Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hiki ndo anachofanya Juma Pondamali sasa

Muktasari:

  • Mwanaspoti limefanya mahojiano na Pondamali, ambaye anaelezea maisha yake ya sasa na zamani, pamoja na kile anachokiona kinafanywa na makipa wazawa na wageni katika Ligi Kuu Bara.

WAHENGA hawakukosea kusema jungu kuu halikosi ukoko, ndicho kinachotakiwa kufanywa na kizazi cha Gen Z katika mpira wa miguu, kuendelea kujifunza kwa kocha mkongwe wa makipa, Juma Pondamali.

Mwanaspoti limefanya mahojiano na Pondamali, ambaye anaelezea maisha yake ya sasa na zamani, pamoja na kile anachokiona kinafanywa na makipa wazawa na wageni katika Ligi Kuu Bara.

ANAFANYA NINI KWA SASA

Akizungumzia kile anachofanya sasa, kipa huyo wa zamani anasema “natambua watu wengi wanajiuliza nipo wapi kwa sasa kutokana na ukimya wangu wa muda mrefu, kwani sijafundisha timu yoyote ya Ligi Kuu takribani miaka minne.

“Kwa sasa nasimamia kituo cha kukuza vipaji vya vijana wanasoka kinachoitwa Garden, kipo Kinondoni. Tunaandaa magolikipa watakaokuwa na viwango vya juu vitakavyolinufaisha taifa la Tanzania.”

Anasema kituo hicho kina zaidi ya magolikipa 20, huku wachezaji wa ndani wakiwa takribani 60, ambao wanajengwa kucheza soka la kisasa na kuendana na viwango sawa na wageni wanaokuja kucheza nchini.

“Lakini ligi zikisimama kuna wachezaji wengi wanakuja kufanya mazoezi, hivyo vijana wanapochanganyika na watu wazima linakuwa jambo linalowajengea kujiamini zaidi na kuamini ndoto zao zitakuwa halisi, kwa kuwaona mastaa ana kwa ana,”  anasema na kuongeza:

“Mazoezi ya makipa yanaanza saa 12:30 asubuhi hadi saa 2:00. Kuanzia saa 2:00 inachezwa mechi hadi saa 6:00. Kila mchezaji anapata dakika 20 za kucheza, lengo ni kila mchezaji ajisikie ana haki ya kuwepo katika kituo hicho.

“Katika kituo hicho tupo makocha wanne wa magolikipa, ingawa nasimama kama mshauri wa kiufundi, kuhakikisha wanaelekezwa makipa namna ya kusimama mipira ya hatari inapokuwa mbele yao. Kila mmoja hasimami ili mradi.”

Anasema ingawa yeye zamani alikuwa anacheza kwa mbwembwe, hawafundishi hivyo makipa hao, kwani wanahitaji kucheza kwa umakini na nidhamu ya juu.

“Uhuni hautakiwi kabisa kwenye mpira wa miguu, hilo lazima nisisitize kabisa. Ndiyo maana kuna aina wanatakiwa wainue miguu ili kutengeneza balansi ya mwili ili usilemewe upande mmoja.”

MAKIPA WAZAWA

Anasema kiwango cha makipa wazawa kipo chini kuliko cha wageni, jambo analoliona linahitaji kufanyiwa kazi na makocha wanaowafu ndisha, ili warejee kwenye ushindani kwa faida ya timu ya taifa.

“Kwa namna nilivyofuatilia mechi za Ligi Kuu, ninayemuona anacheza kwa kiwango kizuri ni kipa wa Yanga, Djigui Diarra. Anajiamini kwenye kuokoa, anaanzisha mashambulizi, kwa sababu nchini kwao Mali alikotokea alianza kucheza nafasi ya kiungo namba sita, hilo linamfanya awe mchezaji wa 13 ndani ya uwanja, ukiacha nafasi yake ya kukaa golin” anasema Pondamali na kuongeza:

“Makipa wetu wa ndani ni wachache ambao walianzia kucheza nafasi za ndani, ndiyo maana wanafanya makosa makubwa. Asilimia kubwa wengi wao wametokea kwenye ndondo, pamoja na hilo wanakuwa na nafasi ya kutengenezwa.

“Nitoe mfano hai wakati nafundisha Yanga, makipa wote walikuwa wanaitwa timu ya taifa. Kulikuwa na Ally Mustafa ‘Bartez’, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ramadhani Kabwili, aliyekuwa anaitwa timu za taifa za vijana, kwa sababu walijengwa katika misingi imara.”

Anasema kabla ya mechi alikuwa anamuandaa kipa mapema, akimweleza mechi ambazo anatakiwa kucheza na kumuonyesha kasoro zake, ili arekebishe mapema.

