Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Der Klassiker... Ni Bayern vs Dortmund

EP 01

Muktasari:

  • wenyeji wa Dortmund katika pambano la Der Klassiker. Mechi hiyo itakuwa ya kwanza kwa Kane kurejea uwanjani tangu hafla ya utoaji wa tuzo iliyofanyika Jumatatu.

MUNICH, UJERUMANI: LIGI Kuu Ujerumani (Bundesliga), itapigwa leo ambapo kuna mechi kibao zinazochezwa, lakini macho na masikio ya mashabiki wengi wa soka yataelekezwa katika Dabi ya Ujerumani maarufu kama Der Klassiker (German Clasico), ambako wababe Bayern Munich wataikaribisha Borussia Dortmund katika Uwanja wa Allianz Arena jijini Munich kuanzia saa 2:30 usiku.

Wiki hii ilikuwa nzuri kwa kila mmoja anayehusishwa na Bayern Munich, baada ya Harry Kane kutwaa tuzo ya Ballon d’Or iliyomfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Bayern kushinda tuzo hiyo kubwa zaidi ya mchezaji binafsi katika soka tangu Karl-Heinz Rummenigge alipofanya hivyo 1981.

Pia amekuwa mchezaji wa kwanza wa Bundesliga kutwaa tuzo hiyo tangu nyota wa zamani wa Borussia Dortmund, Matthias Sammer, aliposhinda 1996.

Mambo yanaweza kuwa mazuri zaidi kwa Bayern, leo Jumamosi, watakapokuwa wenyeji wa Dortmund katika pambano la Der Klassiker. Mechi hiyo itakuwa ya kwanza kwa Kane kurejea uwanjani tangu hafla ya utoaji wa tuzo iliyofanyika Jumatatu.

Hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza Jumatano wakati Bayern ilipoichakaza Magdeburg kwa mabao 6-1 katika Kombe la DFB-Pokal, licha ya kuwa kwenye benchi la wachezaji wa akiba.

Timu zote mbili zina pointi 17 baada ya kucheza mechi saba, huku kila moja ikishinda tano na sare mbili, hivyo ndizo timu pekee ambazo bado hazijapoteza mchezo katika Bundesliga msimu wa 2026-27, Bayern Munich ikiongoza ilhali Dortmund ikiifuatia kwenye msimamo wa Bundesliga.

DE 03

Katika misimu miwili kati ya mitatu iliyopita ya Bundesliga, Bayern imekuwa timu iliyozuia Dortmund kuendelea na rekodi ya kutopoteza mchezo wa kwanza wa msimu.

Iliwafunga wapinzani wake hao kwa mabao 2-1 jijini Munich katika mchezo wa saba wa msimu wa 2025-26, baada ya kuichapa kwa mabao 4-0 jijini Dortmund katika mchezo wa 10 wa msimu wa 2023-24.

Zaidi ya hapo, Bayern haijapoteza mchezo wowote katika mechi 21 zilizopita za ligi ikiwa kileleni mwa msimamo na kucheza dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili (imeshinda 13 na kutoka sare nane).

Hiyo ndiyo rekodi ndefu zaidi ya aina hiyo kuwahi kufikiwa na timu yoyote katika historia ya Bundesliga. Mara ya mwisho Bayern kupoteza mchezo wa aina hiyo ilikuwa Januari 2015, ilipochapwa mabao 4-1 na Wolfsburg.

DE 02

Na unapokuwa na mchezaji bora zaidi duniani katika kikosi daima unakuwa na matumaini ya kupata ushindi. Kane amefunga mabao sita katika mechi zake sita zilizopita za Bundesliga dhidi ya Dortmund. Katika mechi yake ya kwanza ya Der Klassiker, Novemba 2023, alifunga hat-trick, huku Februari mwaka huu akifunga mabao mawili.

Hata hivyo, Kane siyo mshambuliaji pekee ambaye kikosi cha wageni cha Niko Kovac kinapaswa kumuangalia kwa karibu. Idadi yake ya michango tisa ya mabao (mabao manne na asisti tano) katika Bundesliga msimu huu inalingana na ile ya mwenzake Michael Olise (mabao sita na asisti tatu).

