Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kosa la Simba kwa Mwalimu ni hili

MWALIMU Pict

Muktasari:

  • Taharuki ilitokana na sababu mchezaji huyo jana yake alikuwa amefanya mazoezi na kikosi cha Simba na hadi chakula cha jioni alikula pamoja na wenzake na baada ya hapo ndiPo akatimka.

JUZI Jumanne ilikuwa ni siku ya taharuki kwa watu wa mpira kuanzia hapa kijiweni na Tanzania kijumla baada ya Selemani Mwalimu kutua Yanga.

Taharuki ilitokana na sababu mchezaji huyo jana yake alikuwa amefanya mazoezi na kikosi cha Simba na hadi chakula cha jioni alikula pamoja na wenzake na baada ya hapo ndiPo akatimka.

Tathmini ya harakaharaka ya kijiwe imegundua kosa moja kubwa ambalo Simba imelifanya tena kwa kurudia na likasabisha jambo hilo ambalo hapana shaka limewaumiza.

Kosa hilo ni kufanya mambo kwa mazoea ambalo imelirudia zaidi ya mara tatu.

Ilianza kufanya kosa hilo kwa kushindwa kumalizana mapema na Wydad AC juu ya kumwomba tena kwa mkopo mshambuliaji huyo wakati msimu uliopita unaendelea.

Kusubiri hadi msimu umalizike maana yake ilijiweka katika mazingira ya presha kwa vile muda huo Wydad walikuwa na machaguo ya sehemu nyingi za kumpeleka na wakapata hela.

Mara ya pili wakarudia kosa la kuleta mazoea kwa kutolipa kwa wakati malipo ya Wydad waliyokubaliana huku wakimtangaza Mwalimu. Labda waliona mchezaji na klabu inayommiliki hawatoweza kubadili uelekeo.

Baada ya Wydad kukasirika na kumrudisha Morocco mchezaji wao, Simba ilipaswa kujifunza kwa kosa lililotokea mwanzo lakini ikawa tofauti kwani ikajikuta inamtambulisha huku ikiwa haijamalizana na Wydad.

Mwishowe wamekutana na pigo ambalo labda litawapa darasa kwa siku za usoni na wasirudie tena kufanya mambo kwa mazoea.