Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BAJANA  ‘Nyani mzee’ aliyekwepa mishale mingi

BAJANA Pict

Muktasari:

  • Awali, Bajana akifahamika kama Braison Raphael Nkulula alijiunga na akademi ya Azam FC 2011 baada ya kung’ara kwenye mashindano ya Copa Coca-Cola akiwa na timu ya Mkoa wa Kigoma.

SAFARI ya Sospeter Bajana kwenye viunga vya Azam Complex imemalizika rasmi baada ya kuaga Alhamisi, Septemba 4 mwaka huu.

Awali, Bajana akifahamika kama Braison Raphael Nkulula alijiunga na akademi ya Azam FC 2011 baada ya kung’ara kwenye mashindano ya Copa Coca-Cola akiwa na timu ya Mkoa wa Kigoma.

Akapandishwa timu kubwa 2014 na kudumu hadi anapoondoka baada ya takriban miaka 15. Huu ni muda mrefu ambao katika mazingira yoyote lazima kutakuwa na milima ya kupanda na mabonde ya kushuka.

Na hii ndio mishale mingi ninayotaka kuizungumzia hapa.


1. ALICHELEWA KUPANDISHWA

Bajana wakati ule akifahamika kama Braison Raphael alijiunga akademi ya Azam akiwa sambamba na wenzake kadhaa kama Aishi Manula, Mudathir Yahya, Joseph Kimwaga, Farid Mussa, Kelvin Friday, Gadiel Michael na kadhalika. Wachezaji hao wakaisaidia akademi ya Azam kushinda ubingwa wa Ligi ya Vijana 2012. Msimu wa 2013/14 Azam haikusajili mchezaji mpya hata mmoja badala yake ilipandisha vijana sita kutoka kundi hilo.

Nahodha wao, Mgaya Abdul (mdogo wake Juma Abdul Mgaya), Dizana Issa, Ismail Gambo pamoja na wengine niliowataja hapo juu wakapandishwa mapema mwanzo wa msimu. Yeye akasubiri hadi mzunguko wa pili wa msimu ndipo akapandishwa. Japo siku ya kwanza kuichezea timu kubwa alikuwa na Mudathir na Gadiel Michael.  Ilikuwa Februari 26, 2014 dhidi ya Ashanti United. Huo pia ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Idd Seleman ‘Nado’ akipandishwa kutoka akademi ya Ashanti United.

BAJA 06

2. MIKOPO

Bajana wakati ule alikaribia kuachwa kikosini baada ya mikopo kadhaa. Baadhi ya viongozi waliamini atakuja kuisaidia timu baadaye lakini wengine wakataka aachwe kwa sababu hawakuona hilo.

Baada ya majadiliano ikakubaliwa atolewe kwa mkopo...na ikawa mikopo!

Mkopo wa kwanza ulikuwa Januari 2015 alipotolewa kwenda Ndanda ili kupata muda zaidi wa kucheza baada ya ufinyu wa nafasi kwenye kikosi.

Mkopo wake ulipoisha akarudi Chamazi, lakini bado akaonekana hawezi kupata nafasi, akatolewa tena kwa mkopo kurudi Ndanda msimu wote wa 2015/16. Safari hii akiwa na Abdalah Kheri Sebo.

Msimu huo ulipoisha akarudi Chamazi, lakini bado akaonekana hajamomaa akapelekwa Mbeya City msimu wa 2016/17. Akarudi Chamazi 2017/18, lakini akaonekana hatoshi akapelekwa tena kwa mkopo KMC 2018/19. Baada ya msimu huo akarudi Chamazi kupambania namba na ndio hakutoka tena hadi sasa anapoondoka.

BAJA 02

3. CHUPUCHUPU AONDOSHWE

Baada ya msimu wa 2019/20, kocha wa Azam wa wakati huo, Aristica Cioaba alisema hamhitaji Bajana msimu wa 2020/21. Sambamba naye Cioaba hakumhitaji Salmin Hoza, Mwadin Ali, Joseph Mahundi na Idd Kipagwile. Mwadini alikuwa ameshamaliza mkataba wake.

Akaachwa. Mahundi alibakisha miezi sita akalipwa chake na kuendelea na maisha. Hoza na Bajana walibaki na mikataba mirefu hivyo wakatakiwa kutolewa kwa mkopo. Hoza akaenda Dodoma Jiji kimbembe kikabaki kwa Bajana.

Hadi dirisha linafungwa hakupata timu hivyo akabaki Azam. Lakini, Cioaba alishasema mchezaji huyo hayumo kwenye mipango yake kwa hiyo si sehemu ya kikosi chake. Bajana akabaki akifanya mazoezi na timu ya vijana kwa sababu hakutakiwa kwenye timu ya wakubwa.

Msimu ukaanza na Azam wakashinda mechi saba mfululizo. Cioaba akawa shujaa. Lakini ghafla mambo yakabadilika. Wakafungwa mechi ya nane, wakatoa sare ya tisa, wakashinda ya kumi. Halafu vikaja vipigo viwili mfululizo - Cioaba akafukuzwa kazi.