Olise amefanikiwa kufunga angalau bao moja na kutoa asisti moja katika mechi tatu kati ya nne zilizopita za Bundesliga. Amefanya hivyo katika idadi hiyo hiyo ya mechi ambayo aliweza kufikia katika mechi zake 23 zilizotangulia.

Nyota huyo wa zamani wa Crystal Palace alifunga bao lililohitimisha ushindi wa Bayern wa mabao 3-1 dhidi ya Freiburg mwishoni mwa wiki iliyopita. Katika mechi hiyo, kocha msaidizi Aaron Danks, ndiye aliyekuwa akisimamia timu badala ya Vincent Kompany, ambaye bado anaendelea kupata nafuu baada ya kuanguka katika eneo la mazoezi la klabu hiyo wiki iliyopita.

Bayern imefunga mabao 25 msimu huu, ikiwa ndiyo timu iliyofunga mabao mengi zaidi katika Bundesliga. Pia ina rekodi ya pili bora ya ulinzi kwenye ligi hiyo baada ya kuruhusu mabao sita pekee.

Cha kushangaza zaidi, mabao 18 kati ya hayo 25 yamefungwa katika mechi tatu za kwanza za Bayern ilipokuwa mwenyeji msimu huu. Hiyo ni rekodi mpya kwa klabu yoyote katika hatua hii ya msimu.

EP 02

Bayern imefunga angalau mara tano katika kila mechi nne za mwisho za Bundesliga ilizocheza nyumbani, ikijumuisha msimu uliopita. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo kufikia rekodi hiyo.

Hata hivyo, Dortmund ndiyo timu pekee ya Bundesliga yenye rekodi bora ya ulinzi kuliko Bayern, kwani mabao manne iliyoruhusu ndiyo machache zaidi kwa timu yoyote katika ligi tano bora za Ulaya.

Dortmund imecheza mechi tano bila kuruhusu bao katika mechi zake saba za mwanzo, ikiweka rekodi inayolingana na ile ya klabu hiyo iliyowekwa katika misimu ya 2017-18 na 2020-21.

Maximilian Beier anaweza kuwa mchezaji wa kuangaliwa zaidi katika kikosi chao baada ya kufikisha michango 13 ya mabao katika Bundesliga mwaka 2026 (mabao saba na asisti sita).

Mchezaji pekee raia wa Ujerumani aliyefanya vizuri zaidi mwaka huu ni Deniz Undav wa VfB Stuttgart aliyehusika na mabao 17. Aidha, mabao 11 kati ya 12 ambayo Dortmund imefunga katika Bundesliga msimu huu yamefungwa wakati Beier akiwa uwanjani.


DE 04

HUKO NYUMA

Hii itakuwa mara ya 141 kwa Bayern na Dortmund kukutana katika mashindano rasmi tangu kuanzishwa kwa Bundesliga 1963 na huu ndio mchezo uliochezwa mara nyingi zaidi katika historia ya soka la kulipwa nchini Ujerumani.

Bayern imepoteza mechi nyingi zaidi dhidi ya Dortmund kuliko ilivyopoteza dhidi ya mpinzani mwingine yeyote katika mashindano yote, ikiwa imechapwa mara 33.

Hata hivyo, Bayern imepoteza mchezo mmoja pekee kati ya mechi 17 zilizopita ilizokutana na Dortmund (imeshinda 13, sare tatu na kupoteza mmoja). Kipigo hicho kilikuwa cha mabao 2-0 nyumbani chini ya kocha Thomas Tuchel, Machi 2024.

Kompyuta maalumu ya utabiri ya Opta inaipa Bayern nafasi kubwa ya kupata pointi zote tatu kwa asilimia 67.2, huku Dortmund ikipewa 15.4 na  asilimia 17.4 ikionyesha uwezekano wa timu hizo kutoka sare.