Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Doumbia hana cha kujitetea tena

DOUMBIA Pict

Muktasari:

  • Mwanzoni alipoanza kutofunga, alijitetea na tulimtetea kwamba ni mgeni bado hajazoea ligi hivyo apewe muda mambo yatakaa sawa.

BWANA Ibrahim Doumbia kuanzia sasa anatakiwa kuhakikisha anaendeleza makali ya kufunga na mashabiki wa Simba wanatakiwa kumdai.

Hana sababu yoyote hivi sasa ambayo anaweza kuitumia iwapo ukame wake wa mabao utarudi tena.

Mwanzoni alipoanza kutofunga, alijitetea na tulimtetea kwamba ni mgeni bado hajazoea ligi hivyo apewe muda mambo yatakaa sawa.

Lakini kwa sisi watu wa mpira, muda huo angalau basi uwe mechi tano au 10 na sio mechi au siku nyingi maana timu nayo inahitaji matokeo mazuri.

Baadaye tukahamisha utetezi kuwa labda kinachomgharimu Doumbia ni kutokuwa sawa kisaikolojia hivyo anapoteza uwezo wa kujiamini.

Hapa kijiweni tukawa tunatamani Doumbia afanye kitu kama alichokifanya juzi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wale jamaa wa Guinea Ikweta.

Kwa sababu ilionekana kwamba akipata bao, atakaa sawa na kujiamini kwake kutaongezeka na hivyo hatokuwa anapata tena kiwewe akiwa karibu na goli la timu pinzani.

Na hatimaye juzi amefunga mabao mawili huku timu yake ikiua sita hivyo kama huko kupoteza hali ya kujiamini hatutegemei kuendelea kutumika kama utetezi.

Baada ya hapa hana tena sababu za kutuambia ili tumuelewe iwapo ubutu wake wa kufunga utarudi tena.