Desemba 2020 akaja kocha mpya, George Lwandamina. Yeye akataka kuwaona wachezaji wote wa Azam na Bajana akawemo. Lwandamina akampenda na kumfanya kuwa sehemu muhimu ya kikosi chake.

Na hata manahodha, Aggrey Moris, Salum Abubakary ‘Sure Boy’ na Mudathir waliposimamishwa akamteua Bajana kuwa nahodha. Yaani kutoka kutohitajika kikosini hadi kuwa nahodha. Mambo yalienda haraka sana.

BAJA 03

4. ALIPONEA HAPA

Januari 2021 Azam ikiwa na Lwandamina ilitolewa na Yanga kwa mikwaju ya penalti nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi.  Lakini, Lwandamina kama kocha mpya, akaomba kwa viongozi timu iendelee kubaki Zanzibar kwa mazoezi zaidi. Wachezaji waandamizi hawakufurahia.Walitaka warudi kupumzika. Lwandamina akalalamika kwa uongozi wanamkwamisha.

Viongozi walishtuka kutosikia jina la Bajana kwa sababu hilo ndio lilikuwa genge lake. Ilikuwaje Bajana asiwe katika kundi hilo?

Na hata baadaye mwakwa huo wachezaji ‘waasi’ waliposimamishwa kwa utovu wa nidhamu, Bajana hakuwa nao na ndicho kisa cha kupewa unahodha.

BAJA 04

5. SAKATA LA MKATABA

Mkataba wa Bajana ulitakiwa kumalizika 2022/23.

Mazungumzo ya mkataba mpya yalikuwa magumu kutokana na mahitaji ya mchezaji huyo. Wakati huo Azam ilikuwa chini ya kocha wa muda, Kali Ongala. Miezi michache kabla ya kumalizika kwa msimu, Azam wakapata kocha mpya atakayechukua timu msimu ujao wa 2023/24.

Kocha huyo alikuwa Yousouph Dabo kutoka Senegal. Dabo akaja na akawa anatembea na timu ili kuijua zaidi kabla hajaanza kazi. Akawa anawatathmini wachezaji wake mmoja baada ya mwingine na ndipo alipompa nafasi kubwa Bajana kwenye kikosi msimu uliofuata. Hivyo akawaambia viongozi wafanye wanaloweza kumbakisha kwa sababu yupo kwenye mipango yake.  Hata hivyo, haikuwa rahisi kwani siku ya mchezo wa mwisho wa ligi Bajana alikuwa hajasaini na hajui hatima yake. Akautumia mchezo huo dhidi ya Polisi Tanzania kuaga mashabiki baada ya filimbi ya mwisho. Aliamini mazungumzo ya mkataba mpya yameshindikana na hivyo hatakwepo msimu ujao.

Lakini kumbe wakati mchezo unaendelea wawakilishi wake walifikia makubaliano na klabu.

Hivyo akasaini baada ya mchezo ule huku akiwa ameshaaga. Hii ni sawa na kilichotokea mwaka huu kwa kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez aliaga kabisa kwa mashabiki lakini akaishia kubaki.

BAJA 05

6. UNAHODHA

Septemba 2021 Bajana alipewa unahodha na Lwandamina baada ya Agrey Moris kusimamishwa. Desemba Aggrey akarudi na kuchukua nafasi akawa mmoja wa wasaidizi.

2023 Aggrey akastaafu na Bajana akawa na matumaini ya kurudia unahodha.

Lakini Dabo hakutaka, hivyo akamteua Daniel Amoah kuwa nahodha na Lusajo Mwaikenda kuwa msaidizi. Bajana akatolewa kabisa kwenye mfumo.

Na hii ni kutokana na mivutano kadhaa kati ya Bajana na Dabo iliyotawala uhusiano kama kocha na mchezaji. Mivutano hiyo ilisababisha wawili hao kutozungumza - hata salamu, lakini waliendelea kufanya kazi pamoja. Japo walikuwa hawasalimiani, lakini kazini walizungumza.

Dabo alimtegemea  Bajana katika kikosi na Bajana alimkubali Dabo kwa mbinu zake. Katika mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania, Bajana ambaye alifunga bao la dakika ya kwanza na kisha kuumia na kutoka, alimfuata Dabo na kumshauri afanye mabadiliko..

Dabo akafanya hivyo na kweli Nado akaleta tofauti. Kwani hadi dakika ya 85 matokeo yalikuwa 1-1 ndipo Nado akaingia na kufunga bao la ushindi. Majeraha aliyopata hapo yakamuweka nje hadi mwisho wa msimu wa 2023/24. Na hata msimu wa 2024/25 ulipoanza hakuwa amepona. Dabo akafukuzwa baada ya mechi moja ya ligi ya msimu mpya. Lusajo Mwaikenda ambaye alibaki kama nahodha baada ya Amoah kuondoka akamrudishia Bajana unahodha wake.

Hata kocha mpya, Rachid Taoussi alipokuja alikuta Bajana amesharudishiwa kitambaa. Na ndicho alichokuwa nacho hadi sasa anapoondoka!