Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jicho la tatu pingamizi la Yanga kwa Karia

PUMZI Pict

JUMAMOSI ya Juni 28, saa 9:30 alasiri, mabingwa wapya wa soka nchini, Yanga waliwasilisha pingamizi lao dhidi ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia likiwa limesainiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Andre Ntine.


Katika pingamizi hilo Yanga inaitaka Kamati ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti Wakili Kilomoni Kibamba kumuondoa Karia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo ikiwa na hoja kuu tatu:


1. Matumizi mabaya ya madaraka kwa kuchukua endorsement (dhamana) 46 kati ya 47

2. Kuanza kampeni kabla ya muda kwa kukusanya endorsement 46 kabla ya tangazo la uchaguzi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

3. Inapinga Karia kugombea mara ya tatu ikisema ni kinyume cha sera ya michezo nchini, ambayo inataka vyama vya michezo viongozi wake kukaa madarakani kwa vipindi 3 vya miaka mitatu mitatu au vipindi 2 vya miaka minne minne.

PUM 01

HOJA DHAIFU

Ukiziangalia hoja hizi kwa jicho la kitaalamu utaona kabisa Yanga imepaniki...lakini hoja zake hazina mashiko hata kidogo. MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA & KUANZA KAMPENI MAPEMA.

Desemba 21, 2025 katika mkutano mkuu wa TFF uliofanyika mjini Moshi, wanachama wa TFF kwa hiyari yao walipitisha Azimio la Mkutano Mkuu kwa pamoja kumuunga Mkono Rais Karia kugombea tena nafasi hiyo ya urais wa shirikisho hilo.

Kila mmoja na kwa pamoja walikubaliana kutoa endorsements kwa Wallace Karia wakiongozwa na matamko ya Murtaza Mangungu (Mwenyekiti wa Simba) na Injinia Hersi Saidi (Rais wa Yanga).

Kwa hatua ile ikawa dhahiri kuwa, ENDORSEMENTS nyingi kati ya 47 zinaweza kwenda kumthibitisha Wallace Karia kugombea kama takwa na Azimio rasmi la Mkutano Mkuu wa TFF. Halafu leo Yanga inamtuhumu Karia kutumia vibaya madaraka kwa kuchukua dhamana (endorsement) zote, ilhali yenyewe imempa na hata Rais wake alikuwa mmoja wa watu waliosimama kwenye mkutano ule kuahidi endorsement kwa Karia.

PUM 02

UFAFANUZI

Dhamana hutolewa na washirika wanaounda TFF, ambao wako 47. Washirika hao ambao kwa jina rasmi huitwa WANACHAMA, ni kama ifuatavyo:

1. Vyama shiriki - 5 (TWFA, TAFCA, SPUTANZA, FRAT, TASMA)

2. Timu za Ligi Kuu - 16

3. Vyama vya Mikoa - 26

PUM 03

5+16+26=47.

Kila mwanachama katika hawa, anapaswa kutoa endorsement moja kwa mgombea mmoja kwa kila nafasi inayogombewa.

Aidha, Katiba ya TFF na kanuni za uchaguzi hazitaji muda rasmi wa endossement, hivyo zinaweza kutolewa wakati wowote, na hakuna idadi ya mwisho...ipo ya kwanza tu ambayo ni tano.

Yanga walikuwepo katika mkutano ule wa Moshi na walitoa endorsement yao pale sambamba na wajumbe wengine wote 47...leo kuja kulalamika ni muendelezo wa matatizo yao ya Idara ya Sheria.

PUM 04

KUGOMBEA MARA YA TATU

Katiba ya TFF tangu enzi za FAT haikuwa na ukomo wa vipindi vya uongozi, hadi alipoingia Karia mwaka 2017.

Yeye ndiye aliyebadilisha katiba na kuweka ukomo wa muda wa uongozi kuwa vipindi viwili. Lakini mabadiliko haya yalikuja baada ya kumaliza muhula wake wa kwanza wa 2017 - 2021.

Kwa maana rahisi ni kwamba yale mabadiliko hayahesabu ule muhula wa kwanza...yanaanzia kutumika katika muhula wa pili wa 2021-2025.

Hivyo kile kipindi cha Karia cha kuanzia 2017-2021 kinahukumiwa na katiba ya zamani ambayo haikuwa na ukomo.

Kipindi cha pili cha kuanzia 2021-2025, ndicho kinachohukumiwa na katiba mpya...kwa hiyo kinahesabika kama cha kwanza kwa Karia.

Hivyo katiba ya sasa inamtambua Karia kama Rais wa TFF kwa kipindi kimoja, na anaruhusiwa kugombea tena kipindi cha pili patika uchaguzi huu. Sio kwamba Yanga hawakuliona hili...ambalo ni jambo lililo wazi na dhahiri, ila wana vita yao wanapigana.

Ilitarajiwa kwamba Yanga, lazima ifanye kila inaloweza ili kuuondoa kabisa utawala wa Karia madarakani kwa sababu utawaletea tabu msimu ujao ukibaki.

Vurugu walizofanya Yanga katika sakata la mechi ya watani zimewatengenezea uadui mkubwa sana na TFF.

Yanga walijinasibu wakati ule kwamba wanapigania kanuni za mpira, lakini nafsini mwao wanajua kabisa kwamba wao ni kati ya wavunjaji wakuu wa kanuni hizo na TFF hii imekuwa ikiwalea.

Ushahidi mkubwa kabisa ni usajili wa Twisila Kisinda mwaka 2022 ambao ulifanyika nje ya utaratibu. Yanga ilimsaini Lazarous Kambole, Mzambia aliyekuwa akicheza Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. Lakini kabla dirisha halijafungwa ikabaini kwamba ana majeraha makubwa yatakayomuweka nje kwa zaidi ya miezi sita.

Ikataka kumkata ili imsajili Kisinda kuchukua nafasi ya Kambole. Lakini kiutaratibu, mchezaji anayesajiliwa kwenye dirisha moja la usajili, haruhusiwi kukatwa...labda auzwe kwenda timu nyingine.

Kwa majeraha ya Kambole asingeweza kuuzwa...lakini TFF ikaisaidia kuvunja kanuni ili ifanikishe hilo. Wakati ule TFF ya Karia na Yanga zilikuwa na uhusiano mzuri sana...lakini kwa mtafaruku wa sasa, maisha yatakuwa magumu sana. Ndio maana Yanga wanataka kuhakikisha wanasafisha nyumba ili mambo yasiwe mengi.

Huenda hofu yao ni kwamba, Karia akibaki madarakani, pamoja na Katibu Mkuu, Kidao Wilfred, maisha ya Yanga yatakuwa magumu sana msimu ujao na wakati wote watakaokuwa madarakani. Lakini ni bahati mbaya sana kwao kwamba wamechelewa sana kwa sasa. Ngoja tuone!