Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sitaki tena Urais – Sehemu ya 31

RAIS 31 Pict

ILIKOISHIA

Mimi niliruka chini. Yeye akashuka kwa kukumbatia ule mti.

Tulipokuwa chini, nikamuuliza:

“Sasa tunakwenda wapi?”

“Kuna hoteli moja inayotoa huduma saa ishirini na nne. Tutakwenda na bodaboda.”

Kwa vile mimi nilikuwa mgeni na mwenyeji alikuwa yeye, sikumuuliza ni hoteli gani.

Tukatembea kwa miguu kuelekea barabarani. Mimi nilikuwa na wasiwasi kwa vile ulikuwa usiku mwingi, lakini mwenzangu hakuwa na wasiwasi hata chembe..

SASA ENDELEA


TUKAFIKA barabarani na palikuwa na kituo cha pikipiki  za bodaboda. Akakodi pikipiki moja ambayo tulipanda mshikaki. Alitangullia yeye kukaa kwenye siti, mimi nikakaa nyuma yake. Ilibidi tugandamiane ili niwee kukaa vizuri. Katika kufanya hivyo niliona maajabu. Msichana alikuwa akinukia hewa tamu ambayo katika maisha yangu sikuwahi kuisikia hata siku moja.

Nguo ake zilikuwa inanukia manukato yaliyokuwa yakinisisimua. Nywele ake zilikuwa na harufu mbali. Sikujua zilikuwa zinanukia harufu gani jamani. Lakini ilikuwa harufu nzuri kama ya mawaridi.

Baada ya mwendo mfupi wa pikipiki tukatokea kwenye hoteli moja iliyokuwa inapigwa muziki. Tukashuka kwenye pikipiki. Zena ndiye aliyemlipa mwenye bodaboda. Tukaingia mle hotelini.

‘utakula nini?” Zena akaniulia wakati tunakaa kwenye viti.

“Kuna chakula gani?”

“Muda huu chakula kilichopo ni chipsi na ndizi za kuchoma.”

“Nitakula chipsi.”

Zena akamuita mhudumu na kuagia chipsi na nusu kuku sahani mbili na soda mbili. Bada ya muda kidogo tukaletewa chakula tulichoagiza. Zena akanikaribisha.

“Karibu tule.”

“Asante.”

Tukaanza kula. Wakati wote tubqjula nilikuwa nikimuwaza Yule msichana. Nilikuwa nikijiuliza kwanini kwana alikuwa joka kisha akabadilika na kuwa binaadamu na kwanini alikuwa anekaa juu ya mti? Maswali hayo sikuweza kuyapatia majibu. Kwa vile alikuwa ndiye mwenyeji wangu ilinibidi nimuamini a kumfuatisha.

Baada ya kula Zena aliniuliza kama nilishiba. Bukamjibu kuwa nimeshiba, Baada ya kulipa pesa akaniambia.

“Twendezetu.”

Tukatoka nje ya ile hoteli na kukkodi pikipiki nyinginr ya bodaboda. Tulikaa mshikaki kama mwanzo. Kusema kweli hewa ya Yule msichana pamoja na manukato aliyojitia nyweleni na kwenye nguo zake viliniliwaza sana.

Pikipiki ilitupeleka mahali palipokuwa na ulemti. Lakini kitu cha ajabu nilichokiona ule mtu haukuwepo tena. Badala yake tuliona jumba la kifahari lililokuwa ndani ya geti.

Tuliposhuka kwenye pikipiki Zena alifugua mlango wa geti akaniambia.

“Karibu ndani.”

Aliingia yeye kwanza kisha nikaingia mimi. Lilikuwa ni jambo lililonishangaza sana. Kule kuingia humo ndani niliingia kwa sababu sikuwa na jinsi lakini nisingeingia. Nikalitazama lile jumba kwa ndani. Kwa kweli lilionesha lilikuwa jumba lililogharimu pesa nyingi.

Zena alikwenda kufungua mlango wa kuingilia kwenye jumba hilo. Nikiwa nimenywea nilikuwa nikimfuata nyuma huku nikimuogopa.

“Karibu.” Akanikaribisha tena. Pengine alishaniona kuwa nimegwaya.

Tukaingiandani ajumba hilo.

“Karibu ukae.’ Zena akaniambia kwa upole.

