Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diaby, Akamiko nendeni na deni la Azam

AKAMINKO Pict

Muktasari:

  • Yule Yoro Diaby anaondoka akiwa ameitumikia Azam FC kwa misimu miwili tangu alipojiunga nayo mwaka 2024 akitokea Stade Malien ya Mali na James Akaminko ameichezea timu hiyo kwa misimu minne tangu alipojiunga nayo 22.

MIONGONI mwa wachezaji tisa ambao wamepewa mkono wa kwaheri na Azam FC ikiwa na maana kwamba hawatoichezea timu hiyo msimu ujao ni beki Yoro Diaby na kiungo James Akaminko.

Yule Yoro Diaby anaondoka akiwa ameitumikia Azam FC kwa misimu miwili tangu alipojiunga nayo mwaka 2024 akitokea Stade Malien ya Mali na James Akaminko ameichezea timu hiyo kwa misimu minne tangu alipojiunga nayo 2022.

Hata hivyo kijiwe kinaona kwamba wachezaji hao wawili wanaondoka wakiwa hawaidai chochote ingawa wao ndio wanadaiwa na klabu hiyo. Hawaidai Azam FC kwa sababu klabu hiyo iliwatimizia stahiki zao zote na kwa wakati sahihi na ndio maana hatukusikia au kuona wakiwa na malalamiko yoyote kuhusu malipo au mahitaji mengine yaliyopo kwenye mikataba yao na klabu hizo.

Hata hivyo wao wanaondoka wakiwa na deni la kushindwa kutoa mchango stahiki katika kuiwezesha Azam FC kutimiza lengo lake kuu ambalo ni kutwaa mataji makubwa nchini.

Yule Yoro Diaby alikuwa na mfululizo wa makosa ambayo yameigharimu Azam FC katika michezo mingi ya mashindano tofauti kwa kuziwezesha timu pinzani kupata ambayo mara kadhaa ziliifanya timu hiyo isipate ushindi.

Halafu kuna James Akaminko. Wakati anakuja nchini watu wengi walimtabiria kwamba atakuja kuwa miongoni mwa mastaa wakubwa katika ligi yetu hapa nchini kutokana na kiwango alichokionyesha siku za mwanzo.

Hata hivyo ameshindwa kutoa kile ambacho kilitabiriwa kwake. Changamoto kubwa aliyonayo ni kutokuwa na muendelezo wa kiwango bora ambapo kuna mechi anaonyesha kuwa wa moto na mechi nyingine hachezi vizuri.

Hakuna timu ambayo ingekubali kuendelea kumwaga fedha za kumhudumia mchezaji ambaye anang’aa katika mechi dhidi ya Simba na Yanga tu halafu mechi nyingine zote anashindwa kuonyesha kiwango bora.