Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JACKIE CHAN: Fundi aliyegoma kuacha pesa

ATM Pict

Muktasari:

  • Hivi karibuni aliachia muvi yake nyingine iitwayo The Shadow's Edge ambayo inaoneakana kupokewa vizuri kuanzia barani Asia na hata sehemu nyingine duniani.

HONG KONG, CHINA: AKIWA na umri wa miaka 71, ambao watu wengi walitegemea kuona akipumzika baada ya kutumika kwa muda mrefu katika kiwanda cha uigizaji wa filamu na kutengeneza utajiri mkubwa, Jackie Chan ameendelea kuachia vitu siku hadi siku akigoma kabisa kustaafu.

Hivi karibuni aliachia muvi yake nyingine iitwayo The Shadow's Edge ambayo inaoneakana kupokewa vizuri kuanzia barani Asia na hata sehemu nyingine duniani.

Achana na burudani ambayo anaitoa, kugoma kustaafu kwa Jackie Chan kunamfanya kuendelea kutajirika siku hadi siku kutokana na mkwanja wa maana anaoupata kupitia filamu pamoja na biashara zake. Leo tumekusogezea ATM yake inavyojaa noti kwa kuangalia utajiri alionao na jinsi anavyopiga pesa.

AT 05

ANAPIGAJE PESA
Jackie Chan ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 400 milioni. Sehemu kubwa ya utajiri huo umetokana na mapato na mauzo ya filamu, ubalozi wa kampuni mbalimbali na faida za kampuni anazomiliki.

Kwanza kabisa staa huyu ana kampuni yake iitwayo JC Group inayojihusisha na uzalishaji wa filamu, usimamizi wa wasanii, miradi ya hoteli na migahawa, bidhaa za urembo na mavazi.
Kimsingi kampuni hii ndio injini ya utajiri wake na kwa mwaka humpa zaidi ya Dola 50 milioni kama faida.

Mwigizaji huyu pia anapata pesa kupitia ubalozi wake wa kampuni mbalimbali kama Adidas, Emirates Airlines, Canon na Wuling Motors ambazo kwa mwaka humwingizia zaidi ya Dola 20 milioni.

Jackie Chan pia anamiliki mtandao mkubwa wa majumba ya sinema zaidi ya 70 huko China na Hong Kong kupitia kampuni yake ya Jackie Chan Cinema.


AT 04

NYUMBA
Anamiliki nyumba za kifahari huko China, Hong Kong na Marekani zenye thamani ya zaidi ya Dola 35 milioni.

Maeneo ya Beverly Hills, Marekani ana nyumba ya kifahari yenye thamani ya Dola 10 milioni pia anazo nyingine mbili nyingine zilizopo Beijing, China zenye thamani ya Dola 12 milioni.

Kule Hong Kong ana nyumba yake iliyopo maeneo ya Mlimani yenye thamani ya Dola 8 milioni.


AT 01

MSAADA KWA JAMII
Kupitia Jackie Chan Charitable Foundation iliyoanzishwa 1988, Chan amekuwa mmoja wa watu waliotoa misaada mingi zaidi barani Asia.

Taasisi yake imekuwa ikitoa misaada wakati wa maafa, bima za afya kwa watoto maskini, ujenzi wa shule zaidi ya 20 China, fedha za matibabu kwa wagonjwa wasiojiweza katika bara zima la Asia.


AT 02

NDEGE
Jackie Chan ni mmoja wa wasanii wachache barani Asia wanaomiliki ndege binafsi. Ana ndege aina ya Embraer Legacy 650 ambayo ina thamani ya Dola 30 milioni.

Alipata ndege hiyo aliposaini mkataba kama balozi wa ndege za Embraer.


AT 03

 NDINGA
Bugatti Veyron - Dola 1.2 milioni 
Lamborghini Aventador - Dola 500,000
Bentley Mulsanne - Dola 310,000
Rolls-Royce Phantom - Dola 450,000
Mitsubishi 3000GT Spyder - Dola 51,000


MAISHA NA BATA
Jackie Chan sio mtu wa bata sana, lakini mara kadhaa ameonekana akiwa na familia yake sehemu za starehe. Yupo katika ndoa na Joan Lin na wamebarikiwa watoto wawili, mmoja wa kiume ambaye ndio mkubwa na mdogo wa kike.

Staa huyu muda mwingi huutumia katika biashara zake, uzalishaji wa filamu na shughuli za kijamii.