Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LeBron: Ubingwa Lakers! Hapana

Muktasari:

  • Unajua kwa nini? Wengi wanajua LeBron katua Lakers na hivyo mambo yatakuwa safi kwa timu hiyo. Hata hivyo, ghafla kawaacha watu vinywa wazi baada ya kuitoa timu yake hiyo kwenye orodha ya timu zitakazobeba taji la msimu ujao.

NDO hivyo. Nyota wa mpira wa kikapu Marekani (NBA), King LeBron James wa Los Angeles Lakers kashtua kinoma dunia na kusababisha mpasuko wa wafuatiliaji wa ligi hiyo.

Unajua kwa nini? Wengi wanajua LeBron katua Lakers na hivyo mambo yatakuwa safi kwa timu hiyo. Hata hivyo, ghafla kawaacha watu vinywa wazi baada ya kuitoa timu yake hiyo kwenye orodha ya timu zitakazobeba taji la msimu ujao.

Jambo hilo limesababisha mpasuko kwa wafuatiliaji wengi wa ligi hiyo, huku wengine wakimuunga mkono na wengine kuamini ameongea hayo kisiasa tu ili timu yake isikamiwe na kukutana na upinzani katika Ukanda wa Magharibi.

Nyota huyo ambaye amecheza mfululizo katika Ukanda wa Mashariki akiwa na timu za Miami Heat na Clevaland Cavaliers, amezitaja timu sita zenye uwezekano wa kutwaa ubingwa msimu huu unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba.

Katika orodha hiyo, LeBron ameiondoa timu yake hiyo pamoja na Cavaliers na kuzipa nafasi Golden State Warriors, Houston Rockets, Oklahoma City Thunder, Boston Celtics, Toronto Raptors na Philadelphia 76ers.

Huo ndio mtazamo wake. Je yuko sahihi? wakati utaongea. Tusubiri tuone pale ligi itakapoanza kwa miamba hiyo kuonyeshana kazi, huenda jamaa anataka wapinzani wasiwakamie.