Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De La Fuente amzidi akili Scaloni

MBINU Pict

Muktasari:

  • Argentina ilicheza kwa tahadhari kubwa kiasi cha kushindwa hata kupiga shuti lililolenga lango ndani ya dakika 105 za kwanza kabla ya Hispania kupata bao la ushindi. Mwishowe, mabingwa hao watetezi walilipa gharama ya kucheza kwa kujihami kupita kiasi.

MIAMI, MAREKANI: BAADA ya nusu fainali mbili zilizojaa drama na burudani, wengi walitarajia fainali ya Kombe la Dunia 2026 iwe ya aina yake. Hata hivyo, mchezo huo haukufikia matarajio, lakini mwisho wa siku Hispania ilionyesha kwa nini ilistahili kutwaa ubingwa.

Argentina ilicheza kwa tahadhari kubwa kiasi cha kushindwa hata kupiga shuti lililolenga lango ndani ya dakika 105 za kwanza kabla ya Hispania kupata bao la ushindi. Mwishowe, mabingwa hao watetezi walilipa gharama ya kucheza kwa kujihami kupita kiasi.


De la Fuente ashinda vita

Kocha wa Hispania, Luis de la Fuente, alithibitisha ubora wake wa kusoma mchezo kwa kutumia benchi lake kwa wakati sahihi.

Licha ya timu yake kutawala mchezo tangu mwanzo, hakuridhika na kiwango hicho na akaamua kufanya mabadiliko muhimu. Aliwatoa washambuliaji Mikel Oyarzabal dakika ya 62 na Alex Baena dakika ya 75, ingawa wote walikuwa wakicheza vizuri.

Walioingia kuchukua nafasi zao, Ferran Torres na Nico Williams, walibadili kabisa sura ya mchezo. Ushirikiano wao ulizaa bao pekee la ushindi huku Williams akiwa tishio kubwa kwa safu ya ulinzi ya Argentina hadi dakika za mwisho.

Mabadiliko hayo yalionyesha namna kocha anavyoweza kubadili matokeo ya mchezo kupitia maamuzi sahihi, jambo ambalo linaweza kumpa kocha wa England, Thomas Tuchel, kazi ya ziada ya kujifunza kabla ya kukutana na mabingwa hao wapya wa dunia kwenye Nations League.


England ingeipa Hispania upinzani zaidi?

Baada ya kushuhudia namna Argentina ilivyocheza, wengi walibaki wakijiuliza kama England ingekuwa mpinzani bora zaidi kwa Hispania.

Tofauti na ilivyokuwa ilipoiondoa England katika nusu fainali, Argentina ilionekana kupoteza makali yake kabisa. Haikuonyesha kasi, presha wala ukali uliokuwa umezoeleka katika mechi zilizopita.

Kwa muda mrefu wa mchezo, mabingwa hao watetezi walionekana kuridhika kujilinda badala ya kushambulia. Hata walipopata nafasi ya kusawazisha mwishoni kupitia Giuliano Simeone, shuti lake la voli lilipaa juu ya lango.

MBIN 01

Martinez aibeba Argentina

Kama kuna mchezaji aliyewafanya Argentina ibaki kwenye mchezo kwa muda mrefu, basi ni kipa Emiliano Martinez.

Mlinda mlango huyo wa Aston Villa aliokoa mashambulizi mengi ya Hispania na kufanya zaidi ya save 10 ndani ya dakika 90 za kawaida.

Miongoni mwa mabao aliyookoa ni kichwa cha Aymeric Laporte kilichokuwa kinaelekea kona ya juu pamoja na shuti kali la Nico Williams.

Licha ya mara nyingi kulaumiwa kwa tabia zake, safari hii Martinez alionyesha utulivu mkubwa na kama mchezo ungeenda mikwaju ya penalti, wengi wangempa nafasi kubwa ya kuibeba tena Argentina.

MBIN 02

Rodri arudisha hadhi yake

Kiungo wa Hispania, Rodri, aliendelea kuthibitisha kuwa ni mmoja wa viungo bora duniani.

Baada ya kusumbuliwa na majeraha yaliyomfanya kushuka kiwango katika misimu miwili iliyopita akiwa Manchester City, Rodri ameonyesha kurejea kwenye ubora wake katika Kombe hili la Dunia.

Aliiongoza Hispania kwa utulivu mkubwa, akipoteza pasi chache sana na kushinda mapambano mengi ya katikati ya uwanja kabla ya kutolewa dakika za nyongeza.

Kiwango chake kitakuwa habari njema kwa Manchester City, ambayo inatarajia kumjenga upya kama mhimili wa kikosi chake.

MBIN 03

Burudani kubwa nje ya uwanja

Kwa upande wa maandalizi, fainali hiyo ilikuwa ya kiwango cha juu.

Uwanja ulijaa mashabiki huku mastaa wa dunia kama Tom Cruise, Robbie Williams, Chris Martin, Madonna na Justin Bieber wakihudhuria na kuongeza mvuto wa tukio hilo.

Hata hivyo, ndani ya uwanja mchezo haukuwa na kasi wala ubora uliotarajiwa kwa sehemu kubwa ya dakika zake.

Joto kali la mchana pamoja na mapumziko ya dakika 27 kati ya vipindi viwili vilionekana kuathiri kasi ya mchezo.

Licha ya hayo yote, Hispania ilimaliza kazi yake kwa mafanikio na kutwaa taji la dunia, huku Argentina ikiondoka ikiwa imeonyesha kiwango cha chini kuliko ilichokionyesha katika hatua za awali za mashindano.