Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcola: Sawa, shida ya liverpool hii hapa

BARCOLA Pict

Muktasari:

  • Licha ya Liverpool kutumia fedha nyingi katika usajili, tatizo kubwa la kiungo mkabaji linaendelea kuon-ekana wazi, huku kocha Andoni Iraola akianza maisha yake Anfield kwa sare nyingine ya 2-2 dhidi ya Nottingham Forest.

LONDON, ENGLAND: INAONEKANA kuna mtu amelala kazini ndani ya Anfield au huenda timu ya usajili inayoongozwa na Richard Hughes haikuona tatizo ambalo lilikuwa wazi kwa kila mmoja msimu uliopita.

Licha ya Liverpool kutumia fedha nyingi katika usajili, tatizo kubwa la kiungo mkabaji linaendelea kuon-ekana wazi, huku kocha Andoni Iraola akianza maisha yake Anfield kwa sare nyingine ya 2-2 dhidi ya Nottingham Forest.

Liverpool ilionyesha mapungufu makubwa katika eneo la kiungo hasa kwenye ulinzi, huku wapinzani wakipenya kirahisi kupitia katikati ya uwanja.

Kulikuwa na ukosefu wa nguvu katika kukaba, huku matumaini yakiwa kwa Dominik Szoboszlai na Alex-is Mac Allister ni wachezaji wenye mwelekeo mkubwa wa kushambulia na kubadilisha asili yao na kuwa wapiganaji wa kuilinda timu.

Lakini baada ya Iraola kuiongoza Liverpool katika mchezo wake wa kwanza wa nyumbani, mambo yalionekana kama yamerudi pale pale.

Forest walifanya mashambulizi ya kushtukiza kwa kasi na kuleta taharuki kubwa, huku Szoboszlai na Mac Allister wakionekana kupoteza mwelekeo kila walipokuwa hawana mpira.

BARC 04

BARCOLA SI JIBU PEKEE

Ni kweli, kuna furaha baada ya Hughes kufikia makubaliano ya ada inayoweza kufikia pauni123 milioni  na Paris Saint-Germain kwa ajili ya winga Bradley Barcola, ambaye anatarajiwa kukamilisha usajili wake ndani ya saa 24 na kulipwa mshahara wa takribani Pauni 300,000 kwa wiki.

Barcola ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na anaweza kuwa kivutio kikubwa katika safu ya ushambuliaji, hasa baada ya kuondoka kwa Mo Salah.

Tatizo ni moja Barcola ni winga. Huhitaji kuwa mtaalamu wa soka kutambua kwamba mchezaji mwenye kipaji kama Barcola anaweza kuwa mrithi mzuri wa Salah, lakini kinachoshangaza ni kwamba Liverpool imetumia zaidi ya miezi mitatu kumfuatilia Mfaransa huyo huku ikiacha pengo kubwa zaidi katika eneo la kiungo.

Na sasa, mapenzi hayo kwa Barcola yanaweza kugeuka kuwa uamuzi wa gharama kubwa.


BARC 02

FOREST WALIPITA KATIKATI

Nottingham Forest kama Newcastle United ilivyofanya katika mechi ya kwanza ya msimu waliingia mo-ja kwa moja katikati ya Liverpool na kuifanya safu ya kiungo ya Iraola ionekane dhaifu.

Dan Ndoye alifunga bao moja na angeweza kufunga mawili zaidi, wakati Igor Jesus katika kipindi cha kwanza alipata nafasi ya kuingia eneo la hatari la Liverpool kutokana na pasi sahihi na za kasi zilizotoka nyuma.

Liverpool ilipata nafasi pia. Florian Wirtz alifunga, lakini bao lake lilikataliwa kwa tofauti ndogo sana ya kuotea, muda mfupi baada ya Ndoye kufungua ukurasa wa mabao.

Wirtz alikuwa tayari amepoteza nafasi mbili kabla ya hapo.

Lakini, sekunde chache kabla ya mapumziko, Alisson alilazimika kuonyesha kiwango cha juu kabisa ku-muokoa Liverpool dhidi ya Jesus.

Kama Forest wangeenda mapumzikoni wakiwa mbele kwa mabao 2-0, huenda mchezo huo ungekuwa umefikia ukingoni.


