Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sitaki tena Urais – Sehemu ya 20

RAIS 20 Pict

ILIKOISHIA

Herman na Deo walikuwa wakitazamana mara kwa mara waliposikia maneno yaliyokuwa yakimsakama Rais Shanga.

Walifahamu na kuamini kuwa kazi nzito ilikuwa inawasubiri, kwani watu hao walionekana kutotii serikali.

Wakati makachero hao wakiyatafakari maneno yaliyokuwa yakizungumzwa, walishitushwa walipoisikia ile sauti ikisema:

“Leo kuna sura mbili ngeni. Tungependa watu hao ambao wanajifahamu kuwa hawahusiki humu ndani wafike hapa mbele!”

SASA ENDELEA


DEO na Herman wakatazamana, nyuso zao zikiwa zimetaharuki. Walishatambua kuwa walikuwa wanasemwa wao. Lakini hakukuwa na yeyote aliyekuwa tayari kunyanyuka kwenye kiti.

Kila mmoja alikuwa akijiuliza ni muda gani yalifanyika mawasiliano kuwa kuna wageni walioingia wakati hakukuwa na mtu yeyote aliyeonesha kuwajali.

“Mnaojitambua kuwa ni wageni humu ndani mfike hapa mbele” Ilikuwa sauti ya Osaka aliyekuwa amesimama mbele karibu na meza kuu.

Deo alimuonesha ishara Herman kuwa wainuke na waende kule wanakoitwa. Walinyanyuka kwa pamoja na kutembea kikakamavu kuelekea ilikokuwa meza kuu.

“Karibuni sana” Osaka aliwambia mara tu walipofika karibu yake.

“Asante, tunashukuru” Deo alimjibu.

“Nyinyi ni kina nani na mnatoka wapi?”

Deo na Herman walitoa vitambulisho vyao na kumuonesha Osaka.

“Sisi ni maofisa upelelezi kutoka makao ya plisi. Tulikuwa tunafuatilia mikutano yetu” Herman akamwambia Osaka.

“Mbona hamkujitambulisha kabla?”

“Tulikuja kwa ajili ya kufanya upelelezi, tusingeweza kujitambulisha kabla”

“Mmekuja kupeleleza nini hapa?”

“Kupeleleza kama mnaendelea na shughuli zenu wakati serikali ilishawapiga marufuku” alimjibu Deo.

“Tulishamwambia Rais kuwa hawezi kutupiga marufuku kwa sababu kuwepo kwetu kunatambulika kimataifa”

“Kwa hiyo mlikuwa mnavunja amri halali ya serikali?” Herman akamuuliza Osaka.

“Serikali ni ya nani? Serikali ni yetu! Nyinyi hamuwezi kujua hilo”

“Sawa. Sasa sisi tumemaliza kazi yetu tunaondoka”

Deo na Herman waligeuka na kuelekea kwenye ngazi za kutokea.

“Msiondoke…hebu rudini hapa!” Osaka akawambia.

Deo na Herman hawakumsikiliza, waliendelea kwenda. Walipofika kwenye ngazi Deo alitoa simu na kumpigia mkuu wa kikosi cha polisi kilichokuwa kinawasubiri nje.

“Sasa mnaweza kuingia, wameshamaliza shughuli zao”  Deo alisema kwenye simu huku wakipanda ngazi haraka haraka.

Osaka na wenzake wawili waliwafuata. Makachero hao waliwaona wakaharakisha kupanda ngazi. Walifika kwenye mlango wa ngazi wakawa wanaelekea kwenye mlango wa kutokea kwenye jumba hilo.

Huko nje mkuu wa kikosi cha polisi alibisha geti. Geti hilo lilifunguliwa na mlinzi. Askari wapatao kumi wakaingia wakiwa na bunduki.

Waliwaona Deo na Herman wakitoka ndani ya jumba hilo na nyuma yao kulikuwa na watu watatu wakiwafuata.

