Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KEVIN HART; Komediani mwenye pesa zake

ATM Pict

Muktasari:

  • Mbali na mafanikio aliyonayo ya kisanii gumzo kubwa lilikuwa juu ya kiasi kikubwa cha utajiri ambacho staa huyo amejijengea kupitia filamu, vichekesho, biashara na matangazo.

LOS ANGELES, MAREKANI: WIKIENDI iliyopita jina la Kevin Hart lilitikisa tena mitandaoni baada ya kampuni anayomiliki ya uzalishaji ya Hartbeat kutajwa kuwa moja ya taasisi za burudani zinazokua kwa kasi zaidi Marekani.

Mbali na mafanikio aliyonayo ya kisanii gumzo kubwa lilikuwa juu ya kiasi kikubwa cha utajiri ambacho staa huyo amejijengea kupitia filamu, vichekesho, biashara na matangazo.

Kevin, aliyeanza kama mchekeshaji wa ‘stand-up comedy’, leo hii ni miongoni mwa wasanii tajiri zaidi duniani. Je anapigaje mwanja? Msome hapa ujue undani.

AT 03

ANAPIGAJE PESA

Kwa sasa utajiri wa Kevin Hart unaokadiriwa kufikia zaidi ya Dola 450 milioni umetokana na dili mbalimbali.

Kwanza ni kupitia filamu ambako hupata kati ya Dola 10 hadi 20 milioni kwa filamu moja.

Pia anapata pesa kupitia vipindi vya stand-up comedy ambako ndiko anaonekana kupatia umaarufu na pesa zaidi.

Amekuwa akilipwa pia kwa kuandaa shoo za kuchekesha kwa kushirikiana na kampuni ya Netflix ambayo humlipa hadi Dola 15 milioni.

Anamiliki kampuni ya uandaaji wa matamasha ya kuchekesha na filamu iitwayo Hartbeat & Laugh Out Loud Studios.

Mbali ya yote hayo jamaa ni balozi wa kampuni kibao ikiwamo Nike, Chase Bank, Tommy John (nguo za ndani), Hydrow Fitness, DraftKings ambazo kwa mwaka humpa mkwanja wa takriban Dola 25 milioni.

Mwaka 2023 alitajwa na jarida la Forbes kuwa mmoja wa wasanii wanaolipwa zaidi duniani akivuna Dola 60 milioni kwa mwaka mmoja

AT 05

MIJENGO

Nyumba anayoishi kwa sasa ipo eneo ya Calabasas huko California yenye thamani ya takribani Dola  12 milioni, ambayo ndani yake ina eneo la kufanyia mazoezi, bwawa kubwa la kuogelea na bustani ya kifahari.

Pia ana nyumba huko Encino, aliyoinunua kwa ajili ya kupangisha, ina thamani ya Dola 7 milioni.

Vilevile anamiliki eneo  kubwa la ardhi lililopo Calabasas alilolinunua kwa Dola 5 milioni.

AT 04

MSAADA KWA JAMII

Mara nyingi Kevin Hart hutoa misaada kupitia taasisi ya Help From The Hart Charity, ambayo husaidia kusomesha kwa watoto kutoka familia duni, kutoa ufadhili wa masomo, kusaidia waathirika wa majanga ya asili kama vimbunga na mafuriko.

Mwaka 2022, alitoa zaidi ya Dola 1 milioni kama Scholarship kusaidia wanafunzi wa masomo ya sayansi.

AT 02

FAMILIA NA BATA

Hart yupo katika ndoa na Eniko Parrish na wamejaliwa kupata watoto  watoto wawili ambao ni Kenzo na Kaori.

Pia ana watoto wawili wengine aliowapata na aliyekuwa mke wake wa kwanza, Torrei Hart ambao ni Heaven na Hendrix.

Inaelezwa Hart ni mtu anayependa kutumia muda mwingi na familia pamoja na kufanya mazoezi.