Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Clara piga zako hela huko Marekani

CLARA Pict

Muktasari:

  • Pongezi ndio kitu cha msingi ambacho kijiwe kinakupa leo hii kwani umefanya jambo la kuiheshimisha nchi kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa soka la wanawake kununuliwa kwa pesa nyingi.

CLARA Luvanga hongera sana kwa kufanya uhamisho wa kibunda kirefu cha fedha kutoka Saudi Arabia kwenda Marekani.

Pongezi ndio kitu cha msingi ambacho kijiwe kinakupa leo hii kwani umefanya jambo la kuiheshimisha nchi kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa soka la wanawake kununuliwa kwa pesa nyingi.

Ushauri kuhusu hela unazopata huko na jinsi ya kuzitumia sijui kuwekeza hilo ni jambo ambalo sisi hapa kijiweni tuna kuachia wewe mwenyewe kwa sababu hilo ni jasho lako na unajua umevuja kiasi gani na njia gani umepita hadi umefika hapo ulipo.

Tunajua huko unakoenda unaenda kupiga hela ndefu sana za mshahara na bonasi zaidi ya zile ulizokuwa unapata Saudi Arabia hivyo jambo la msingi kwako ni kuzifurahia hela zako, kama utaamua kula bata we kula sana tu.

Kitu ambacho labda hapa kijiweni tunaweza kukushauri ni upande wa kazi yako kwamba hakikisha unalinda kipaji chako ili kiendelee kuwa chanzo cha wewe kupata hayo mahela mengi unayoyapata sasa au hata zaidi.

Tun achoamini wewe hakuna kipya huko majuu ambacho kitakufanya upoteze hali ya kujiamini au ubweteke kwa mafanikio unayopata kwa sababu huko majuu hii sio mara ya kwanza wewe unaenda na hauna ushamba nako. Katika yote utakayofanya huko Marekani, jambo la msingi ni kuhakikisha unapiga mzigo wa kutosha mazoezini na katika mechi jambo litakalofanya upate nafasi kikosini.

Hao wenzetu wanataka kazi tu bwana. Usije kufikiria hata siku moja kwamba utapata tu nafasi ya kucheza kwa sababu umenunuliwa kwa hela nyingi na wanakulipa mshahara mkubwa.

Suala la hao kumpotezea mchezaji hata kama wanamlipa hela nyingi za mshahara au walimsajili kwa gharama kubwa ni jambo rahisi kwao.