Osaka na wenzake wawili ndio waliokamatwa kwanza. Polisi walikwenda katika ukumbi wa chini na kuamrisha watu wote waliokuwa humo ndani watoke. Watu hao walitii amri na kutoka lakini kivuli kilichokuwa kwenye kioo kilikuwa kikiendelea kulaani.

“Serikali imepalia makaa ya moto…serikali imepalia makaa ya moto!”

Hakukuwa na polisi yeyote aliyejua mtu huyo alikuwa wapi na mara baada ya kusema hivyo mwanga wa kioo hicho ulitoweka, kukawa kimya kabisa.

Polisi hao hawakuwakamata watu wote. Wale waliojitaja kuwa viongozi wa kundi hilo ndio waliochukuliwa na polisi. Jumla walikuwa watu saba.

Baadhi ya polisi waliondoka na viongozi hao na baadhi yao walibaki katika jumba hilo kuweka ulinzi.

Ndani ya kituo kikuu cha polisi cha Maloto viongozi hao walikiri kuendelea na shughuli zao licha ya kupigwa marufuku na serikali. Pia walikiri kuwa kiongozi wao aliahidi kupambana na utawala wa Rais Shanga.

“Mtapambana na utawala wa Rais Shanga kwa namna gani?” Kachero Shamla aliyepewa jukumu la kuchunguza na kuandaa kesi ya viongzi hao alimuuliza Osaka.

“Hilo analijua kiongozi wetu”

“Ni yupi?”

“Hayuko hapa”

“Alikuwepo wakati nyinyi mnakamatwa?”

Alikuwepo lakini hakuna polisi anayeweza kumkamata”

“Kwanini?”

“Ssi tunaona kivuli chake tu. Yeye mwenyewe hatujawahi kumuona hata siku moja”

“Mnakiona kivuli chake wakati yeye mwenyewe akiwa wapi?”

“Akiwa kwenye chumba chake maalum”

“Hicho kivuli mnakiona kwa wapi?”

“Katika ukumbi wetu wa mikutano”

“Hicho chumba chake kipo wapi?”

“Kipo katika jumba letu”

“Sasa  kwanini unasema hamjamuona wakati anafika wenye jumba lenu?”

“Yeye ni mwiko kuonekana. Analetwa kwa gari maalum na walinzi wake wanne. Gari lake linaingia hadi ndani ya jumba letu karibu na chumba chake. Anaposhuka anaingia kwenye chumba hicho na kuendesha mikutano akiwa humo humo hadi anapoondoka”

Maelezo ya Osaka yalikuwa yakiwashangaza polisi waliokuwa wakimsikiliza na mara kwa mar walikuwa wakitazamana.

“Sasa tutarudi na wewe kwenye jumba lenu utuoneshe hicho chumba” Shamla alimwambia Osaka.

“Sawa twendeni”

Dakika chache baadaye Shamla na askari wengine watatu wa upelelezi na polisi sita waliokuwa na bunduki wakiwa wamefuatana na Osaka walirudi tena katika jumba hilo lililokuwa limewekewa ulinzi na polisi.

Polisi hao walilipekua jumba zima. Waliingia katika kila chumba hadi walipokigundua chumba alichokuwa anakitumia kiongozi wao waliyekuwa wanamuita Master.

Chumba hicho kilikuwa na kamera pamoja na vifaa maalum vilivyoweza kusafirisha kivuli cha Master hadi kwenye kioo kilichokuwa ndani ya ofisi ya Osaka na kwenye ukumbi wa mikutano. Polisi waligundua kuwa viooo hivyo vilikuwa maalum. Vilikuwa ni aina ya vioo vinavyotumika kwenye simu, televisheni na kompyuta.

Hata hivyo waliikuta ofisi ya Master ikiwa tupu. Mwenyewe hakuwepo.

“Anaishi wapi?” Kachero Shamla akamuuliza Osaka.

Osaka alibetua mabega yake.

“Hakuna anayejua anaishi wapi?”