Pondamali anasema:”Inashangaza kuona linapigwa shuti mita 35 kipa anafungwa, maana wakati mwingine wanatoka eneo walilosimama bila hesabu. Lazima uibie hatua moja ukiusoma mpira una mwelekeo gani.”

Anaongeza: “Huwa nashangaa nikimuona kipa anashika kiuno badala ya kuwaonyesha washambuliaji kwamba wapo golini. Lazima ujitambulishe, mfano unaanza kurukaruka kuhakikisha unamchanganya awe anafikiria apige engo gani, siyo kuwapa urahisi wafungaji.”

Anasema alianza kucheza mpira akiwa na miaka 13, ilikuwa mwaka 1970, na akaja kuanza kupata nafasi mwaka 1976. Makocha hawakufanya haraka kumchezesha, bali walihakikisha anapata misingi sahihi. Baada ya kufikisha umri wa miaka 20 nika chaguliwa kuichezea timu ya taifa,” anasema na kuongeza:

Kinachochangia makipa wa sasa wasiwe na viwango vizuri, kocha anamfundisha kipa mwezi mmoja, halafu unataka acheze kwa kiwango kizuri. Lazima aive na aondolewe kasoro ndogondogo.”

HIVI HATAKI WACHEZAJI WAIGE

Anasema zamani kulikuwa hakuna mechi zilizoonyeshwa, tofauti na sasa, hivyo uhuni mwingi ulikuwa ukifanyika, ambao akiufanya mchezaji wa sasa ni rahisi timu yake kuigharimu.

“Zamani na sasa mambo ni tofauti. Kwanza mechi zilikuwa hazionyeshwi. Fikiria mimi nilikuwa nashuti mkono mmoja, nimedaka. Tulicheza Yanga dhidi ya Africa Sports, nikawa nampiga chenga mshambuliaji Victor Mkanwa, akaninyang’anya akanifunga bao. Hivyo dakika 90 zilimalizika kwa sare ya bao 1-1.

“Sasa Fred Felix Minziro alijua mimi ni mtata, hakuna anayeniweza, akawa aniuza kwa mashabiki ili wanipige. Kilichokuwa kimeniokoa ni mapolisi ambao waliwahi kuwahi, hivyo wakanipeleka hadi kwenye gari,”  anasema Pondamali na kuongeza:

“Nikamwambia kwa kuwa unaniuza kwa mashabiki, sasa usubiri tutakutana kambini. Siku hiyo hakutokea.

Ninachoweza kuwashauri makipa wa sasa waachane na mbwembwe ambazo zinaweza zikawagharimu. Mfano wafanye kosa kama langu, lazima wataonekana wameuza mechi, wakati mwingine inakuwa siyo kweli.

Unapomuuliza kwa nini watu walikuwa wanamuona mbabe? Pondamali anajibu akisema: “Nje na soka mimi nilijifunza kareti, kumfuu, ndiyo maana nawaambia vijana wa sasa, wasije wakaona mimi ni mzee wakanichezea na kuniona nimechoka, watakula kichapo hawataamini.”

Kipaji kingine alichonacho nyota huyo mkongwe wa soka ni mwanamuziki, akisema hadi sasa amefikisha nyimbo 40, akimtaja Peter Manyika (marehemu) kwamba wakati wa uhai wake alikuwa anashindana naye. Pia aliwahi kufanya kazi ya DJ.

Mbali na hilo, anaelezea namna ambavyo ilikuwa rahisi kumpata mwanamke wake wa kizungu, kwamba anajua kuzungumza Kiingereza.

“Nimefundisha Yanga nikiwa na makocha wa kigeni na timu ya taifa. Je, unadhani nilikuwa nazungumza nao lugha gani? Maana makocha wa kigeni ukisema mechi atadaka Dida, anakuliza kwa nini. Lazima utoe sababu.”anasema.

Anaongeza kuwa, “kwanza watu wanapaswa kujua CV yangu mimi inasemaje. Nina leseni ya FIFA na CAF, nilisoma Marekani, Brazil ilikuwa kozi ya mwezi mmoja.

“Kuhusu mke wangu ambaye kwa sasa anafanya kazi zake Arusha, nilikutana naye wakati nafanya shughuli zangu za DJ na miongoni mwa ma-DJ niliyokuwa nawakubali enzi hizo ni Jimmy Suma.

“Huyo Mzungu nimebahatika kupata naye watoto wawili, ila kwa ujumla nina watoto 12. Kuna mwingine anasoma sekondari, ana akili kubwa sana, jeshi limemchukua na kumsomesha, halafu yupo anayecheza mpira katika timu ya KMC.”