Nikakaa kwenye masofa yaliyokuwa yanapendeza. Nilikaa kwa uoga na kutojiamini.

“Jisikie uko nyumbani.” Zena akaniambia huku akiketi knda yangu.

Pengine alishazitambua hisia zangu.

Kila nilichokiona humo ndani kilikuwa cha thamani.

“Hapa ndiyo nyumbani kwangu.”

Nilitaka kumuuliza , :Mbona hii nyumba haikuwepo hapo mwanzo, imetokea wapi?” Lakini kulikuja kitu kikanizuia kuuliza hivyo.

Pia nilitaka kumuuliza kama ile nyumba ilikuwa mali yake. Kwa jinsi nilivyokuwa nimegwaya sikuweza kuuliza chochote. Nikawa nalifikiria lile begi langu nililoliacha juu ya mti ambalo lilikuwa na suruali yangu na Tsheti yangu ya akiba.

Ili nisikae kimya sana nikajikuta nikimuuliaza.

“Unaishi hapa?”

“Ndiyo ninaishi hapa.”

“Unaishi mwenyewe?”

“Ndiyo ninaishi mwenyewe, ulidhani nina mume?”

“Nilidhani labda unaishi na wazazi.”

“Hapana. Wazazi wangu wako Zanzibar.”

“Sasa unaishije hapa peke yako?”

“Ninaishi. Kama nitakuwa na mwenzangu utakuwa wewe.”

Kimoyomoyo nilihuana nikajiambia.

“Mimi nina hadhi gani ya kuishi na wewe?”

Kama vile aliyasikia mawazo yangu msichana akacheka.

Nikjishitukia na kumuuliza.

“Unacheka nini>:

“Si nimekupenda mwenyewe.” Akaniambia na kuinuka.

“Njoo.”

Nikainuka na kumfuata. Alikwenda kufungua mlango wa chumba kimojawapo akaingia.

“Karibu na huku.”

Na mimi nikaingia katika kile chumba. Kilikuwa chumba kipana kilichokuwa na kitanda kipana sana kilivhotandikwa vizuri. Upande wa mchagoni kulikuwa na bikabati viwili, kimoja kila upande wa kitanda.

Nikashituka nilipoliona begi langu nililoliacha kwenye mti likiwa kwenye godoro.

“Si begi langu hili?” nikamuuliza Yule msichana.

Zena naye akaniuliza. Kwani uliwahi kuingia humu?”

“Nililiacha juu ya mti.”

Zena akacheka.

“Ndilo hilo begi lako. Ulifikiri limrpotea?”

“Ni kweli. Nilijua limepotea.”

“Si nilikwambia liachetu halitaibiwa wala  kupotea.”

“Uliniambia.”

“HIki ndio chumba change.”

“Unalala humu?”

“Na wewe pia utalala humu.”

Nikawa nimeduwaa. Zena alikuwa akinitazama. Nilipomtupia macho akawa anacjeka.

“Acha tukaoge kwana.”

Aliponiambia hivyo Zena aligeuka upande mwingine akavua nguo ake ote mbele yangu na kuchukua taulo akajifunga. Alijifunga kuanzia kifuani hadi karibu na magoti. Taulo nyingine akanirushia mimi.

Nikavua shati langu. Sikujua ningeliweka wapi. Nikachukua lile begi langu nikalifungua na kulitia shati hilo. Nikafungua mkanda wa suruali kisha nikafunga ile taulo. Nikaiachia suruali iteremke chini. Nayo nikaitia kwenye begi.

Msichana akanishika mkono na kuniongoza hadi kwenye mlango wa bafuni.

Nilichokikumbuka ni Zena kufungua mlango wa bafu akaingia akiwa amenishika mkono. Na mimi nikaingia. Sikukumbuka tena kitu kingine kilichotokea.

Kwa mbali nikajihisi kuvuta ile hewa ya Zena hasa ya nywele zake. Nikahisi kama fahamu ilikuwa zikinirudia kidogodogo. Nikafumbua macho yangu na kumuona Zena amelala kifuani kwangu. Nilihisi kama alikuwa amelala usingizi. Tulikuwa tumelala kwenye kile kitanda kipana. Miili yetu ikiwa imefinikwa shuka kuanzia nyayoni hadi kifuani.