“Si kweli. Ukweli ni kwamba mnajua lakini mnaficha. Sisi tutamtafuta na atapatikana. Tunataka atueleze jinsi atakavyopambana na utawala wa Rais Shanga”.

Katika kupekuepekua ofisi polisi walikamata nyaraka mbalimbali zikiwemo fomu za wanachama pamoja na picha zao. Fomu hizo zilichukuliwa kituo cha polisi kwa ukaguzi zaidi.

Wakati watuhumiwa hao waliokamatwa wamewekwa ndani, polisi na makachero walianza kuzikagua nyaraka walizozikamata.

Kulikuwa na zaidi ya fomu hamsini za wanachama. Kila fomu ilikuwa na jina na picha ya mwanachama. Polisi walianza kuigundua fomu ya kanali Mbasha aliyeongoza uasi nchini humo na kuuawa na maafisa usalama.

“Kumbe kanali Mbasha alikuwa mwanachama wao?” Polisi mmoja akauliza kwa mshangao.

“Wakati Mbasha anauawa ilisemekana alisema kuwa freemaso wamemponza” Polisi mwingine naye akasema.

Hapo hapo Kachero Shamla akaokota fomu ya Niwako aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani na hatimaye kufukuzwa kazi na Rais Shanga.

“Hii ni fomu ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani!” Shamla aliwambia wenzake.

Polisi waliokuwa hapo walipigwa na mshangao.

“Kumbe na yeye alikuwa mwanachama?” Polisi mmoja akauliza.

Ghafla Shamla tena akaiona fomu iliyokuwa na jina na picha ya  Rais Shanga!

“Hapa naona fomu yenye picha na jina la Rais Shanga!”

Polisi na makachero wote waliokuwa hapo walishikwa na mshangao.

“Nataka Osaka akatolewe aletwe hapa atueleze kuhusu hii fomu yenye jina la rais” Shamla aliwambia polisi.

Polisi mmoja alikwenda kumtoa Osaka na kumpeleka katika chumba hicho walichokuwemo polisi na makachero. “Tunataka utueleze kuhusu hizi fomu tulizozichukua katika ofisi yako” Shamla alimwambia Osaka.

“Nieleze kitu gani?”

Shamla alimuonesha Osaka fomu ya kanali Mbasha na kumuuliza.

“Huyu ni nani?”

“Jina lake na picha yake vinamuonesha”

“Ni kanali Mbasha?”

“Ndiyo”

“Alikuwa mwanachama wenu?”

“Ndiyo”

Shamla alichukua fomu nyingine iliyomuonesha aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani akamuonesha Osaka.

“Na huyu si ndiye aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani kabla ya kufukuzwa na rais?”

“Niye yeye”

Shamla sasa alimuonesha fomu iliyokuwa na picha na jina la Rais Shanga.

“Fomu hii ina jina la Rais Shanga na picha yake, unaweza kutueleza nini kuhususiana na Rais Shanga?” Shamla akamuuliza Osaka.

“Ni vizuri aulizwe rais mwenyewe, mimi siwezi kumsemea rais”

“Nimekuuliza wewe kwa sababu wewe ni kiongozi wa kundi hili na fomu hizi zimekutwa ofisini kwako”

“Mimi siwezi kumsemea rais kama ni mwanachama wetu au la. Ningependa aulizwe mwenyewe”

                                      ****************

Ilikuwa saa tatu asubuhi, Rais Shanga akiwa ofisini kwake ikulu alipojulishwa kuwa mkuu wa jeshi la polisi amefika ikulu akiomba kukutana naye.

Rais Shanga alitoa ruhusa mkuu huyo aingie ofisini kwake. Mkuu wajeshi la polisi alipoingia ofisini humo alisalimiana na rais na kumueleza kuwa kulikuwa na tatizo lililotokea kwa upande wa polisi.

“Tatizo gani?” Shanga akamuuliza. Mkuu wa Jeshi la pPolisi alifungua mkoba wake na kutoa fomu tatu za kundi la freemaso zilizokuwa na majina ya Rais Shanga. Kanal Mbasha na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani.