Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baraza asipoangalia hatoboi Pamba Jiji

BARAZA Pict
BARAZA Pict

Muktasari:

  • Sawa mpira unadunda lakini kwa hadhi ya timu ya Pamba Jiji, haikutakiwa eti katika mechi sita za kwanza za ligi iwe imepata pointi moja tu huku ikiwa nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi.

HUU mwanzo wa Pamba Jiji katika Ligi Kuu msimu huu unaogopesha kweli na kiukweli hauendani na heshima na jina la timu hiyo ya Mwanza.

Sawa mpira unadunda lakini kwa hadhi ya timu ya Pamba Jiji, haikutakiwa eti katika mechi sita za kwanza za ligi iwe imepata pointi moja tu huku ikiwa nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi.

Hata kama kufanya vibaya kupo, ilitakiwa angalau basi iwe hata na pointi tatu lakini moja kwenye mechi sita basi angalau ingekuwa na pointi tatu kwamba nusu ya mechi ilizocheza.

Katika upelelezi wa kijiwe, wadau wa Pamba Jiji na mashabiki baadhi wa soka Mwanza wametupa umbea wa mambo mawili ambayo tathmini ya timu inaona yanasababisha mwenendo wao usiwe mzuri katika mechi hizi za mwanzoni.

Jambo la kwanza ambalo ndio kubwa eti ni kupishana mitazamo kwa baadhi ya wazito ndani ya timu hiyo hivyo kumetokea kamgawanyiko ambacho kanayumbisha timu na sasa wanapambana kukatibu. Lingine ni majeraha ya wachezaji wao baadhi hasa mabeki jambo linalofanya ukuta wao uchelewe kuzoeana na kujikuta ukifanya makosa yanayoigharimu timu.

Lakini pamoja na hayo, mtu mmoja ndiye atajikuta katika kikaango iwapo mambo yataendelea kuwa mabaya katika timu hiyo naye ni kocha wao mkuu Francis Baraza.

Watu watasahau kwamba hakukuwa na maelewano kwenye timu na pia hawawezi kukumbuka kwamba Baraza ameanza msimu akiwa na wachezaji majeruhi wa nafasi muhimu uwanjani. Wao wataona njia sahihi ya kutibu kinachoendelea ni kumuacha Kocha Baraza hivyo anapaswa kukaa kwa tahadhari na kuwahimiza wachezaji wake wampambanie.