BARC 03

LIVERPOOL WANAHITAJI ‘MTU’

Tatizo la Liverpool liko wazi wanahitaji mchezaji ambaye yuko tayari kupambana, kukaba, kuvunja mashambulizi na kufanya kazi chafu ili kuilinda safu yao ya nyuma.

Wanahitaji kiungo mkabaji ambaye haogopi kukabiliana na wapinzani, hata kama italazimika kupata kadi ya njano.

Cha kushangaza ni kwamba dirisha la usajili linakaribia kufungwa, lakini bado hakuna mchezaji wa aina hiyo aliyeletwa Anfield.

Gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard  ambaye enzi zake hakujulikana kwa kukwepa ‘tako’ kali wala kadi nyekundu alieleza tatizo hilo kwa ufupi.

Akizungumzia Liverpool ya Iraola, ambayo sasa imelazimika kupambana na kusaka sare ya 2-2 katika mechi mbili chini ya kocha huyo, Gerrard alisema, “wao ni wazuri kupita kiasi. Wana wachezaji wengi wazuri kiufundi, lakini wanakosa ule ukali kidogo. Kila eneo la uwanja wanapaswa kuwa tayari zaidi, hata kuchukua kadi za njano inapobidi. Hilo ndilo tatizo analokabiliana nalo Iraola,unahitaji ukali, huwezi kuwa mzuri kiasi hicho.”


BARC 01

MUNOZ ANA UKALI

Kwa upande mwingine, Victor Munoz ambaye ana umri sawa na Barcola, lakini amesajiliwa kwa gha-rama inayokadiriwa kuwa robo tu ya fedha zinazohitajika kumnunua Mfaransa huyo, anaonekana kuwa na kitu ambacho Liverpool inakikosa.

Mchezaji huyo wa Hispania alionyesha kujituma kwa kiwango kikubwa akifunga bao la pili la Liverpool katika dakika ya 82 baada ya kugeuka kwa ustadi na kupiga shuti kali lililozaa bao la kusawazisha.


HII SI TIMU

Iraola anaonekana anakusanyiko la wachezaji wenye vipaji binafsi, lakini bado hajajenga timu yenye mshikamano, huku kukiwa hakuna mtu katikati ya uwanja mwenye uwezo wa kuwaunganisha na kuwapa nguvu.

Wirtz anaonekana kuwa mpole kupita kiasi katika mapambano, na hali hiyo hiyo inaonekana kwa Alexander Isak, mmoja wa wachezaji waliosajiliwa kwa zaidi ya Pauni 100 milioni msimu uliopita.

Isak alifunga bao la kwanza la kusawazisha, lakini anaonekana kukosa ule uwezo wa kimwili unaohitaji-ka kwa mchezaji anayepaswa kupambana katika eneo la hatari.


BARCOLA PEKEE HAITOSHI

Hakuna ubishi kwamba kuwa na Barcola pamoja na Wirtz na Isak kutafanya Liverpool iwe na nguvu zaidi katika ushambuliaji.

Lakini kama hawatakuwa na kiungo anayejua kushinda mipira, kuvunja mashambulizi na kuilinda safu ya nyuma, Barcola anaweza kuishia kuwa mchezaji mwingine wa kuvutia kwenye kikosi, badala ya ku-wa suluhisho la matatizo yao.

Iraola alikuwa sahihi kulalamikia kuchelewa kwa dakika tatu wakati mwamuzi wa nne, Tim Robinson, alipokuwa akihangaika kubadilisha ubao wa wachezaji wa akiba huku Rio Ngumoha, Ryan Gravenberch na Kostas Tsimikas wakisubiri kuingia.

Kwa kuchelewa huko, Forest walipata nafasi ya kujipanga na kutumia mwanya huo. Lakini hata tukio hilo haliwezi kuficha tatizo kubwa zaidi.

Mabadiliko ya haraka ya Liam Delap aliyesajiliwa kwa Pauni 50 milioni yalifanya tukio lililozaa penalti yenye utata baada ya Neco Williams kuanguka kabla Morgan Gibbs-White kuitumia nafasi hiyo na kui-fungia Forest bao.