Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawa hapa miamba wa tuzo nane NBA 2026/27

TUZO Pict

Muktasari:

  • Ni vyema ikaeleweka kwamba msimu umeanza ukiwa miongoni mwa misimu inayovutia zaidi katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mabadiliko yaliyofanyika wakati wa mapumziko ya ligi, uwezekano wa kuwa na kundi la wachezaji chipukizi lenye ubora wa kihistoria na ligi ambayo tayari ina wachezaji wengi wenye vipaji vikubwa.

DETROIT, MAREKANI: LIGI ya Kikapu Marekani (NBA) msimu wa 2026/27 ilirejea usiku wa kuamkia jana, ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya Detroit Pistons na Boston Celtics, lakini nyuma ya mtifuano ulioanza kuna mambo kibao ambayo yanatarajiwa ifikapo mwisho Juni, 2027.

Mbali ya kuwapo kwa matukio yatakayoambatana na michuano hiyo, kuna tuzo kadhaa zinazoanza kuwaniwa kuanzia mwanzo wa ligi na huu ndio utabiri wa mchezaji bora (MVP), Mchezaji Bora Chipukizi, Mchezaji Bora wa Ulinzi wa Mwaka, Mchezaji Chipukizi Bora wa Mwaka, Mchezaji Bora wa Akiba wa Mwaka, Mchezaji Aliyeboreshwa Zaidi, Mchezaji Bora katika Nyakati Muhimu, Kocha Bora wa Mwaka na tuzo nyingine za msimu.

Ni vyema ikaeleweka kwamba msimu umeanza ukiwa miongoni mwa misimu inayovutia zaidi katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mabadiliko yaliyofanyika wakati wa mapumziko ya ligi, uwezekano wa kuwa na kundi la wachezaji chipukizi lenye ubora wa kihistoria na ligi ambayo tayari ina wachezaji wengi wenye vipaji vikubwa.

Lakini, ni wachezaji gani, kwa maana hiyo, watakaokuwa vinara wa msimu wa kawaida wa ligi? Twende pamoja, lakini kumbuka kwamba huu ni utabiri tu.


TUZ 0

MVP

Nyota anayepewa nafasi kubwa ni Victor Wembanyama wa San Antonio Spurs; na sababu inaelezwa kwamba ni chaguo lisilo na ubishi mkubwa. Msimu uliopita, Wembanyama alipiga hatua kutoka kuwa nyota mkubwa hadi mchezaji anayetarajiwa kuingia katika orodha ya wachezaji bora wa muda wote.

Alishika nafasi ya kwanza kwa tofauti kubwa katika kipimo cha jumla cha DRIP, kinachokadiria mchango wa mchezaji katika tofauti ya pointi za timu yake kwa kila umiliki 100 wa mpira. Na sasa, mshambuliaji huyo wa nafasi ya nne mwenye urefu wa futi 7 na inchi 4 anatoka katika kushindwa kwa maumivu kwenye fainali za NBA na amedhamiria kuthibitisha kuwa ndiye mchezaji bora zaidi duniani bila kupingwa.

Wembanyama atarejea kwa nguvu, na kitu pekee kinachoweza kumzuia ni sharti la ligi linalomtaka mchezaji kucheza angalau mechi 65 ili kustahili tuzo hiyo.

Wengine wanaotabiriwa kupambania MVP ni Shai Gilgeous-Alexander (Oklahoma City Thunder), Nikola Jokic (Denver Nuggets), Luka Doncic (Los Angeles Lakers) na Giannis Antetokounmpo (Miami Heat).


TUZ 02

MLINZI BORA WA MWAKA

Wembanyama kwa mara nyingine anapewa nafasi ikielezwa kwamba ni wachezaji watatu pekee waliowahi kushinda tuzo za MVP na Mlinzi Bora wa Mwaka katika msimu mmoja ambao ni Michael Jordan (1987-88), Hakeem Olajuwon (1993-94) na Giannis Antetokounmpo (2019-20). Wembanyama anapaswa kuwa mchezaji wa nne, na msimu huu unaonekana kuwa wakati mwafaka kwake kufanya hivyo.

Sababu inayomfanya awe mbele kwa mbali ya wachezaji wengine ni kwamba anaongoza kwa tofauti kubwa katika kipimo cha D-DRIP, kinachotathmini mchango wa mchezaji katika ulinzi.

Anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kushinda tuzo kwa kura za pamoja za majaji  katika historia ya tuzo hiyo. Atakuwa mchezaji bora zaidi wa ulinzi katika ligi kwa muda wote atakaokuwa katika kilele cha uwezo wake, isipokuwa kiumbe mwingine wa ajabu aamue kuvamia sayari hii.

Wengine wanaopigiwa upatu ni Chet Holmgren (Oklahoma City Thunder), Ausar Thompson (Detroit Pistons), Rudy Gobert (Minnesota Timberwolves) na Bam Adebayo (Miami Heat).


TUZ 03

CHIPUKIZI BORA WA MWAKA

Hapa kuna mwamba Cameron Boozer wa Memphis Grizzlies inayeelezwa kwamba kushinda tuzo ya Mchezaji Chipukizi Bora wa Mwaka mara nyingi hutegemea mchezaji kuwa na takwimu kubwa huku akionyesha uwezo mkubwa wa kuimarika zaidi baadaye.

Hakuna mchezaji katika kundi la mwaka huu anayeonekana kuwa tayari kufanya hivyo kama Boozer. Grizzlies wako katika hatua ya kuanza upya ujenzi wa timu yao na watataka kuonyesha ulimwengu kipaji chao kipya na changa.

Mchezaji huyo aliyetoka Chuo Kikuu cha Duke pia anasifiwa na wachambuzi wa wachezaji wanaotarajiwa kuchaguliwa katika rasimu ya NBA kutokana na mtindo wake wa uchezaji unaomwezesha kutoa mchango mkubwa mara moja.

Uwezo huo ulimsaidia kuwa miongoni mwa waliofika hatua ya mwisho kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Naismith msimu uliopita. Tangu mwaka 2000, ni wachezaji chipukizi watatu pekee; Wembanyama, Karl-Anthony Towns na Blake Griffin waliowahi kuwa na wastani wa angalau pointi 18 na ribaundi nane huku wakicheza angalau mechi 50.

Wote walishinda tuzo hiyo. Boozer ana uwezo wa kufikia takwimu hizo, hasa akipewa nafasi kubwa ya kucheza na kuwa sehemu muhimu ya timu. Lakini kuna wengine kama AJ Dybantsa (Washington Wizards), Darryn Peterson (Utah Jazz), Caleb Wilson (Chicago Bulls) na Darius Acuff Jr (Sacramento Kings).


TUZ 04

MCHEZAJI BORA WA AKIBA

Ajay Mitchell wa Oklahoma City Thunder anatajwa katika nafasi hii na sababu inatajwa kwamba alikuwa mchezaji bora wa akiba katika ligi msimu uliopita. Kati ya wanaowania wote alikuwa na alama za juu zaidi katika kipimo. Bahati mbaya kwa mlinzi huyo wa kufunga vikapu mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4, jeraha alilopata mwishoni mwa msimu lilipunguza kasi yake.


TUZ 05

STAA BORA WA AKIBA

Historia inaonyesha kuwa ili kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Akiba wa Mwaka, mchezaji anahitaji kuwa na wastani wa angalau pointi 13 kwa kila mechi na kucheza timu iliyomaliza katika nafasi nne za juu.

Thunder wanatarajiwa kuwa timu yenye nguvu kubwa, huku Mitchell akiwa na wastani wa pointi 13.6 kwa kila mechi katika msimu wake wa pili.

Mradi Jalen Williams abaki na afya njema na Mitchell asilazimike kutumia muda mwingi katika kikosi cha kwanza, basi hakuna sababu ya msingi ya kutompa tuzo hiyo. Wengine ni pamoja na Dylan Harper (San Antonio Spurs), Ayo Dosunmu (Minnesota Timberwolves), Sam Merrill (Cleveland Cavaliers) na Miles McBride (New York Knicks).


TUZ 06

MCHEZAJI ALIYEBORESHWA ZAIDI

Katika kipengele hiki kuna Coby White wa Charlotte Hornets na hii ndiyo tuzo ngumu zaidi kutabiri kwa sababu, kimsingi, inapaswa kwenda kwa mchezaji ambaye maendeleo yake makubwa hayakutarajiwa na wengi. Inaamika kwamba mara nyingi sana tuzo ya Mchezaji Aliyeboreshwa Zaidi (MIP) huenda kwa mchezaji kijana anayefuata tu mkondo wa kawaida wa maendeleo.

