Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Azam hii sajilini mabeki na kipa

AZAM FC inaendelea na kambi yake ya maandalizi ya msimu mpya hapa Sousse nchini Tunisia na Kocha Yousouph Dabo anatoa dozi ya hatari.
Moja kati ya maeneo ambayo Dabo kayatolea sana macho ni safu ya kiungo na ile ya  ushambuliaji.
Anatumia muda mwingi sana kuzinoa safu hizo kila siku ya mazoezi.

Kwenye safu ya kiungo kuna Sospeter Bajana, James Akaminko na Feisal Salum.
Lakinia kuna Isah Ndala na Tape Edigno ambao nao wana mabalaa yao makubwa katika eneo hilo.
Viungo wa pembeni kuna Abdul Sopu, Gjibril Sillah, Kipre Junior na Idd Nado.

Safu ya ushambuliaji kuna Prince Dube, Idris Mbombo na Alassane Diao.
Lakini mwalimu Dabo anataka kumbadilisha Ayubu Lyanga kutoka winga ili atumike kwenye eneo la ushambuliaji wa kati.
Hawa ndiyo watu ambao Dabo anakesha nao usiku na anashinda nao mchana kuhakikisha wanakuwa silaha yake ya maangamizi.


RATIBA ILIVYO
Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku, kila siku na Ijumaa ya Julai 14, Azam ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan kwenye uwanja wa Marsa mjini Tunis.
Mechi hii ilianza saa 11:30 jioni kwa saa za Tunisia, lakini asubuhi ya siku hiyo Dabo alikuwa na kipindi cha mazoezi kwa vijana wake kama kawaida...na aliwakamua kweli kweli.
Yaani dozi ya mazoezi ya siku hiyo ilikuwa nzito kiasi kwamba huwezi kuamini kwamba hawa ndiyo wachezaji ambao jioni watacheza mechi dhidi ya Al Hilal ya Ibenge, ambayo iko hapa Tunisia kwa ajili ya kushiriki mashindano ya klabu bingwa ya nchi za kiarabu.
Ushindi wa 3-0 dhidi ya miamba hao ambayo waliwatoa mabingwa wa Tanzania kwenye ligi ya mabingwa na kukosa bahati kidogo tu kuwatoa Al Ahly ya Misri, unaonesha ni namna gani vijana wa Dabo wanaenda vizuri.


HAPA NDIPO PENYEWE
Yousouph Dabo ni muumini wa soka la kushambulia na kumiliki mpira. Anasema ili timu iwe bora katika umiliki wa mpira, inatakiwa iwe na safu ya kiungo yenye watu wanaoelewana sana.
Kwa hiyo mazoezi yake yanalenga katika kuwafanya viungo wake waelewane zaidi na zaidi ili waweze kupishana uwanjani kama mataiiri ya tingatinga.
'Azam FC ina wachezaji wazuri sana kiufundi, wanachopungukiwa ni mbinu kidogo tu', alisema Dabo kwenye moja ya mahojiano yake yaliyochapishwa kwenye akaunti ya Instagram ya Azam FC.
Mbinu anazozizungumzia hapo ndiyo hizo anazowapa wachezaji hawa.

Anasema anataka timu yake iwe na uwezo wa kujenga mashambulizi kila baada ya dakika tatu.
Yaani timu ifike kwa mpinzani kila baada ya dakika tatu.
'Ili hilo liwezekane, ni lazima wachezaji wawe timamu sana kimwili', anasema Dabo na kusisitiza kwamba ndiyo maana anawapa dozi kubwa ya mazoezi.
Baada ya mechi ya Al Hilal, hakuna mapumziko, ni vipindi viwili tena vya mazoezi, Jumamosi ya Julai 15, asubuhi na jioni.

Asubuhi ni gym na mchana uwanjani. Na hii ndiyo mara ya kwanza kwa Azam FC kutumia jim tangu waje Tunisia.
Dabo anasema wachezaji wa mpira wanahitaji mazoezi ya kuwa na mpira zaidi kuliko kitu chochote.
'Timu yangu itafanya raundi moja tu ya kukimbia ili kupasha moto misuli katika awamu ya kwanza. Baada ya hapo upashaji misuli unahamia kwenye matumizi ya mpira...yaani wanapasha moto misuli huku wakiwa na mpira. Mpira unatakiwa uwazoee na wao wauzoee ili wawe marafiki zaidi na zaidi ', anasema Dabo.
'Hayo yakikamilika, itawapa uhuru viungo kufikisha mipira mingi kwa washambuliaji.

Hii ina maana kwamba tutatengeneza nafasi nyingi zaidi na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufunga.'


URAHISI WA KUFUNGA
Dabo anayafanya yote hayo ili kurahisisha kufunga. Azam inafunga mabao machache kulinganisha na wapinzani kwenye mbio za ubingwa wa Ligi. Wakikuzidi uwezo wa kufunga, ni vigumu sana kuwazidi alama za ubingwa kwa sababu mabao ndiyo yanayoleta ushindi. Tunatakiwa tufunge zaidi'. Anasema Dabo kwa kumalizia.
Dabo anataka mabao tu. Hizi ni salamu kwa timu za ligi kuu kujiandaa kusajili mabeki na makipa maana kuna bomu linapikwa huku.