Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuna mtu ananyolewa! Man United ugenini, Arsenal yaifuata Bayern Munich

KUNYOLEWA Pict

Muktasari:

  • PSG imetwaa mataji mawili mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika misimu miwili ya mwisho iliyopita baada ya kuichapa Arsenal kwa mikwaju ya penalti katika fainali ya msimu uliopita na kwa mara nyingine timu hiyo ni miongoni mwa zinazopigiwa upatu kutwaa taji hilo msimu huu.

MUNICH, UJERUMANI: ACHANA na mechi tisa zilizopigwa jana, ikiwamo ya wababe Ulaya kwa sasa PSG dhidi ya Barcelona, leo kinapigwa tena ambapo michezo tisa inachezwa katika viwanja tofauti.

PSG imetwaa mataji mawili mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika misimu miwili ya mwisho iliyopita baada ya kuichapa Arsenal kwa mikwaju ya penalti katika fainali ya msimu uliopita na kwa mara nyingine timu hiyo ni miongoni mwa zinazopigiwa upatu kutwaa taji hilo msimu huu.

Timu ya mwisho kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya misimu mitatu mfululizo ilikuwa Real Madrid iliyofanya hivyo 2015/16, 2016/17 na 2017/18.

Lakini, leo, Jumatano, Oktoba 21, miongoni mwa mechi zitakazoanza mapema ni ile ambayo Como ya kocha Cesc Fabregas itakuwa mwenyeji wa vigogo wa Ligi Kuu England, Manchester United.

Timu zote mbili zitakuwa na matumaini ya kufuta machungu ya vipigo zilivyovipata katika mechi za raundi ya pili. Manchester United ilifungwa na Atletico Madrid.

KUNYO 03

Como ilifungwa mabao 3-2 na Feyenoord Jumatano iliyopita, lakini kucheza nyumbani kunaweza kuwa faida muhimu katika mchezo huu.

Manchester United imeshinda mechi moja tu kati ya 10 za mwisho za ugenini katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Como ikiwa ilipata ushindi mkubwa wa mabao 4-1 dhidi ya RB Leipzig katika Uwanja wa Stadio Giuseppe Sinigaglia kwenye mechi ya raundi ya kwanza.

Kwa mujibu wa Opta, Como ina nafasi kubwa zaidi ya kushinda ikiwa nyumbani ikipewa asilimia 41.7.

Ushindi wa nyumbani mwingine unatarajiwa katika mchezo kati ya Lille ya Ufaransa na Galatasaray ya Uturuki, ambapo klabu hiyo ya Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1) inatabiriwa kushinda katika asilimia 44.5. Hata hivyo, mechi inayovutia zaidi ni safari ya Arsenal kukabiliana na Bayern Munich.

Timu hizo mbili ambazo zimekuwa zikifanya vizuri zaidi Ulaya katika miaka ya karibuni zitakutana kwenye Uwanja wa Allianz Arena, huku Arsenal ikilenga kurudia ushindi wa mabao 3-1 ilioupata dhidi ya Bayern msimu uliopita katika hatua ya ligi.

KUNYO 01

Ushindi huo ulikuwa miongoni mwa 14 mfululizo ambao Arsenal iliupata katika hatua ya ligi ya mashindano hayo.

Ushindi wa hivi karibuni katika mfululizo huo ulikuwa wa mabao 3-0 dhidi ya Lille nyumbani katika raundi ya pili.

Hata hivyo, Arsenal italazimika kumdhibiti Harry Kane, mshambuliaji wa zamani wa Tottenham ambaye amefunga mabao 15 katika mechi 22 alizocheza dhidi ya Arsenal katika maisha yake ya soka.

Hicho ni kiwango cha tatu kwa ukubwa cha mabao aliyofunga dhidi ya mpinzani mmoja katika maisha yake ya soka. Amefunga mabao mengi zaidi dhidi ya Leicester ikiwa ni 20 katika mechi 20, na Everton 16 katika mechi 17.

KUNYO 02

Ha ta hivyo, kuna takwimu moja muhimu ya kuzingatia; Arsenal imepoteza asilimia 53 ya mechi zake dhidi ya Bayern Munich, ikiwa ni mechi nane kati ya 15.

Miongoni mwa timu ambazo Arsenal imekutana nazo mara tano au zaidi katika mashindano makubwa ya Ulaya, ni dhidi ya Barcelona pekee na ina kiwango kikubwa zaidi cha kupoteza mechi, kwa asilimia 67, ikiwa ni mechi sita kati ya tisa.

