Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii ndo Endorsement ya Uchaguzi Mkuu TFF

UCHAGUZI Pict

Muktasari:

  • Uchaguzi huo wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 16 jijini Tanga kuhitimisha miaka minne ya uongozi wa sasa na zoezi la kuchukua na kurudisha fomu lilifanyika kati ya Juni 16-20 na jumla ya wagombea 25 wamejitosa kwenye kinyang'anyiro, wakiwamo sita wa nafasi ya Urais.

KIPYENGA cha Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kimeshapulizwa na kwa sasa mchakato wa uchaguzi huo upo hatua ya Mchujo kwa wagombea waliojitokeza kuwania nafasi saba za uongozi wa shirikisho hilo, ikiwamo moja ya Urais na sita za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.


Uchaguzi huo wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 16 jijini Tanga kuhitimisha miaka minne ya uongozi wa sasa na zoezi la kuchukua na kurudisha fomu lilifanyika kati ya Juni 16-20 na jumla ya wagombea 25 wamejitosa kwenye kinyang'anyiro, wakiwamo sita wa nafasi ya Urais.


Licha ya kwamba orodha kamili bado haijaanikwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, lakini baadhi ya wagombea hao sita wa nafasi ya Urais yupo anayetetea kiti, Wallace Karia, Dk Mshindo Msolla, Ally Mayay na Shija Richard, wakati kwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji inaelezwa ina wagombea 19 akiwamo nyota wa zamani wa Yanga, Ally Msigwa.

Wagombea hao wote kwa sasa wanasikilizia zoezi la mchujo wa awali wa kujua kama wamekidhi vigezo vya kuendelea kuwepo katika kinyang'anyiro hicho kabla ya kufanyiwa usaili na wakipenya hapo watakuwa na suala la kusikilizia pingamizi kisha kuruhusiwa kufanya kampeni.

Mchujo huo umeanza kufanyika juzi Jumamosi na utafungwa leo Jumatatu (Juni 21-23) kisha kesho Jumanne na Jumatano (juni 24-25) ndipo majina ya waliopenya hapo yatatangazwa na kuchapishwa.

Hata hivyo, siku ya kufungwa kwa zoezi la kuchukua na kurudisha fomu, kuna baadhi ya wagombea walikaririwa wakilalamikiwa kushindwa kupata wajumbe wa mkutano wa TFF wa kuwaidhinishia fomu zao (endorsement) kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa TFF ya mwaka 2021.

Suala la endorsement (udhamini) kwa fomu za ugombea ni moja ya vigezo muhimu za kuwapitia wanaowania uongozi kupata sifa ya kuendelea na mchakato, lipo kwenye kanuni hizo za TFF Ibara ya 10(3-4) kikieleza ni  vipi kwa wagombea wanaojitosa kwenye uchaguzi huo wa Shirikisho wafanye.

Hata hivyo, kumekuwa na sintofahamu juu ya suala la udhamini (endorsement) baadhi wakilalamikia kufanyiwa faulo na kuamini endorsement inawabeba zaidi wagombea waliopo ndani ya TFF kuliko walio nje na kuna waliotishia kukimbilia mahakamani na kamati nyingine za kisheria za TFF.

UCH 01

ENDORSEMENT NI NINI?

Kwa muktadha wa Uchaguzi Mkuu wa TFF, neno 'Endorsement' linamaanisha kuidhinishwa au kuungwa mkono rasmi kwa mgombea fulani kutoka kwa Wajumbe wanaoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo ambao ni 47.

Hii hutumika mara nyingi kuongeza heshima na mvuto kwa mgombea hasa kwa wapigakura na kwa mujibu wa Kanuni ya Uchaguzi wa TFF Ibara ya 10 kifungu cha 3-4 kimeainisha mgombea yeyote ni lazima apata endorsement isiyopungua wajumbe watano.

Vifungu hivyo vimeweka bayana; Mgombea wa Urais wa TFF lazima awe na barua tano za udhamini kutoka kwa wanachama wa TFF, huku kwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji kutoka kanda, lazima awe na barua ya udhamini kutoka Chama cha Soka cha Mkoa husika.

Mjumbe na Mwanachama hapaswi kumdhamini mgombea zaidi ya mmoja kwa nafasi moja  vinginevyo udhamini wote utakuwa batili.

