Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sitaki tena Urais – Sehemu ya 29

Muktasari:

  • Pia alimueleza jinsi alivyokubali kujiunga na freemaso na kutoa ahadi ya uongo kuwa atamtoa mwanawe pindi atakapopata urais.

Ilikoishia

Hapo ndipo Shanga alipomueleza mke wake ukweli wote. Alimueleza jinsi alivyoshawishiwa na watu wawili ajiunge na freemaso ili apate urais katika ule uchaguzi wa kwanza.

Pia alimueleza jinsi alivyokubali kujiunga na freemaso na kutoa ahadi ya uongo kuwa atamtoa mwanawe pindi atakapopata urais.

Akamueleza jinsi alivyokuja kuwageuka freemaso na kujitoa katika undi lao alipopata urais. Akamueleza kuhusu kifo cha mtoto wao wa kwanza ambaye mwili wake haukupatikana.

SASA ENDELEA


Akamueleza kuhusu uasi wa kijeshi uliotokea ambao ulisababishwa na kundi hilo na akamueleza jinsi alivyowaweka kizuizini viongozi saba wa kundi hilo na baadaye kuwaachia baada ya kutekwa kwa Otis nchini Canada.

“Kwa vile sasa nimechaguliwa tena kuwa rais wanataka wamchukue Otis kama walivyomchukua yule wa kwanza. Nimewambia kama ni huo urais nitauacha lakini mwanangu wasimchukue” Shanga alimueleza mke wake.

Joyce alikuwa ameangua kilio kusikia habari za kifo cha mwanawe wa kwanza.

“Mume wangu ulikuwa una siri kubwa uliyokuwa unanificha”

“Najua nilifanya kosa lakini sikujua kama yangetokea haya”

“Kumbe mwanangu aliliwa…!. Imenitia uchungu sana”

“Hayo yameshapita mke wangu, usiyawaze tena. Kesho najiuzulu urais”

“Una uhakika gani kama Otis ni mzima?”

“Ni mzima kwa sababu wameniambia nikiacha urais na mwanangu atapona”

“Hebu mpigie tumsikie”

Shanga alishindwa kumwambia kwamba alishampigia lakini hapatikani. Akampigia tena.

“Hapatikani” alimwambia mke wake baada ya simu ya Otis kutopatikana.

“Atakuwa salama kweli?”

“Nadhani atakuwa salama, pengine amezima simu tu. Kama wangemchukua wangeniambia wazi”

Joyce akatikisa kichwa.

“Mimi siamini kama mwanangu yuko salama”

“Tutajua hapo asubuhi”

Usiku huo watu hao wawili hawakulala kwa kihoro cha kuuawa kwa Otis.

Mara kwa mara Shanga alikuwa akijaribu kuipiga simu ya Otis bila mafanikio.

Ilipofika saa 12 asubuhi ndipo simu ya Otis ilipopatikana.

“Uko wapi Otis?”

“Niko nyumbani, ndio nimeamka…”\\

“Tangu jana nakutafuta kwenye simu, sikupati”

“Nilizima simu usiku, jana nililala mapema”

“Lakini upo salama?”

“Nipo salama baba”

“Sawa. Nitakupigia baadaye”

“Sawa baba”

Shanga akakata simu na kumtazama mke wake.

“Otis ni mzima. Alikuwa amezima simu. Sasa tuondoke hapa katika nyumba ya serikali twende katika nyumba yangu. Nitatangaza kujiuzulu urais nikiwa huko”.

Mpaka inafika saa mbili asubuhi Shanga na mke wake walikuwa katika nyumba yao binafsi iliyokuwa kando kidogo ya jiji hilo. Shanga alimpigia katibu wake na kumtaka amuitie nyumbani kwake viongozi wa chama chake na baadhi ya maofisa wa serikali aliowataja kwa majina.

“Wafike nyumbani kwangu kabla ya saa tatu. Nina taarifa muhimu ya kuwapa” Shanga alimwambia katibu huyo.

Viongozi wa chama cha UM na baadhi ya maofisa wa serikali walifika nyumbani kwa shanga dakika chache kabla ya saa tatu. Shanga aliwakaribisha na kuwambia.

