Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TYSON FURY: Ngumi nzito, mkwanja mzito

Muktasari:

  • Katika pambano hilo lililokuwa la raundi 12, Fury alilipwa takribani Dola 25 milioni kama sehemu ya malipo.

LONDON, ENGLAND: USIKU wa juzi Jumamosi, bondia raia wa England, Tyson Fury alipamba sana vichwa vya habari baada ya kumchapa mpinzani wake Arslanbek Makhmudov kutoka Urusi.

Katika pambano hilo lililokuwa la raundi 12, Fury alilipwa takribani Dola 25 milioni kama sehemu ya malipo.

Hata hivyo, kiasi hicho cha pesa kinaonekana ni kidogo sana ikilinganishwa na kile ambacho anatarajia kukipata ikiwa atapigana na Anthony Joshua baadae mwaka huu.

Katika pambano hilo la Joshua, pesa za kabla ya kupanda ulingoni zinakadiriwa ni zaidi ya Dola 60 milioni kwa kila bondia.

Leo tumekusogezea hapa utajiri kamili wa Tyson ambaye kwa mwaka huu anaweza kuingia katika tatu bora ya mabondia walioingiza pesa nyingi zaidi ikiwa pambano hilo dhidi ya Joshua litakuwepo.

ANAPIGAJE PESA

Kwa sasa, Fury anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 100 milioni. Asilimia 70 ya utajiri wake inatokana na malipo anayoyapata kutokana na mapambano mbalimbali.

Mapambano yake dhidi ya mastaa kama Deontay Wilder na Dillian Whyte yanatajwa kuwa ndiyo yalimwingizia pesa nyingi zaidi katika maisha yake ndondi.

Dhidi ya Wilder aliingiza jumla  Dola 80 milioni na dhidi ya Whyte alipata Dola 30 milioni.

Pambano dhidi ya Dillian Whyte lilimwingizia zaidi ya Dola milioni 30

Kwa mwaka anakadiriwa kupata hadi Dola 200 milioni kupitia malipo ya mapambano pekee.

Mbali na mapambano, Fury pia hupata pesa kutokana na mikataba ya udhamini aliyoingia na kampuni mbalimbali.

Fundi huyu pia ana udhamini na kampuni kama MTK Global, WOW Hydrate na Fashion Nova na kwa pamoja kwa mwaka hupata Dola 15 milioni kwa mwaka.

Kupitia mitandao ya kijamii pia bondia huyu hupata mpunga wa kutosha na kwa mwaka anakadiriwa kupata Dola 50000 kwa kila chapisho.

MIJENGO

Fury anaishi katika jumba la kifahari jijini Morecambe, England, lenye thamani ya zaidi ya Pauni 4 milioni ambalo ndani yake lina Gym kubwa ya mazoezi ya ndondi, bwawa la kuogelea na sehemu kubwa ya kupumzikia.


NDINGA

Range Rover – Pauni 100,000

Mercedes-Benz S-Class – Pauni 120,000

Rolls-Royce Phantom – Pauni 350,000

Ferrari Portofino – Pauni 200,000

Ferrari GTC4Luss-Pauni 250,000.

Porsche Taycan-Pauni 150,000.

Range Rover Sport SVR-Pauni 50,000.

MSAADA KWA JAMII

Fury ni mmoja kati ya wanamichezo wanaojulikana kwa kuwa na  moyo wa kusaidia sana jamii.

Baada ya pambano lake na Wilder, alitangaza kutoa sehemu kubwa ya mapato yake kwa ajili ya kusaidia watu wasio na makazi.

Pia amekuwa mstari wa mbele kuzungumzia, afya ya akili na mara kadhaa amekuwa akisapoti miradi ya maendeleo katika nchi mbalimbali huko  Asia na Afrika.


FAMILIA, MAISHA BINAFSI

Tyson Fury yupo katika ndoa na mrembo Paris Fury, ambaye amebahatika kuzaa naye watoto wanne, wawili wa kiume na wawili wa kike.

Mara kadhaa amekuwa akiweka wazi familia yake ina mchango mkubwa katika maisha yake, hasa katika kipindi alichopitia changamoto za afya ya akili na matumizi ya dawa za kulevya.