Hii ina maana kila mgombea aliyechukua fomu katika Uchaguzi wa TFF ukiacha sifa nyingine zikiwamo Elimu na kadhalika ni lazima apate barua ya kuidhinishwa na wajumbe wasiopungua watano kati ya 47 wanaoshiriki uchaguzi mkuu wa TFF.

UCH 02

UGUMU UPO HAPA

Ibara hiyo ya 10 (3-4) imeweka wazi mjumbe mmoja kati ya wale 47 wa kuidhinisha mgombea, hapaswi kumuunga mkono zaidi ya mgombea mmoja, yaani mjumbe akimpendekeza mgombea A, hawezi tena kumuidhinisha au kumdhamini mgombea B hata kama ni rafiki yake.

Hata hivyo, kilichotokea kwa sasa ni karibu wajumbe 47 wa mkutano huo, inaelezwa walishaelekeza uungwaji mkono wao kwa mmoja wa wagombea, hivyo wengine wamekosa uidhinishwaji na kwa manaa hiyo, wagombea waliokwama wamekosa sifa za kuendelea na uchaguzi.

Kwa wanaokumbuka katika Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wajumbe wote zikiwamo klabu kubwa za Simba na Yanga zilitangaza kumuunga mkono Rais wa sasa wa shirikisho hilo, Wallace Karia, hii ikiwa na maana tayari milango ilishafungwa mapema kabla ya zoezi la uchaguzi huo uliofunguliwa Juni 16 na utaendelea hadi siku wa kupiga kura yaani Agosti 16.

Karia alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Rais wa TFF 2017 alipopata jumla ya kura 95 kati ya 128 zilizopigwa katika uchaguzi huo, huku tatu zikiharibika akiwashinda Ally Mayay (9), Shija Richard (9), Iman Madega (8), Fredrick Mwakalebela (3) na Emmanuel Kimbe aliyeambulia kura moja tu.

Akatetea tena kiti katika uchaguzi uliopita uliofanyika Agosti 7, 2021 ambao ulianza kutumia Kanuni za Uchaguzi za Mwaka 2021 alipoidhinishwa na wajumbe 81 na safari hii amejitosa tena kutetea akianza kutumikia kwa awali ya pili kwa mujibu wa marekebisho yaliyofanyika ya katiba ya TFF.

UCH 03

WAJUMBE HAO NI WAPI?

Kwa mujibu wa orodha ya wanaotoa uidhinishaji (endorsement) kwa wagombea wa TFF ni wajumbe 47 ambao mchanganuo wake upo hivi;

1. Vyama vya Soka vya Mikoa (FA) vyenye wajumbe 26.

Mikoa hiyo 26 yenye wajumbe wa kuidhinisha (endorsement ) wagombea wa uchaguzi wa TFF ni; Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Katavi, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida, Songwe, Tabora na Tanga.

Hata hivyo, Tanzania kwa ujumla ina mikoa 31 ikiwamo na Zanzibar, ila hiyo 26 inatambulika kwa msingi wa uanachama wa TFF Bara.

2. Klabu za Ligi Kuu ambazo ni 16, kila moja ikiwakilishwa na mtu mmoja pia.

3. Chama wa Waamuzi Tanzania (FRAT) chenye mjumbe mmoja vilevile

4. Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA)-1

5. Chama cha Madaktari wa Michezo (TSMA)-1

6. Chama cha Wachezaji (SPUTANZA)-1

7. Chama cha Soka la Wanawake (TWFA)-1

Ukijumuisha wajumbe hao wote yaani 26+16+1+1+1+1+1 idadi ya jumla inakuwa 47 na hao ndio wanaotakiwa kuombwa udhamini na wagombea angalau kila mmoja apate wajumbe wasiopunguza watano, lakini kuna wagombea wanadai hawajapata hata mmoja.

UCH 04

SIO KURA HALISI

Licha ya kwamba udhinishaji au udhamini umekuwa kikwazo kwa baadhi ya wagombea, ila ukweli ni kwamba hizo siyo kura halisi za uchaguzi wa TFF.

Ni muhimu kuelewa kuwa endorsement sio kura, bali ni tamko la wazi la kuunga mkono. Kura halisi hupigwa na wajumbe waliopo kisheria kwenye uchaguzi ambao una wajumbe wasiozidi 100 baada ya marekebisho ya taratibu, sheria na kanuni za uchaguzi huo yaliyofanyika mwaka 2020 mkoani Kigoma.