Kwa vile nilihisi kwamba Zena alikuwa amelala sikutaka kujitikisa nikihofia kuwa ningemuamsha. Nikanyamaa kimya lakini akilini mwangu nilikuwa nikijiulia tulilala muda gani pale kitandani? KUmbukumbu zangu ziliishia tunaingia bafuni. Sikukumbuka jinsi tulivyooga na tulivyotoka humo bafuni. Sikukumbuka baada ya kutoka bafuni tulifanya nini. Nilichokiona wakati ninazinduka ni kumuona Zena amenilalia.

Nikajiuliza ni kitu gani kilirusha fahamu zangu wakati tunaingia bafuni. Nilikuwa nimeshikwa na usingizi? Hata kama ulikuwa usingizi usingizi gani unamshika mtu wakati anatembea au yuko wima? Sikupata jibu.

Licha ya hofu na wasiwasi nilivyokuwa navyo nilihisi rah asana kulaliwa na Yule msichana kifuani huku hewa yake ikihinikiza pua yangu. Nilitamani yuendelee kulala vilevile kwa muda mrefu.

Kwa vile taa yenye mwanga hafifu ya rangi ya bluu ilikuwa inawaka mle chumbani nikawa nazitazama nywele za Yule msichana. Kwanza nilidhani alikuwa amevaa wigi akini baadaye niligundua zilikuwa ni nwele zake halisi. Zilikuwa ndefu na zilizojaa kichwani.

Nikaja kugusagusa ngozi yake na kuichunguza. Ngozi yake ilikuwa laini kama ya motto mchanga. Nilishinfwa kugundua kama ni losheni iliyoiweka ngozi yake kuwa hivyo.

Sasa nikawa naraka kufunua shuka ili niuone mwili wake. Nikamuona Zena akifurukuta. Nikatulia. Alifurukuta  akakiondoa kichwa chake kwenye kifua change na kugeuka upande mwingine. Nilidhani angeamka lakini akaendelea kulala.

Simu yangu ilikuwa imewekwa kwenye kikabati kilichokuwa mchagoni mwa kitanda upande wangu. Nikanyoosha mkono na kuichukua. Nilitaka kutaama saa nijue ilikuwa saa ngapi.

Nilipotazama saa nilishituka nilipoona ilikuwa saa kumi na mbili asubuhi. Kumbe kulikuwa kumeshakucha. Masaa yote nililala na Zena bila kujijua.

Kitu ambacho nilishindwa kukijua ni je nilikuwa nimepotewa na fahamu nilipokuwa bafuni na Zena akaniogesha na kuja kunilaza kitandani? Au nilikuwa timamu ila nimepoteza kumbukumbu ya vitendo nilivyofanya, kwamba nilioga mwenyewe nikatoka bafuni kwa miguu  yagu na kuja kitandani?

Nikaendelea kujiuliza, kama nilikuwa timamu bila shaka nilitenda mambo mengi bila mimi mwenyewe kukumbuka.

Na ni kwanini imekuwa hivyo? Nikajiuliza.

Maswali yote niliyojiuliza sikuwa na majibu nayo. Nikabaki kama mjinga kuangalia  nini kitatokea.

Hata hivyo tayari nilishapata shaka kwamba yule msichana hakuwa wa kawaida. Kitu ambacho kilinipa moyo wa kuendelea kuwa naye ni kwamba nilikuwa nimempenda na alikuwa mzuri. Na yeye pia alikuwa ameonesha kunipenda.

Ghafla msichana huyo alijinyoosha kisha akainuka na kukaa kitandani. Nilijitahidi nione matiti yake lakini sikuyaona. Wakati wote alikuwa amekiziba kifua chake kwa kutumia shuka tuliokuwa tumejifinika.

“Asubuhi njema Karim,” akanisalimia.

“Njema na kwako Zena,” nikamjibu.

“NI saa ngapi sasa?”

“Ni saa kumi na mbili asubuhi.”

“Nakwenda maliwatoni.”

Alishuka kwenye kitanda akiwa ameishika shuka tuliokuwa tumejifinika. Akajifunga nayo kwenye kifua na kuniacha wazi. Nilipojiona nipo mtupu nilishuka kitandani nikavaa nguo yangu ya ndani iliyokuwa iko chini kisha nikakaa kitandani.

Baada ya dakika kadhaa, Zena akarudi akiwa amevaa taulo. Alikuwa ameshaoga.