbio za bao la buku: Ronaldo 979, Lionel Messi amfuata 927
Muktasari:
- Bao hilo limemfanya Ronaldo kubakiwa na mabao 21 pekee kufikisha lengo lake la kufunga mabao 1,000 katika soka la ushin dani, rekodi ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na mashabiki duniani.
RIYADH, SAUDI ARABIA: MKONGWE Cristiano Ronaldo amezidi kusogea kwenye historia ya soka baada ya kufunga bao lingine katika ushindi wa Al Nassr wa mabao 2-1 dhidi ya Abha, na kufikisha idadi yake ya mabao rasmi 979 katika mechi zote za ushindani.
Bao hilo limemfanya Ronaldo kubakiwa na mabao 21 pekee kufikisha lengo lake la kufunga mabao 1,000 katika soka la ushin dani, rekodi ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na mashabiki duniani.
Kwa namna ya kipekee, Ronaldo alifunga bao hilo dakika ya 21, akiibuka ndani ya eneo la hatari na kupiga kichwa kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Angelo.
Bao hilo liliifungulia Al Nassr njia ya ushindi, huku bao la pili likifungwa na Abdullah Al-Hamdan kabla Abha kujibu kupitia Nabil Fekir dakika ya 75 kwa mkwaju wa moja kwa moja wa mpira wa adhabu.
Ushindi huo umeifanya Al Nassr kufikisha pointi 15 baada ya michezo sita ya Ligi Kuu Saudi Arabia na kubaki kileleni mwa msimamo ikiwa na poi nti sa wa na Al Hilal na Al Qadsiah.
Ronaldo, mwenye umri wa miaka 41, hakufunga bao hilo pekee, kwani alikaribia kuongeza idadi yake mara mbili katika kipindi cha kwanza.
Shuti lake moja liligonga mw amba kabla nafasi nyingine muda mfupi baadaye kuondolewa kwenye mstari wa goli na beki wa Abha.
Katika msimu huu wa Ligi Kuu Saudi Arabia, Ronaldo sasa amefunga mabao matatu, huku jumla yake ya mabao katika ligi hiyo tangu alipowasili Saudi Arabia mwaka 2022 ikiwa 131.
Katika safari yake ya kufikisha mabao 979, Ronaldo amefunga mabao mengi zaidi akiwa Real Madrid ambako alifunga 451.
Anafuatiwa na mabao 146 aliyofunga akiwa na timu ya taifa ya Ureno, 145 Manchester United, 131 Al Nassr, 101 Juventus na matano aliyofunga Sporting CP mwanzoni mwa taaluma yake.
Kwa upande mwingine, Lionel Messi ndiye anayemfuata Ronaldo kwa karibu katika mbio hizi akiwa na mabao 927, tofauti ya mabao 52.
Messi pia ni miongoni mwa wachezaji 30 walioteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu. Kwa Ronaldo, sasa hesabu iko wazi ya mabao 21 tu ndiyo yanayomzuia kufikisha idadi ya mabao 1,000.
Al Nassr itaendelea na ratiba yake katika Ligi Kuu Saudi Arabia na mashindano ya Asia, huku Ronaldo akiendelea kuongeza idadi yake katika kile kinachoweza kuwa sura ya mwisho ya ushindani mkubwa uliotawala soka kwa zaidi ya miongo miwili.
Mbio za kufikisha mabao 1,000 sasa zimekuwa moja ya sura kubwa zaidi katika safari ya Ronaldo, huku kila bao jipya likimpeleka hatua moja karibu na rekodi hiyo ya kihistoria.