Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hispania yaweka rekodi ya historia duniani

MASHINE Pict

Muktasari:

  • Miaka miwili tu baada ya kutwaa ubingwa wa Euro 2024, La Roja imekamilisha safari ya mafanikio kwa kutwaa taji la dunia, ikiiga rekodi waliyoifanya mwaka 2010 walipotwaa Kombe la Dunia miaka miwili baada ya kushinda Euro 2008.

LOS ANGELES, MAREKANI: HISPANIA imeendelea kuthibitisha ubabe wake kwenye soka la dunia baada ya kutwaa Kombe la Dunia 2026 kwa kuichapa Argentina bao 1-0 katika fainali iliyochezwa New Jersey, Marekani, na kuandika historia nyingine kubwa.

Miaka miwili tu baada ya kutwaa ubingwa wa Euro 2024, La Roja imekamilisha safari ya mafanikio kwa kutwaa taji la dunia, ikiiga rekodi waliyoifanya mwaka 2010 walipotwaa Kombe la Dunia miaka miwili baada ya kushinda Euro 2008.

Ushindi huo umeifanya Hispania kuwa taifa la kwanza katika historia kushikilia kwa wakati mmoja mataji ya Kombe la Dunia kwa timu za wanaume na wanawake, baada ya timu ya wanawake kuibuka bingwa wa dunia mwaka 2023 kwa kuifunga England mjini Sydney.

YAM 06

Lakini mafanikio hayo hayaishii hapo.

Timu ya wanaume pia ilitwaa UEFA Nations League mwaka 2023 na medali ya dhahabu ya Olimpiki mwaka 2024, huku wanawake wakitwaa mataji mawili mfululizo ya Nations League mwaka 2024 na 2025.

Kwa ujumla, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Hispania imeshinda mataji 16 ya dunia na Ulaya kuanzia ngazi ya chini ya miaka 17 hadi timu za wakubwa, jambo linaloonyesha uimara wa mfumo wao wa ukuzaji vipaji.

Mchambuzi wa soka wa Hispania, Guillem Balague, amesema mafanikio hayo si bahati bali ni matokeo ya mfumo uliojengwa kwa muda mrefu.

“Huu ni utawala wa kweli. Kila mtu anaamini katika mfumo wetu wa uchezaji na muhimu zaidi hatujawahi kusimama. Tumefika kileleni tena kama tulivyofanya mwaka 2010,” amesema Balague.

TRUM 02

Mashine ya mataji

Kwa upande wa wanawake, Hispania imekusanya mataji 11 kati ya mwaka 2022 na 2026, yakiwemo Kombe la Dunia 2023, Nations League mara mbili (2024 na 2025), Kombe la Dunia la chini ya miaka 20 mwaka 2022, mataji matano mfululizo ya Euro U-19 kuanzia 2022 hadi 2026, pamoja na Kombe la Dunia na Euro U-17.

Kwa wanaume, wamekusanya mataji matano katika kipindi hicho, yakiwemo Kombe la Dunia 2026, Euro 2024, Nations League 2023, dhahabu ya Olimpiki 2024 na Euro U-19 mwaka 2026.


De La Fuente ageuza kila kitu

Mafanikio haya yamekuja chini ya kocha Luis de la Fuente, ambaye aliteuliwa Desemba 2022 baada ya Hispania kutolewa na Morocco katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Wakati huo wengi waliona uteuzi wake kuwa wa hatari kwa sababu hakuwahi kuinoa klabu kubwa barani Ulaya.

Hata hivyo, ndani ya miaka minne ameiongoza Hispania kutwaa Nations League, Euro na sasa Kombe la Dunia.

Balague amesema siri ya De la Fuente ni kuufahamu mfumo wa soka wa Hispania tangu ngazi za vijana.

“Alikuwa anawafahamu karibu wachezaji wote tangu walipokuwa kwenye akademi. Hilo limeifanya timu ikue pamoja,” amesema.

Kiungo wa zamani wa Hispania, Juan Mata, anaamini mafanikio hayo ndiyo mwanzo wa enzi mpya.

“Hii si timu ya sasa pekee, bali ni timu ya baadaye pia,” amesema Mata.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 ameweka utamaduni wa kuheshimu wapinzani, kuwa na subira na kutoridhika na mafanikio.

Baada ya kutwaa Kombe la Dunia, amesema baadhi ya wachezaji walimuuliza ni kitu gani kimebaki kushinda.

“Tukagundua kilichobaki ni mechi inayofuata mwezi Septemba. Timu hii haitosheki na mafanikio,” amesema.

YAM 02

MAFANIKIO yamevuka hadi ngazi ya klabu

Ubora wa soka la Hispania sasa unaonekana hata kwenye klabu, huku makocha wengi wa nchi hiyo wakizidi kuaminiwa katika ligi kubwa duniani.

Licha ya Pep Guardiola kuondoka Manchester City baada ya miaka 10 ya mafanikio, robo ya makocha watakaoanza msimu wa 2026-27 wa Ligi Kuu England ni Wahispania.

Kwa sasa Hispania haijapoteza mechi yoyote katika michezo 38 mfululizo kwenye mashindano yote, rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na taifa lolote kutoka Ulaya au Amerika Kusini.


Wanawake nao wanatikisa

Mapinduzi makubwa yameonekana pia kwenye soka la wanawake.

Baada ya kushinda Kombe la Dunia mwaka 2023, Hispania iliendelea kutawala kwa kutwaa Nations League mwaka 2024 na 2025.

Mchezaji wa zamani wa Barcelona na mwandishi wa habari, Maria Garrido, amesema mazingira ya soka la wanawake yamebadilika kwa kiwango kikubwa.

“Miaka 10 iliyopita hakukuwa hata na akademi ya wasichana ya La Masia. Tulijigharamia usafiri kwenda mazoezini na hatukulipwa chochote. Leo hali imebadilika kabisa kwa uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu, akademi na maendeleo ya vijana,” amesema.

YAM 01

Mustakabali unaonekana salama

Hispania inaendelea kuzalisha nyota wenye uwezo mkubwa.

Lamine Yamal na Pau Cubarsi tayari wameonja ubingwa wa Kombe la Dunia wakiwa na miaka 19 pekee.

Yamal ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo zaidi kucheza fainali ya Kombe la Dunia, nyuma ya Pele wa Brazil mwaka 1958 na Giuseppe Bergomi wa Italia mwaka 1982.

Kwa mara ya kwanza pia Hispania ilianza fainali ya Kombe la Dunia ikiwa na vijana wawili wenye umri chini ya miaka 20 katika kikosi cha kwanza.

Kwa upande wa wanawake, Vicky Lopez tayari ameshinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu akiwa na Barcelona akiwa na umri wa miaka 19, huku Salma Paralluelo akiwa tayari ameichezea Hispania zaidi ya mechi 50 kabla ya kutimiza miaka 23.

Kipa wa zamani wa England, Joe Hart, amesema hakuna timu iliyokaribia kiwango cha Hispania kwenye Kombe la Dunia.

“Hakuna aliyeikaribia Hispania. Waliruhusu mashuti 10 tu yaliyolenga lango katika mashindano yote,” amesema.

Naye mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa, Thierry Henry, anaamini utawala wa Hispania bado una safari ndefu.

“Sifa kubwa zinapaswa kwenda kwenye mfumo wao. Zamani Hispania haikuwa inashinda hivi, lakini sasa wanashinda kila ngazi ya mashindano,” amesema.