Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mangungu, Magori ile ya Malawi poa sana...

MANGUNGU Pict

Muktasari:

  • Sisi hapa kijiweni mara zote tumekuwa tukiwahimiza Simba wazike tofauti zao na wawe kitu kimoja kwa ajili ya ustawi wa klabu yao badala ya kuwa na minyukano.

ILE video inayowaonyesha Mzee Murtaza Mangungu na Mzee Crescentius Magori wakitoka pamoja uwanjani kule Malawi ina maana kubwa sana kwa Simba.

Sisi hapa kijiweni mara zote tumekuwa tukiwahimiza Simba wazike tofauti zao na wawe kitu kimoja kwa ajili ya ustawi wa klabu yao badala ya kuwa na minyukano.

Si mmeona wenyewe mambo hayajawa mabaya kule Malawi dhidi ya Mighty Wanderers na wameshinda ugenini hivyo hawatokuwa na kazi kubwa nyumbani katika marudiano.

Kupishana kauli na migongano kwenye timu ni jambo la kawaida na halijaanza leo lakini halipaswi kuonyeshwa hadharani hadi kupelekea watu kugawanyika na kuanza kuonyesheana vidole.

Shida watu wanapoonyesha kutofautiana hadharani lazima makundi yaibuke na kuchagua upande wa kusapoti ili tu kuonyeshana nani zaidi.

Kwa uzoefu wetu hapo lazima timu iathirike maana kwa mpira wetu ulivyo ndio yataanza mambo ya kupigishana shoti ili kila upande uukomoe mwingine na uibuke.

Haya mambo sio bhana. Simba ni timu kubwa ambayo inatakiwa kufokasi na mambo ya uwanjani ambayo ni kushindania makombe na sio kusakana uchawi nani mbaya na nani mzuri.

Magori na Mangungu wakiendelea kuonyesha kuwa wapo pamoja, wale machawa wa kila upande nao lazima watulie tu na kurudisha nguvu kusapoti timu yao kwenye kibarua kilicho mbele yake.

Kauli mbiu ya Simba si Nguvu Moja? Basi watuonyeshe kwa vitendo maana ya msemo huo badala ya kwenda kinyume chake.