Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jota alivyokutana na mkewe maktaba ya sekondari

MKE Pict

LIVERPOOL, ENGLAND: BARABARA iliyomuua Diogo Jota ni hatari sana na kumekuwa na ajali za kutisha, kwa mujibu wa maelezo ya madereva na maofisa usalama wa wanaoishi eneo hilo.


Kuna kona kali na barabara iliyolala upande mmoja, mashimo makubwa barabarani ambayo yamekuwa majanga makubwa kwa madereva, akiwamo Jota na mdogo wake, Andre, 25.


Staa huyo wa Liverpool, Jota, 28, alifariki dunia usiku wa Jumatano baada ya tairi ya gari lake Lamborghini kupasuka na kusababisha gari hiyo kutoka barabarani na kuwaka moto. Ndugu hao wawili walikuwa wakipita huko Zamora, Hispania katika barabara ya A-52 kuelekea Santander, ili kuwahi kivuko cha kuwapeleka Uingereza.

Ofisa mmoja wa serikali huko Zamora alisema A-52 ni habari sana. Na chanzo kingine kilibainisha kwamba kenye aneo ambalo Jota alipata ajali barabara yake kuna kona na inaruhusu mwendokasi wa kilomita 120 kwa saa. Kinachoelezwa ni kwamba ajali nyingi sana zimekuwa zikitokea eneo hilo.

MK 01

Kitu kingine ukiweka kando mashimo, barabara hiyo pia kumekuwa na wanyama wanaokatiza.

Lililotokea limetokea, lakini Jota ameondoka na kuachana mrembo matata kabisa, Rute Cardoso, aliyefunga naye pingu za maisha hivi karibuni na wawili hao, wakiwa na familia changa.

Jota na mrembo Rute kwa mara ya kwanza walikutana kwenye maktaba ya vitabu wakiwa sekondari na katika kipindi cha miaka 13 waliyokuwa pamoja, wametengeneza uhusiano mkubwa wa kirafiki kuliko wa kuwa wapenzi. Jota hakuwa mtu wa kujionyesha, wakati mrembo Rute alikuwa na ndoto za siku moja kuja kuanza masomo ya shahada ya masoko, ambayo tayari ameshajidahili.

MK 02

Lakini, sasa ndoto ya wawili hao, Jota na Rute imezimika kama mshumaa kwenye upepo, mmoja akitangulia mbele ya haki. Baada ya harusi yao, wenyewe walianza kupostiana kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii hasa ule wa Instagramu.

Picha zao zinaaonyesha eneo alilofungia ndoa yao kwenye kanisa moja ya Katoliki karibu na Mto Douro uliopo huko Porto, Juni, ambapo ni siku chache tu zilizopita. Hivyo, kifo cha Joto ni pigo kubwa sana kwa mrembo Rute.

Uhusiano wa Jota na mrembo Rute ulianza wakiwa bado watoto kabisa, huku mrembo huyo kupitia picha alizokuwa akimposti mtu, ambaye alimtambulisha kama penzi la maisha yake, aliweka na maelezo. 'Que lindinho!' kwa lugha ya kimombo 'How cute!' akijaribu kumwelekezea kipenzi chake.

MK 03

Harusi yao ilikuwa yenye mvuto mkubwa na kuvutia wengi, wakati wapendanao wa muda mrefu, waliofanikiwa kupata watoto pamoja walipoamua kufunga pingu za maisha.

Wakati Jota alipokutana na mke wake mtarajiwa mwaka 2012 akiwa sekondari Gondomar, mji uliopo mashariki mwa Porto, unaofahamika zaidi kwa uhunzi, alikuwa mwenye kujiamini na kujieleza vyema kwa mrembo, ambaye kwa kipindi hicho Rute alikuwa akitokea Jovim, maili chache magharibi karibu na Douro.

Walikuwa daraja moja, ambapo mrembo Rute anafichua Jota alikuwa akifanya mambo yote, kusoma na pia kufanya mambo mengine kabla ya kuingia kwenye mchezo wa soka.

"Alipata alama nzuri, lakini bila ya kusoma sana." alisema mrembo Rute akimzungumzia Jota.

MK 04

Kinachoelezwa ni kwamba mrembo Rute, ndiye aliyekuwa kichocheo za Jota kufanya uamuzi mgumu wa kuhama kutoka Porto hadi Pacos de Ferreira na baadaye Atletico Madrid, kipindi hicho alipokuwa a  umri wa miaka 19 na walihama pamoja na mpenzi wake.

"Diogo alikuwa na ndoto hii, lakini tulipaswa kufanya kitu kimoja baada ya kingine. Hakuwa mjivuni, alibaki kuwa mtu yuleyule," alisema mrembo Rute.

Mrembo Rute anafahamu kila kitu kuhusu mpenzi wake kwamba alikataliwa na timu za Benfica na Porto, ambapo aliamua kwenye klabu ya mtaani ya Gondomar Sport Clube, ambako alifunga mabao 38 kwa msimu mmoja, huku akifanya mazoezi kwenye mashamba ya familia, alikokuwa akigombana na wazazi wake kutokana na kuharibu mazao.

Mrembo Rute aliomba nafasi ya masomo kusomea shahada ya masoko katika Chuo Kikuu cha Mirandela, kaskazini mwa Ureno, lakini alisubiri kuona ni kitu gani kitatokea kwa Jota katika maisha yake ya soka.

MK 05

Hakufahamu kama vitu vingekwenda kwa haraka hivyo na kumshuhudia Jota akihamia kwa mkopo Wolverhampton Wanderers mwaka 2017 baada ya kurejea Ureno kuichezea Porto na mambo kushindwa kwenda sawa. Na mwaka 2020, alijiunga na Liverpool ambapo sasa maisha yake ya soka yakawa juu.

Na kwa mapito yote hayo, mrembo Rute amekuwa akimsapoti mpenzi wake huyo kwenye kila timu anayokwenda kwa sababu wamekuwa pamoja kwenye kupanda na kushuka, wakipambana pamoja.

Wamekuwa wakazi wa Livepool na kupata watoto wao hao, wa kwanza Denis na kisha binti yao Duarte.

Na kuhusu familia yake, Jota alisema:  "Utahitaji kuwa baba bora kwa kadri unavyoweza."

Jota alisema kwamba mkewe ndiye nguzo imara kwenye ustawi wa familia yao changa.

Bila shaka kifo hicho cha ghafla cha Joto, kimeacha simanzi kubwa sana kwa mrembo Rute.

Kifo hicho pia kimeanza sinamzi kubwa kwa umma wa wapenda soka, kama ambavyo ilivyowahi kutokea kwa wanasoka wengine waliopoteza maisha ajalini, akiwamo staa wa zamani wa Arsenal na Real Madrid, Antonio Reyes. Jota atazikwa, leo, Jumamosi.