Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibenge apindua meza Azam FC

PUMZI Pict


MSIMU uliopita, 2025/26, kocha wa Azam FC, Florent Ibenge aliweka rekodi kadhaa ndani ya klabu hiyo nzuri na mbaya pia.


Kwanza kufuzu hatua ya makundi ya mashindano ya Afrika kitu ambacho Azam FC iliteseka nacho kwa miaka mingi.


Pili kumaliza msimu mzima bila kuruhusu hata bao moja katika uwanja wa nyumbani.

Hii haikuwa tu rekodi ya Azam FC, bali nchi kwa ujumla. Haijawahi kutokea timu kwenye historia ya Ligi Kuu Bara kumaliza msimu mzima bila kuruhusu hata bao moja katika uwanja wa nyumbani.

Msimu huu wa 2026/27 ukiwa katika mzunguko wa tatu tayari Ibenge ameweka rekodi nyingine.

Safari hii Mfaransa huyo mwenye asili ya DR Congo anakuwa kocha wa kwanza katika historia ya Azam FC kufikisha mechi zaidi ya moja ya msimu mpya baada ya kumaliza msimu uliotangulia.

Hapa labda nitoe ufafanuzi kidogo.

Azam FC ambayo ilipanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara 2008 imeshakuwa chini ya makocha 18 ambao ni pamoja na Neidar Dos Santos - Brazil (2008-2009), Itamar Amorin - Brazil (2009-2010), Stewart Hall - England (2010 - 2012), Boris Bunjak - Serbia (2012), Stewart Hall - England (2012-2013) na Joseph Omog - Cameroon (2014-2015).

Wengine ni Stewart Hall - England (2015-2016), Zeben Fernandes - Hispania (2016), Aristica Cioaba - Romania (2017-2018), Hans van der Pluijm - Uholanzi (2018-2019), Etienne Ndayiragije - Burundi (2019), Aristica Cioaba - Romania (2019-2020), George Lwandamina - Zambia (2020-2021) na  Abdihamid Moallin - Marekani (2021-2022).

Pia wapo kina Dennis Lavagne - Ufaransa (2022), Kali Ongala - England (2022-2023), Yousouph Dabo - Senegal (2023-2024), Rachid Taoussi (2024-2025) na Florent Ibenge (2025 -).

Katika orodha hii ndefu ya makocha, Ibenge anakuwa kocha wa tatu kuanza msimu na kumaliza bila kufukuzwa katikati.

Lakini hata hivyo, Ibenge amewavuka hao wengine kwa kuwa kocha wa kwanza kuuanza msimu mpya na kucheza mechi tatu.

PUM 03

STEWART JOHN HALL

Hall ambaye alianza na kumaliza salama msimu wa 2011/12 hakupata hata nafasi ya kucheza mechi moja ya ligi ya msimu mpya wa 2012/13.

Alifukuzwa baada ya fainali ya Kombe la Kagame 2012, kwa ukaidi dhidi ya waajiri wake.

Aliambiwa asimpange Mrisho Ngassa kwenye fainali dhidi ya Yanga kwa sababu mchezaji huyo aliibusu jezi ya Yanga aliyopewa na mashabiki wa timu hiyo kwenye nusu fainali.

Hall akakaidi maagizo, akampanga Azam FC ikafungwa na yeye akafukuzwa kabla ya msimu mpya wa ligi wa 2012/13 haujaanza.

PUM 02

YOUSOUPH DABO

Raia huyo wa Senegal alianza na kumaliza salama msimu wa 2023/24 lakini akafukuzwa msimu mpya wa 2024/25 baada ya mechi moja tu ya ligi.

Ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, iliyoisha kwa suluhu.

Kufukuzwa kwake kulichangiwa na mambo mengi, ikiwemo kufungwa 4-1 na Yanga kwenye fainali ya Ngao ya Jamii huku akitumia mfumo ambao haikuwahi kuitumia kabla.

Waajiri wake wakahoji kwanini atumie mfumo ambao hajawahi kuitumia, kwenye mchezo dhidi ya timu kubwa kama Yanga.

Kama alitaka kujaribu mfumo mpya kwanini hakuufanyia kazi kwenye kambi ya maandalizi ya msimu mpya au angesubiri mechi ndogo huko mbele.

Mechi hii ilifuatana sana na mechi za awali za Ligi ya Mabingwa ambayo Azam FC walipangwa na APR ya Rwanda.

Waajiri wake wakaona wasije wakaharibu msimu kwa kumuondoa kocha kuelekea mechi hizo muhimu.

Hata hivyo, bado Azam FC ikafungwa na kutolewa na APR...na waliporudi ndio ukaja mchezo wa JKT...Dabo akafukuzwa.

PUM 01

FLORENT IBENGE

Ibenge alianza na kuumaliza salama msimu wa 2025/26. Tofauti na wenzake, yeye amefanikiwa kuuanza tena msimu mpya wa 2026/27 na sasa amefikisha mechi tatu. Hii ndio rekodi ambayo Ibenge ameweka ndani ya klabu hiyo. Hofu ilikuwa kubwa baada ya sare ya 1-1 na Polisi Tanzania kwenye mchezo wa kwanza wa msimu mpya.

Presha ikawa kwamba endapo mchezo wa pili dhidi ya TRA United wasingeshinda labda maamuzi magumu yangechukuliwa.

Lakini wakashinda 2-1 na pia wakashinda tena 2-1 mchezo uliofuata dhidi ya Pamba. Na sasa anajiandaa kucheza mchezo wa nne, dhidi ya Geita Gold kule Bukombe.

Yawezekana Ibenge akawa kocha wa kwanza wa Azam FC kumaliza misimu miwili mfululizo, endapo atatoboa.