Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City na adhabu ya pointi, Opta yatoa picha

Muktasari:

  • Klabu hiyo inaendelea kusisitiza kuwa haina hatia, na juzi, Ijumaa, ilithibitisha imewasilisha rufaa rasmi kupinga uamuzi wa Ligi Kuu England. Hilo ni tukio ambalo halijawahi kutokea England na kuna mambo mengi ambayo bado hayajajulikana kiasi kwamba haiwezekani kusema kwa uhakika nini kitakachotokea baadaye.

MANCHESTER, ENGLAND: TANGU Manchester City ipatikane na hatia ya kukiuka kanuni za kifedha za Ligi Kuu England kwa miaka tisa (2009-2018), kumekuwapo na mijadala mingi kuhusu adhabu ambayo inaweza kutolewa dhidi yake; lakini je kutakuwa na athari gani katika adhabu ya kupokonywa pointi?

Klabu hiyo inaendelea kusisitiza kuwa haina hatia, na juzi, Ijumaa, ilithibitisha imewasilisha rufaa rasmi kupinga uamuzi wa Ligi Kuu England. Hilo ni tukio ambalo halijawahi kutokea England na kuna mambo mengi ambayo bado hayajajulikana kiasi kwamba haiwezekani kusema kwa uhakika nini kitakachotokea baadaye.

Hata hivyo, mtazamo unaofikiriwa na wengi ni mchakato wowote wa rufaa unaweza kufanya ichukue muda mrefu kabla ya uamuzi wa mwisho kufikiwa kuhusu adhabu ambayo City itatumikia iwapo itashindwa.

Aina za adhabu zinazotajwa ni nyingi, lakini kwa kuwa Everton na Nottingham Forest ziliwahi kupewa adhabu ya kupokonywa pointi kutokana na kukiuka kanuni za kifedha miaka ya karibuni, kuna uwezekano City pia inaweza kukabiliwa na adhabu kama hiyo msimu huu.

Lakini, kile ilichofanya Opta Analyst, mtandao wa takwimu na uchambuzi wa kimichezo ni kutumia kompyuta maalumu kuonyesha kwa usahihi athari ambayo adhabu yoyote ya kupokonywa pointi kwa Man City inaweza kuwa nayo kwenye ligi hiyo msimu wa 2026/27.

Kwa sasa City ndiyo inayoongoza ligi ikiwa ndiyo timu pekee iliyobaki na rekodi ya kushinda kwa asilimia 100, baada ya kuwa timu ya 14 pekee katika historia ya mashindano hayo kuanza msimu kwa ushindi katika mechi tano mfululizo. Lakini, adhabu ya kupokonywa pointi inaweza kuvuruga kabisa msimu wao. Hata hivyo, hata bila adhabu hiyo ingekuwa na kazi kubwa ya kufanya ili kutwaa ubingwa kwa kuwa ni timu nne tu kati ya 14 zilizowahi kuanza msimu kwa ushindi wa mechi tano mfululizo ambazo baadaye zilitwaa ubingwa.


TWENDE KAZI

Ni wazi kuanza msimu kwa kasi siyo lazima kusababishe mafanikio mwishoni na kwa sasa Opta inaitabiria City kuwa timu ya pili yenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa ikiwa na uwezekano wa asilimia 39.9 nyuma ya Arsenal yenye asilimia 44.2. Hii ni kwa kuzingatia kwamba hakutakuwa na adhabu ya kupokonywa pointi, kama ilivyo kwa sasa.

Lakini adhabu ya kupokonywa pointi itaiathiri vipi hasa nafasi zao? Opta imechambua mechi zilizobaki za msimu, kisha ikatumia kila kiwango kinachowezekana cha adhabu ya kupokonywa pointi na kutoa nafasi ambayo City itamaliza katika msimamo wa ligi. Kilicho dhahiri ni iwapo itapigwa na nyundo hiyo nafasi ya kutwaa ubingwa itapungua pamoja na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini labda jambo la kuvutia zaidi ni kujua adhabu ya pointi itahitajika kuwa kubwa kiasi gani ili kufanya iwezekane City kushuka daraja. Kwa mujibu wa matokeo ya uchambuzi wa kompyuta hiyo, nafasi ya City kushuka daraja itakuwa ya uhakika ikimaanisha iwapo itakumbana na adhabu ya kunyang'anywa pointi 74. Kwa kila adhabu ya chini ya pointi 74 kuna angalau uwezekano City inaweza kuepuka kushuka daraja.

Hii ina maana kwamba kompyuta hiyo imebaini kwamba ni nadra ambapo City ikipokonywa pointi 73 lakini ikashinda mechi za kutosha na bado ikamaliza ikiwa na jumla ya pointi nyingi kuliko timu nyingine tatu za mkiani.

Hilo litahitaji City kushinda karibu mechi zote zilizobaki, jambo ambalo lisilowezekana. Kompyutaya Opta ilichukua adhabu ya kupokwa pointi 40 kuifanya City ifikie uwezekano wa zaidi ya asilimia 50 wa kushuka daraja, huku uwezekano huo ukiendelea kuongezeka hadi pointi 60 na nafasi ya kushuka daraja inakuwa karibu sana, ingawa bado haifiki asilimia 100.

Lakini, Opta kwa kila adhabu ya pointi 30 au chini, City ilishuka daraja na kwa adhabu yoyote ya hadi pointi 20, nafasi ya kushuka daraja iliendelea kuwa chini ya asilimia tano, ina maana haiwezekani kushuka.

Kwa upande wa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, adhabu ya kupokwa pointi 38 itapunguza nafasi za City kufuzu hadi chini ya asilimia moja, kwa kuzingatia timu nne za juu za Ligi Kuu England ndizo zinazofuzu mashindano hayo. Iwapo nafasi ya tano itapatikana kama ilivyokuwa katika misimu miwili iliyopita City itakuwa na nafasi zaidi kidogo, kwani itahitaji adhabu ya pointi 40 ili kupunguza nafasi yao ya kufuzu hadi chini ya asilimia moja.

Kwa upande wa mbio za ubingwa, kompyuta hiyo maalumu inakadiria kuwa City itaendelea kuwa na uwezekano wa zaidi ya asilimia 10 wa kutwaa ubingwa ikiwa itapokonywa chini ya pointi 10. Hata hivyo, itahitaji kupokonywa pointi 25 ili nafasi yao ipungue na kuwa chini ya asilimia moja, hivyo kuwa na uwezekano mdogo sana wa kutwaa ubingwa.

Kwa sasa, hakuna anayejua adhabu ambayo City itapewa, lakini kompyuta maalumu ya Opta inaweza kutupa picha zaidi kuhusu athari ya adhabu yoyote inayoweza kutolewa ya kupokonywa pointi.