Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atakayeshinda mchezaji bora 2025/2026 poa tu

MVP Pict

Muktasari:

  • Kiufupi kamati imeteua wachezaji ambao wamestahili na yeyote kati ya hao ambaye ataibuka mshindi halitokuwa jambo la kushangaza.

YALE majina ya wachezaji nane yaliyotangazwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu msimu uliopita wa 2025/2026 kila mmoja anastahili kuwepo katika kinyang’anyiro.

Jamaa walipiga mzigo sana na walizibeba sana timu zao na hakuna aliyewekwa katika ile orodha kwa kupendelewa na ushahidi wa hilo uko wazi.

Ibrahim Bacca alikuwa askari imara wa safu ya ulinzi ya Yanga na akaisaidia kumaliza ikiwa imefungwa mabao machache kama ilivyokuwa kwa Rushine de Reuck wa Simba ambaye timu yake ilishika nafasi ya pili kwa kuruhusu nyavu kutikiswa mara chache.

Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa alitoa mchango mkubwa kwa Azam FC katika kuifungia na kupika mabao kama ilivyokuwa kwa Allan Okello wa Yanga ambaye kwa sasa anacheza soka Morocco.

Okello alifunga mabao 14 na kupiga pasi nane za mwisho huku Fei Toto akifumania nyavu mara 15 na kutoa pasi saba za usaidizi wa mabao.

Mossi Nduwumwe aliyekuwa Mfungaji Bora wa msimu, mabao yake 17 yalitoa mchango wa kuiwezesha Singida Black Stars kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chama alifunga mabao manane na kupiga pasi nne za mwisho huku Maxi Nzengeli yeye licha ya mara nyingi kucheza kiungo wa chini, alifunga mabao sita na kupiga pasi tano za mwisho.

Kwa upande wa Pacome Zouzoua, yeye alifunga mabao tisa na kusaidia kupatikana kwa mabao mengine manne kwa kupiga pasi za mwisho kwa wenzake.

Kiufupi kamati imeteua wachezaji ambao wamestahili na yeyote kati ya hao ambaye ataibuka mshindi halitokuwa jambo la kushangaza.