Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Habibu Kondo ashindwe mwenyewe Bandari

KONDO Pict

Muktasari:

  • Kondo ni kocha mzuri na mzoefu anayeweza kukabiliana na presha za kupandisha timu na hivyo kijiwe kinaamini Bandari Tanzania haijakosea kumchukua na kumkabidhi jukumu hilo muhimu.

BANDARI Tanzania FC wanaonekana wanajipanga vilivyo na Ligi ya Championship msimu ujao wa 2026/2027 baada ya kupanda daraja msimu uliopita.

Kwanza nasikia wamefanya mabadiliko katika benchi lao la ufundi na Omega Seme aliyekuwa kocha mkuu ameondoka na inaripotiwa nafasi yake itachukuliwa na Habibu Kondo.

Kondo ni kocha mzuri na mzoefu anayeweza kukabiliana na presha za kupandisha timu na hivyo kijiwe kinaamini Bandari Tanzania haijakosea kumchukua na kumkabidhi jukumu hilo muhimu.

Ukiondoa Kondo, jamaa wamefanya usajili wa wachezaji wazuri ambao baadhi ni matirio ya kucheza Ligi Kuu kabisa lakini sasa tutawaona katika jezi za Bandari Tanzania wakipambania heshima ya timu hiyo.

Miongoni mwao kuna straika wa mpira Issah Ngoah ambaye Bandari Tanzania imemchukua kutokea Geita Gold ambayo ilimaliza ikiwa kinara wa Ligi ya Championship huku Ngoah akiwa ni miongoni mwa washambuliaji tegemeo.

Halafu nimeona wamemnasa fundi wa kupiga pasi na kuchezesha timu, Ayoub Semtawa ambaye msimu uliomalizika alikuwa akiichezea Namungo FC inayoshiriki Ligi Kuu na amewahi kupita Coastal Union.

Kuna beki wa zamani wa Alliance FC, Mtibwa Sugar na Mbao FC, Geofrey Luseke pamoja na winga wa zamani wa Simba na Coastal Union, Hija Ugando.

Wamemchukua pia Joe Makoye kutoka TRA United huku pia wakipata saini ya mchezaji wa Mtibwa Sugar, Jabir Masumbuko.

Kiukweli Bandari Tanzania wamesajili vizuri na ukizingatia jamaa wanaweza kuihudumia vyema timu, kazi inabaki kwa kocha Habibu Kondo.