Bayern Munich inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu, kwani Wajerumani hao wanapewa asilimia 45.0 ikilinganishwa na 30.7 za Arsenal.

Kwingineko Real Madrid ililazimika kusubiri hadi dakika za mwisho ili kupata pointi zote tatu katika safari yake ya kukutana na Roma kwenye raundi ya pili wiki iliyopita.

KUNYO 04

Madrid ilikuwa nyuma kwa mabao 3-1 zikiwa zimebaki dakika saba tu kabla ya kumalizika kwa mchezo, lakini hatimaye ilishinda kwa mabao 4-3 kutokana na bao la ushindi la Antonio Rudiger dakika ya 90 na safari hii itakuwa mwenyeji wa RB Leipzig katika raundi ya tatu, huku Kylian Mbappe akilenga kuweka historia nyingine.

Mfaransa huyo amehusika katika mabao 97 kwenye mechi 100 za Ligi ya Mabingwa Ulaya, akifunga 72 na asisti 25. Ni wachezaji wanne pekee waliowahi kufikisha mabao 100 waliyofunga au kusaidia kufungwa na wenzao katika mashindano hayo.

Endapo Mbappe atahusika katika mabao matatu kwenye mchezo huo atakuwa mchezaji aliyefikisha idadi hiyo kwa kasi zaidi sawa na Lionel Messi aliyefikisha katika mechi 101.

Wachezaji wengine waliofikia kiwango hicho ni Robert Lewandowski aliyefikisha katika mechi 102, Cristiano Ronaldo mechi 114 na Karim Benzema 134.

KUNYO 05

Kikosi cha Jose Mourinho kinapewa nafasi ya kushinda kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu kwa asilimia 70.5.

Aston Villa iliyopata ushindi mkubwa zaidi katika raundi ya pili, baada ya kuichakaza Fenerbahce kwa mabao 6-0 itakuwa mzigoni miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu zaidi kushinda katika raundi ya tatu pia, ikitabiriwa kuifunga Viking kwa asilimia 72.0.

Ikiwa itashinda, itakuwa mara ya kwanza kwa Aston Villa kushinda mechi nne mfululizo katika Kombe la Ulaya au Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Timu nyingine mbili ambazo zitashinda mechi mbili za mwanzo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu pia zitakuwa wenyeji; Sporting CP itakuwa na matumaini ya kupata pointi nyingine tatu itakapoikaribisha LASK ikipewa asilimia 74.1, ilhali Real Betis nayo inapewa nafasi ya kushinda mbele ya mashabiki wake itakapokutana na Feyenoord kwa asilimia 59.4.

Huku nyuma Inter Milan iliyopata kipigo cha kushangaza cha mabao 4-3 nyumbani dhidi ya Club Brugge, Jumanne iliyopita, lakini sasa ina nafasi ya kufuta machungu ya matokeo hayo kwa kucheza tena nyumbani, safari hii dhidi ya Shakhtar Donetsk kwenye Uwanja wa San Siro.

Inter kwa sasa ipo katika mfululizo wake mbaya zaidi wa kupoteza mechi katika historia ya Kombe la Ulaya/Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwa imepoteza mechi nne mfululizo.

Hata hivyo, inapewa nafasi kubwa ya kurejea kwenye ushindi katika mchezo huu kwa asilimia 75.0.

Tofauti na wapinzani wao waliopoteza, Club Brugge inaingia katika raundi ya tatu ikiwa na morali kubwa kufuatia ushindi huo wa kushangaza nchini Italia.

Nicolo Tresoldi ndiye aliyekuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga mabao matatu. Kwa sasa ana mabao saba katika mechi 12 alizocheza kwa klabu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, na atakuwa na imani ya kuongeza idadi hiyo atakapokutana na Lens.

Lens imekuwa ikiruhusu mabao katika kila moja ya mechi zake 15 zilizopita katika mashindano hayo.

Club Brugge ilishinda mechi zake zote mbili dhidi ya timu za Ufaransa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, kwa tofauti ya mabao matatu katika kila mchezo.

Iliifunga Monaco 4-1 na Marseille 3-1. Brugge inapewa nafasi ya kupata ushindi wa tatu mfululizo dhidi ya timu za Ufaransa kwa asilimia 45.6.