Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maumivu ya kisigino iko hivi

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo maarufu kama El Clasico Ilitazamwa na mamilioni ya mashabiki duniani, na Real Madrid chini ya kocha Jose Morihno ilifanikiwa  kuifunga Barcelona kwa mabao 2-1 ndani ya uwanja wa nyumbani.

WIKI iliyopita ilimalizika katika medani ya soka Jumapili kuliposhuhudiwa mechi kali na maarufu ya wapinzani wa jadi kati ya Barcelona na Real Madrid nchini Hispania iliyopigwa kwenye Uwanja wa Camp Nou uliopo Barcelona.

Mechi hiyo maarufu kama El Clasico Ilitazamwa na mamilioni ya mashabiki duniani, na Real Madrid chini ya kocha Jose Morihno ilifanikiwa  kuifunga Barcelona kwa mabao 2-1 ndani ya uwanja wa nyumbani.

Mara baada ya mechi hiyo kwa utafiti wa kutazama, utabaini wachezaji wengi walitoka uwanjani wakiwa wanachechemea. Hii ni hali ya kawaida kwa wachezaji wanaoshiriki mechi kali kama ile.

Hata katika ligi ya hapa nyumbani, hali hiyo ya wachezaji kupata maumivu ya visigino mara baada ya mechi huwa ni kawaida. Maumivu hayo yanaweza kuwa makali ya wastani mpaka makalI yasiyovumilika. Ukiacha majeraha ya misuli ya paja na kigimbi, wanasoka ambao wanakimbia kasi mara kwa mara uwanjani huwa ni vigumu kukosa kupata maumivu katika eneo la kisigino.

DOK 02

Hii ni kutokana na eneo hilo kuhusika pia katika hekaheka za uwanjani na huku likipokea shinikizo kubwa la uzito wa mwili. Siku ya leo nitawapa ufahamu sababu kwa wanasoka na wakimbiaji wengine kupata maumivu ya kisigino wakati na baada ya kushiriki mazoezi, mashindano au mechi kali.


KINACHOTOKEA KATIKA KISIGINO

Ni kawaida katika maisha ya wanasoka wengine kujiuliza kwa nini wanapata maumivu ya kisigino kiasi cha kushindwa kufanya mazoezi, hii ni kutokana na kuwahi kupata shida hii. Eneo la kisigino ni la chini ya mguu ambalo ni kawaida kupata majeraha au shambulizi la tishu laini ambayo mara kwa mara yamekuwa ni chanzo cha maumivu katika eneo hilo

Tishu laini ijulikanayo kama Archille Tendon ndiyo hupata majeraha mara kwa mara. Nyuzi hii ngumu ni mojawapo wa muhimili mkubwa unaounganisha mfupa wa kisigino na msuli wa kigimbi cha mguu.

DOK 01

Kisigino ni sehemu mojawapo ya eneo la mguu wa chini yaani kifundo cha mguu, eneo ambalo kwa ujumla hupata majeraha ya ndani kwa ndani na kuleta maumivu. Kifundo cha mguu ni ungio bawaba lenye mijongeo miwili yaani kuelekea mwilini na nje ya mwili. Eneo hilo  hukutanisha mifupa miwili ya mguuni pamoja na kisigino ili kuunda ungio la kifundo.

Wakati wa kucheza na kufanya mazoezi ya kawaida ndipo majeraha ya kifundo pamoja na tishu zinazozunguka eneo hilo na nyuzi ya Achiles Tendoni hujitokeza. Shambulizi la nyuzi ngumu katika kisigino kitabibu hujulikana kama Achiles Tendon ni miishilio wa misuli ya kigimbi iliyokamatana pamoja na kwenda kujipachika katika mfupa wa kisigino.

Wanasoka, wanariadha, wacheza kikapu na wanamichezo wengine wote hutumia sana miguu kwa kukimbia, kupigia mpira, kuruka na kutembea hali hii ndio inafanya eneo la kifundo kupata majeraha ya mara kwa mara kutokana na kujipinda au kujivuta nyuzi hizo kupita uwezo wake.

DOK 02

Nyuzi ya Achille tendon, unaposhika juu ya kisigino upande wa nyuma ndipo ilipo. Hupata shambulizi kutokana na mlipuko wa mjibizo wa kinga ya mwili baada ya kupata majeraha ya kifundo. Nyuzi hii ndio inayokuwezesha kunyanyua mwili kwa upande wa nyuma na hata kuruka kichura chura.

Majeraha hayo ikiwamo yale yanayotokea wakati wa michezo pamoja na kutumika sana kuliko pitiliza mfano kufanyishwa mazoezi magumu yaliyopita kiwango na pia magonjwa mengine ya mwilini.

Nyuzi ya Achille pale inapopata shambulizi huweza kusababisha maumivu makali, kuchechemea, kushindwa kuutumia vema mguu wake na kumnyima utulivu wa kimwili na kiakili.

Maumivu huweza kuyahisi zaidi katika kisigino yakisambaa mpaka maeneo ya kigimbi huku yakiuma na kupwita. Mwanamichezo anaweza kuhisi maumivu akijinyanyuka au hata akiwa katika mkanyago wa bapa wa unyayo wa mguu. Anayepata tatizo hili atalazimika kufika katika huduma za afya kwa uchunguzi na matibabu ili kubaini kama tatizo ni lakuhitaji upasuaji.

Matumizi ya kuweka barafu mara tatu kwa siku kwa muda wa dakika 20-15 inasaidia kupunguza maumivu. Dawa za kawaida za kupunguza maumivu na uvimbe zinaweza kutumika ikiwamo zile zakunywa, zakupaka na kuchoma katika msuli. Ila hazipaswi kutumiwa kiholela bila ushauri wa daktari.


DOK 03

KUPUNGUZA MAUMIVU

Mwanasoka au anayeshiriki michezo inayohusisha kukimbia atahitajika kuhakikisha anapasha mwili moto na kunyoosha viungo vya mwili ikiwamo katika eneo la kifundo cha mguu kabla ya kuingia michezoni au mazoezini.

Kufanya hivyo kunaziandaa tishu laini za eneo hilo kuwa na wepesi na hatimaye kuweza kunyumbulika kirahisi bila kuleta majeraha yanayoleta maumivu. Wachezaji wajenge mazoea ya kutembea au kucheza katika maeneo au viwanja ambavyo sakafu yake sio ngumu na yasiyo na vichugu au mabonde.

Kama tatizo hilo linajirudia mara kwa mara ni vizuri mchezaji apumzike siku tatu hadi saba katika mchezo huo, na ashiriki michezo isiyo na kukumbana kimwili ikiwamo kuogelea na kuendesha baiskeli.

Kudhibiti uzito wa mwili ili kupunguza shinikizo kubwa katika kisigino. Ikumbukwe kuwa uzito mkubwa ni moja ya kihatarishi cha kupata maumivu ya kisigino. Ni muhimu buvaa bandeji maalumu ili kuleta utulivu wa ungio la kifundo na hakikisha siku zote unafanya mazoezi ya viungo ya kunyoosha kifundo kabla na baada ya mechi au mazoezi.

Pia muhimu kuzingatia uchaguzi sahihi wa viatu vya mazoezi na vile vya kuchezea kwani viatu vyenye njumu ndefu kupita kiwango kilichowekwa huchangia maumivu ya kisigino. Na zaidi, wasiliana na walimu wa mazoezi juu ya maumivu uliyo nayo. Endapo maumivu yakizidi fika mapema katika huduma za afya kwa ushauri zaidi.