Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jinsi ya kuondoa kitambi bila kwenda GYM

Muktasari:

  • Hii ni kwasababu milli ya wachezaji kandakanda ina hekaheka nyingi zinazoufanya mwili na viungo vyake kutumia nishati nyingi ya mwili ikiwamo mafuta ya ziada kama vile ya kiriba tumbo.

KATIKA maisha ya kila siku ni kawaida kwa watazamaji kuwaona wakiwa viwanjani wakiwa na viriba tumbo, ila ni vigumu sana kuwaona wachezaji wakiwa na viriba tumbo.

Hii ni kwasababu milli ya wachezaji kandakanda ina hekaheka nyingi zinazoufanya mwili na viungo vyake kutumia nishati nyingi ya mwili ikiwamo mafuta ya ziada kama vile ya kiriba tumbo.

Mtazamaji wakila siku anayependa kutazama burudani ya soka anakuwa katika hatari ya kupata unene wenye kuambatana na kiriba tumbo endapo kama si mfanyaji wa mazoezi ya mara kwa mara.

Leo jicho la kitabibu litaangazia kiriba tumbo kwa upande wa watazamaji, tatizo hili ni kiashiria cha unene uliokithiri. Endapo mtazamaji utafanikiwa kukifuta kiriba tumbo basi hata jezi anazovaa za timu yake zitaweza kumpendeza.

Njia zakuondoa kiriba tumbo

Kiriba tumbo au kwa jina lingine kitambi au kwa vijana wakisasa hukiita “futa’ na kule wakijiweni wanakiita kifutio cha simu janja kutokana na tabia ya watu wenye maumbo hayo kutumia eneo hilo kuzisafisha.

Uwepo wa kitambi mwilini ni kiashiria kimojawapo cha unene na ndiyo maana wataalam wa afya hupima mzunguko wake kama moja ya njia ya kutathimini tatizo la unene.

Kiriba tumbo ni matokeo ya ulaji holela wa vyakula na kutoushughulisha mwili na mazoezi au kazi zinazoutembeza mwili.

Utitiri huu wa majina ni ishara inayotupa ujumbe kuwa kitu hiki si cha kawaida na niwajibu kukabiliana nacho. Lakini je unakiondoa vipi kiriba tumbo?

Jibu ni rahisi, ni kufanya mazoezi mepesi na udhibiti wa ulaji holela wa vyakula hasa vinavyonenepesha ambavyo ni pamoja na vyakula vyenye mafuta mengi, sukari na wanga nyingi.

Ulaji wa vyakula visivyokobolewa mfano mikate ya ata ambayo unapoila humfanya mtu kujisikia kuwa ameshiba lakini na pia uwepo mashudu ambayo huwa hayana wanga yapo kuongeza ujazo tu.

Hivyo husaidia kumpunguzia wanga ambayo inachangia kunenepa na kupata kitambi. Vile vile ulaji wa vyakula vya mboga mboga hasa zile mbichi ni mtindo mzuri pia kukabiliana na kitambi.

Pale unapoitazama sahani yako yenye mduara wa nyuzi 360  ya mlo mkuu iwe na chakula robo wanga, robo protini na nusu iwe ni mboga mboga na matunda.

Utahitaji kuwa na mwenendo na mtindo bora wakimaisha kwa kutenga muda mwingi wa mazoezi mepesi ambayo yanahitaji dakika 150 kwa wiki yaani sawa na dakika 30 kwa siku katika siku 5 za wiki.

Kwa wenye vitambi ambao ni wapiga maji ambao tayari wana vitambi ni muhimu kuacha au akishindwa apunguze kiasi cha bia anazokunywa angalau kuwa mnywaji wa mwishoni mwa wiki na sio kila siku.

Kwa upande wa mazoezi si kila zoezi lina matokeo makubwa katika kudhibiti kiriba tumbo. Yapo mazoezi ambayo huitaji kwenda vituo vya mazoezi ambayo yanaonesha kuwa na matokeo makubwa katika kudhibiti kitambi. Mazoezi mepesi yanasaidia kuufanya mwili kushughulisha viungo vingi hivyo kuchoma mafuta yaliyorundikana ikiwamo katika eneo la kitambi.

Lakini inashauriwa ili kuweza kuchoma mafuta ya ziada ni pale utakafanya mazoezi mepesi kwa muda wa dakika 30 kuendelea.

Ni muhimu kabla ya mazoezi yoyote lazima mwili uandaliwe kwa mazoezi ya viungo kwanza ili kuuweka utayari wa viungo kufanya mazoezi kwa ufanisi.

Zoezi la kukimbia kidogo kidogo ni zoezi zuri ambalo linaweza kuwafaa vijana zaidi.

Watu wazima pengine kukimbia ni changamoto wanaweza kufanya zoezi la kutembea lakini kwa mtindo wa kutupa mikono kama vile watembeavyo askari.

Mtindo huo husaidia kushughulisha maeneo mengi ya mwili ikiwamo misuli ya eneo la tumboni.

Kuruka kamba ni moja ya zoezi rahisi lenye matokeo makubwa katika kukabiliana na kiriba tumbo. Tafiti zinaonyesha zoezi hili likifanywa kwa ufanisi linasaidia kupunguza tatizo hili kwa haraka.

Zoezi lingine ni kuogelea pale unapofanya zoezi hili linahusisha utendaji wa misuli mingi ikiwamo ile ya tumboni.

Ili kuweza kukabiliana na tatizo hili kwa umaridadi zaidi inahitaji pia kufanya mazoezi yanayolenga moja kwa moja kuishughulisha misuli ya tumboni ambayo utayafanya ukiwa umetulia.

Ili kuleta matokeo chanya zaidi mazoezi mepesi yanaweza kuchanganywa na mazoezi ya viungo ambayo yanalenga kuishughulisha misuli ya tumboni.

Pia tumia mbinu ya kutumia muda mwingi na mara kwa kwa kukaza misuli yako ya tumbo hata unapokuwa katika kazi zako za kila siku inasaidia kuishughulisha misuli ya tumbo.

Unaweza kutumia dakika 30-60 kufanya mazoezi mepesi na dakika 10 mazoezi ya moja kwa moja ya tumboni. Baada ya mazoezi yoyote muhimu pia kutumia dakika 5 za mazoezi ya kuupoza mwili. Unaweza kuitumia simu janja yako kupakua video mbalimbali zinazoonyesha aina hiyo ya mazoezi haya yakuondoa kitambi au kupakua apps yenye mazoezi hayo ili kukupa ufahamu zaidi.