“Nimewaita kuwaarifu kuwa SITAKI TENA URAIS. Ninajiuzulu.”

Aliposema hivyo alikabidhi barua ya kujiuzulu kwa katibu wake kisha akanyanyuka na mke wake na kuondoka kwa gari.

Watu waliokuwa hapo walikuwa wamepigwa na butwaa kwani tukio hilo lilikuwa la ajabu na lisilo tarajiwa.

Akiwa kwenye gari Shanga alimpigia simu Otis.

“Uko wapi mwanagu?”

“Niko hoteli ninapata kifungua kinywa”

“Mwanangu nimejiuzulu urais, sasa hivi mimi si rais tena wa Kamisa”

“Kwanini baba umefanya hivyo?”

“Ni historia ndefu mwanagu nitakueleza tutakapokutana. Hivi sasa mimi na mama yako tunarudi kijijini kwetu tukajishughulishe na shughuli za kilimo. Natumaini kuwa utatufuata huku”

Walipofika  kijijini kwao Shanga alikutana na Maloto aliyekuwa amehamia kijijini baada ya nyumba yake kuungua akamueleza kwamba alikuwa amejiuzulu na Maloto akamueleza kwamba alikuwa ameacha shughuli za uganga.

“Kwanini?” Shanga akamuuliza.

“Nimetengana na majini wangu.”

“Kwanini mtengane?”

“Itabidi kwanza nikueleze historia yangu ya kuwapata hawa majini.”

“Nieleze.”

“Sababu ya kuwa pata majini hawa ni mtandao wa Face book. Nilipokuwa Tanzania nilikuwa na rafiki mmoja  wa face book. Aliniunga urafiki nikamkubalia.

Alikuwa msichana mrembo ambaye katika maisha yangu sikuwahi kuona mfano wake. Katika maelezo yake aliniambia alikuwa anaitwa Zena binti Jabalkeys. Hakuwa ameolewa. Alikuwa ametoka Zanzibar na alikuwa mkazi wa Dar es Salaam, maeneo ya Tegeta.

Nilipotazama orodha ya marafiki zake niliona watu watatu tu na wote walikuwa wanaume. Nilipoingia kuwachunguza marafiki  hao niligundua wawili walikuwa wakazi wa Dar na mmoja mkazi wa Tanga.

Baada ya kumkubalia urafiki mara moja nikawa naona post zake. Alikuwa akituma post za picha zake zilizomuonesha akiwa katika mazingira tofauti. Baadhi ya picha zilimuonesha akiwa katika maeneo ya mjini. Picha nyingine zilimuonesha akiwa maeneo yasiyofahamika kama vile kwenye majabali na kwenye msitu. Kuna siku alituma picha iliyomuonesha akiwa katika mji wa ajabu na uliokuwa na watu wa ajabu. Picha ambayo alikuwa akipenda kuituma mara kwa mara ni picha iliyoonesha joka kubwa lililokuwa na macho makali. Chini ya picha alikuwa akiandika DRAGON.

Siku ile niliyomkubali uarafiki akanitumia salamu Inboksi.

“Hujambo?”

Nikamjibu.

“Sijambo. Umzima?”

Kwa vile alikuwa online akanijibu hapo hapo.

“Ni mzima, hofu kwako.”

Nikapata shauku ya kuendelea kuchati naye.

“Mimi nashukuru. Uko pande zipi?”

Majibizano yetu yakawa kama ifuatavyo.

“Niko Dar, wakati mwingine Zanzibar.”

“Dar sehemu gani?”

“Tegeta. Wewe uko wapi?”

“Niko Moro”

Ule mtiririko wa majibizano yetu ukanipa raha ya kuendelea. Sasa nikaanza kumtongoza. Lakini nilianzia kwenye uchumba. Kama ni uarafiki tayari tulikuwa marafiki.

“Una mchumba?” Nikamuuliza.

“Sina mchumba,sijafikiria kuolewa bado.”

“Kuolewa ni mpaka ufikirie?”

“Ndiyo.”

“Una rafiki wa kiume?”

“Pia sina.”

