Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Foba na Masalanga wamenikumbusha 1947

HISIA Pict


TUNAMALIZIA shukrani za mwisho mwisho kwa baadhi ya watu walioenda Morocco kucheza Afcon. Mkononi nina makipa wetu wawili. Zubeir Foba Masudi na Hussein Masalanga. Maisha yameenda kasi kwao.


Wamenikumbusha mbali. Kwanza kabisa wamenifurahisha kwa utundu wao ambao wameonyesha kule Morocco. Sikutegemea. Lile lilikuwa jukwaa kubwa. Kipa namba moja alitazamiwa kuwa Yakubu Suleiman. Aliumia katika mazoezi wakati akiwa kambini pale pale Morocco.


Hata kama Yakubu angekuwa fiti kiasi cha kucheza bado angekuwa kipa ambaye hana uzoefu katika jukwaa lile. Yakubu mwenyewe ameichezea Taifa Stars mechi ya kwanza katika kipindi cha mwaka mmoja tu. Na yeye maisha yameenda kasi kwake.

HISI 05

Ndani ya mwaka mmoja amekaa katika lango la Taifa Stars na amekaa katika lango la klabu ya Simba katika michuano ya CAF.

Nyota iliwaka akiwa na klabu yake ya zamani ya JKT Tanzania na ghafla Simba ikamuamini kuwa kipa wa pili nyuma ya Moussa Camara. Baada ya Camara kuumia akapewa jukumu.

Katika timu ya taifa nafasi ilikuwa wazi kwa sababu kwa muda mrefu Aishi Manula alikuwa hachezi pale Msimbazi na alipohamia Azam bado hakuwa katika utimamu hata wa kuwa miongoni mwa makipa watatu wa Taifa Stars ambao wangesafiri kwenda Morocco.

HISI 03

Yakubu alipoumia ilimaanisha kwamba tulikuwa tunahamia kwa kipa ambaye katik hali halisi angeweza kuwa kipa wa tatu katika kikosi cha Taifa Stars kama Manula angekuwa na utimamu wa mwili. Foba. Licha ya kwamba anacheza timu kubwa kama Azam lakini kuna mashabiki wa mpira wetu wamemjulia Foba kule Morocco. Hawakuwa wanamfahamu sana.

Alicheza pambano dhidi ya Nigeria. Binafsi alifanya makosa mawili tu. yote yalitokana na kutoka nje ya eneo lake kwenda kumuwahi Victor Osimihen na kujikuta akipigwa chenga.

Nilidhani angeweza kubaki katika eneo lake kwa sababu Victor halikuwa hajamalizana na walinzi wake. Hata hivyo Victor hakufanikiwa kufunga.

HISI 04

Baada ya hapo Foba alikuwa muhimili mkubwa langoni kwa kuokoa michomo ya Wanigeria. Katika hali ya kawaida tulitegemea kumuona Foba akibabaika sana kwa sababu ilikuwa ni michuano yake ya kwanza mikubwa kuwepo katika lango la Watanzania.

Baadaye aliumia na nafasi ikaenda kwa Hussein Masalanga aliyecheza mechi nyingine. Masalanga anacheza Singida Big Stars na umaarufu wake umekuja katika jezi ya Taifa Stars. Sio wote ambao walimfahamu Masalanga kabla ya michuano hii.

Kiukweli kabisa usingeweza kudhani kwamba Masalanga alikuwa anacheza michuano hii kwa mara ya kwanza. Na wala usingeweza kudhani kwamba hajacheza hata mechi nne za Taifa Stars kabla ya michuano hii.

HISI 02

Mara zote nimesafiri naye akiwa kama kipa namba tatu. Hakuna nafasi ngumu kama ya ugolikipa linapokuja suala la kubadilishana nafasi. Kama kipa namba mbili anaweza kukaa benchi msimu mzima vipi kuhusu kipa namba tatu.

Hata hivyo Masalanga alichukua nafasi yake na kucheza bila ya wasiwasi. Baada ya muda mrefu ujao hatuwezi kutazama nyuma na kujisemesha kwamba Masalanga na Foba walituangusha katika michuano hii. Sio kweli.

Hawakuwa na makosa mengi binafsi. Na unapokumbuka kwamba michuano hii ilikuwa mikubwa kwao na kwa Taifa Stars unalazimika kuwapa hongera kwamba walicheza kama vile wamezoea kukaa katika lango la Taifa Stars.

Foba ametushangaza kwa mambo mawili. Kwanza kabisa ni kumuweka benchi Aishi katika klabu yao ya Azam. Hatujui ni kitu gani kinamtokea Aishi.

HISI 01

Huu ni mjadala wa siku nyingine. Tulidhani kwamba kwa kurudi Azam akitokea Simba alikokuwa na mgogoro na timu hiyo labda ndio ingekuwa nafasi ya kukaa langoni kila wiki pale Azam. Haijawa hivyo. Foba ameaminika zaidi.

Lakini pili ametushangaza kwa namna ambavyo alimiliki lango la Taifa Stars kiasi kwamba kuna mashabiki waliamini kwamba hata kama Yakubu angepona bado Foba angestahili kuwa kipa namba moja wa kikosi cha Taifa Stars.

Masalanga amenishangaza kwa mambo mawili. Jambo la kwanza ni kutokuwa na wasiwasi pale langoni. Lakini jambo la pili limenishangaza kuona umri wake. Ana miaka 33. Alikuwa wapi siku zote kuwa mmoja kati ya makipa wanaozungumzwa nchini?

Yote kwa yote makipa hawa wamenikumbusha zamani. Wamenikumbusha mwaka 1947. Wakati huo Tanzania tulikuwa na makipa wengi waliokuwa na uwezo sawa wa kulitumikia taifa. Karibu kila mkoa au kila timu ya ligi kuu ilikuwa na kipa hodari. Kipa ambaye angeweza kukaa katika lango la Taifa Stars na tusingekuwa na wasiwasi.

Kulikuwa na rundo la makipa kama Mohamed Mwameja, Hamis Makene, Paul Rwechungura, Madata Lubigisa, Steven Nemes na wengineo. Kule Zanzibar walikuwa wanatuletea akina Riffat Said, Ally Bushiri, Ridhaa Khamis na Ramadhan Korosheni.

Taifa linahitaji maisha haya kwa mara nyingine tena. Hiki ndicho ambacho tunajivunia kutoka kwa Foba na Masalanga. Tunahitaji wachezaji wengi wenye uwezo katika nafasi mbalimbali tofauti uwanjani. Na tunahitaji wachezaji wenye uwezo ambao sio lazima wawe wanacheza Simba au Yanga kama tulivyozoea.

Tumezoea kukariri majina ya wachezaji wa Simba na Yanga na labda ndio maana watu hawakumfahamu Masalanga kabla ya mechi hizi za Afcon. Mashabiki wamezoea wachezaji wao. Kwa kiasi kikubwa pia jambo hili linapunguza Usimba na Uyanga katika kikosi cha Taifa Stars.

Wachezaji kama kina Foba, Masalanga, Alphone Mabula, Tarryn Allarkhia, Haji Mnoga, Novatus Dismas na wachache wengineo ambao hawachezi wala hawajawahi kucheza Simba na Yanga kwa kiasi kikubwa wameondoa Usimba na Uyanga kwa mashabiki wetu.