Akiwa na Hornets, White anaonekana kuwa mfano bora wa kuunganisha kipaji na fursa. Amekuwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kushambulia, lakini hajawahi kuwa na udhibiti wa nafasi ya mchezaji wa kwanza wa ulinzi wa timu, yaani point guard, bila kushindaniwa.

Kwa kuwa LaMelo Ball ameondoka na sasa kuna mazingira mazuri ya kushambulia yanayomzunguka, akiwemo Kon Knueppel, Brandon Miller na Naz Reid, huu ndio wakati mwafaka kwa White kuonyesha uwezo wake kamili.

Anaweza hata kutoka katika wastani wa pointi 17.4 kwa kila mechi aliokuwa nao msimu uliopita hadi pointi 24 au 25 kwa kila mechi.

Wengine wanaoweza kupambana naye ni Payton Pritchard (Boston Celtics), Gui Santos (Golden State Warriors), Ty Jerome (Memphis Grizzlies) na Julian Strawther (Denver Nuggets).


TUZ 07

MCHEZAJI BORA NYAKATI MUHIMU

Hapa tuzo hiyo inaweza kuondoka na Cade Cunningham wa Detroit Pistons. Kabla ya mshindi wa msimu uliopita, Gilgeous-Alexander, wachezaji watatu wa kwanza kushinda tuzo hiyo iliyoanzishwa miaka mitano iliyopita walikuwa wakichezea timu nzuri ambazo hazikuwa na tabia ya kushinda mechi kwa tofauti kubwa ya pointi.

Ili kushinda tuzo hiyo mchezaji anahitaji kuwa na matukio mengi ya kishujaa mwishoni mwa mechi. Na ili kupata nafasi nyingi za kufanya hivyo, timu yake inapaswa kucheza mechi nyingi zenye ushindani mkali hadi dakika za mwisho.

Pia anapaswa kuwa mchezaji anayejua namna ya kupata pointi ngumu wakati timu yake inapozihitaji. Ndiyo maana Cunningham anaonekana kuwa anayestahili. Mlinzi huyo wa point guard mwenye urefu wa futi 6 na inchi 6 alimaliza nafasi ya nne katika upigaji kura wa tuzo hiyo msimu uliopita.

Ana uwezo mkubwa wa kufunga kwa mitupo ya umbali wa kati, jambo linalowavutia mashabiki wa NBA. Pia, Pistons wanaonekana kuwa katika hatari ya kushuka kiwango baada ya kipindi cha mapumziko ya ligi kilichoambatana na mabadiliko mengi na misukosuko.

Wengine wanaoweza kushindana naye ni Luka Doncic (Los Angeles Lakers), Kyrie Irving (Dallas Mavericks), Jaylen Brown (Philadelphia 76ers) na Tyrese Haliburton (Indiana Pacers).


TUZ 08

KOCHA BORA

Tuzo hii itadondokea kwa kocha wa Miami Heat, Erik Spoelstra. Unaweza kuamini kwamba Spoelstra hajawahi kushinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka? Huenda msimu huu, ambao ni wa 19 kwake akiiongoza Heat ukawa wake wa kwanza kushinda.

Kwa kawaida, tuzo hiyo huenda kwa kocha anayeiongoza timu kufanya vizuri zaidi kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyotarajiwa kabla ya msimu kuanza. Kwa sasa, Heat wanatabiriwa kuwa nafasi ya tano kwa uwezekano wa kushinda ubingwa wa Kanda ya Mashariki.

Hata hivyo, siyo vigumu kumuona Spoelstra akimboresha nyota wake mpya Giannis Antetokounmpo na Bam Adebayo anayeweza kufanya kila kitu uwanjani pamoja na kundi la wachezaji wapambanaji akiwemo Pelle Larsson, Davion Mitchell na Andrew Wiggins kuwa timu inayoshika nafasi tatu za juu kutoka Mashariki.

Akifanikiwa kufanya hivyo huenda Spoelstra akatwaa tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka. Wagombea wengine ni pamoja na Charles Lee (Charlotte Hornets), Will Hardy (Utah Jazz), Mitch Johnson (San Antonio Spurs) na Darko Rajakovic (Toronto Raptors).