“Mrembo kama wewe unakosa  rafiki wa kiume kweli.”

“Labda utakuwa wewe.”

Sijui niseme nilikuwa bwege wa wasichana. Alivyoniambia labda nitakuwa mimi, nikaona moyo wangu unapoa. Nikajikuta nikimwambia.

“Asante.”

“Asante na wewe kwa kukubali ombi langu la urafiki.”

Msichana alizidi kunitia moyo mpaka nikathubutu kumwambia.

“Natamani sana tuonane.”

“Njoo Dar, tutaonana.”

“Nije lini?”

“Siku yoyote utakayopenda.”

“Basi acha nijiandae, nitakufahamisha.”

“Ungependa tuongee kwenye simu?”

“Ndiyo.”

“Nitumie namba yako.”

Nikamtumia namba yangu. Baada ya muda kidogo nikaona ameondoka online. Ilikuwa kama ndio tumeagana. Nilipoona hivyo niliondoka Facebook nikazima data na kuiweka simu kwenye meza.

Muda kidogo nikaona namba inapiga. Ilikuwa namba ngeni. Nikaichukua simu na kuipokea.

“Hello…”

Zilichukua sekunde kadhaa hadi sauti ilipojitokeza kutoka simu ya upande wa pili. Ilikuwa sauti tamu ya msichana mwenye lafudhi ya Kimombasa.

“Hello….ndiyo namba yangu…..”

“Ndiyo namba yako, nani wewe?”

“Mimi Zena binti Jabalkeys.”

“Oh Zena…Ndiye wewe…nimeiona namba yako.”

“Uko wapi muda huu?”

“Niko nyumbani.”

“Unafanya nini?”

“Nimekaa tu chumbani kwangu.”

“Unawaza nini?”

“Maisha….”

“Maisha yana nini Karim?” ( Karimu ndilo jina nililojisajili nalo kwenye Face Book)

“Unajua mimi bado kijana ndiyo kwanza ninayaanza maisha…..”

“Usijali. Tatizo hilo si lako peke yako. Lakini utakapokuwa na mimi tutasaidiana.”

Maneno yake yakanipa tamaa ya kupata msaada wa kimaisha. Nikawaza kwamba pengine Zena alikuwa tajiri au alikuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa vizuri.

“Unashughulika na nini?” Nikamuuliza.

“Biashara tu.”

“Biashara gani?”

“Mmh…Karim ni mapema mno kujua kila kitu changu. Tutazungumza tutakapokutana.”

“Hakuna tatizo.”

“Ukimchunguza sana kuku hutaweza kumla.”

Sikumuelewa lakini nikajidai kucheka na kumjibu.

“Ni kweli.”

Pakapita kimya kifupi kabla ya kumuulia.

“Unaishi na wazazi wako au….?”

“Tutakuja kuzungumza.”

“Sawa. Unaonaje nikija huko siku ya jumamosi na jumalili jioni nikarudi Moro?”

“Unataka uje jumamosi ya wiki hii?”

“Ndiyo.”

“Sawa. Unaweza kuja ukalala kwangu, jumapili jioni ukarudi Moro.”

“Basi nitakuja jumamosi.”

“Sawa.”

Baada ya mazungumzo hayo msichana huyo akaniambia..

“Usiku mwema.”

“Na kwako.”

Akakata simu. Nikaiandikisha namba yake kwenye simu yangu kwa kutumia jina la Zena.

Siku ile nilipoungumza na Zena ilikuwa usiku. Mpaka tunamaliza kuzungumza ilikuwa karibu saa tano usiku.

Usingizi ukaniruka kidogo kutokana na mawazo. Nilimuwaza sana usiku ule. Kikubwa kilichonifanya nimuwaze sana ni ukweli kwamba katika maisha yangu sikuwahi kusuhubiana na msichana jamali na mtembo kama alivyo Zena.

Pia nilijiambia kama Zena atakuwa binti wa tajiri, anaweza kunisaidia kimaisha. Kama alivyoniambia mwenyewe tutakapokutana tutasaidiana.

Nikapata ushawishi wa kwenda Dar ili nionane naye na kama wanavyosema vijana wa kileo tuyajenge.