Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sitaki tena Urais – Sehemu ya 18

Muktasari:

  • “Sisi tukiondoka, na wewe utaondoka urudi kijijini kwa muda,” akamwambia.

Ilikoishia

Wakati wanajeshi hao wameingia katika chumba hicho, Mbasha alimtazama mke wake aliyekuwa mbele yake.

“Sisi tukiondoka, na wewe utaondoka urudi kijijini kwa muda,” akamwambia.

“Kwani nyinyi mtaelekea wapi?”

Kabla ya Mbasha kujibu, geti lilibishwa.

“Kuna mtu anabisha geti,” Mbasha akasema. “Hebu nenda kamsikilize.”

Mke wake alitoka na kwenda kwenye geti, akalifungua.

Maafisa wa usalama wapatao kumi wakaingia wakiwa na bastola mikononi.

“Yuko wapi Kanali Mbasha?” mmoja wao akamuuliza.

SASA ENDELEA


“HAYUPO”

“Wewe ni nani wake?”

“Huyo ni mke wake ninamfahamu” Afisa mwingine akasema.

“Mbasha yumo humu ndani. Gari walilopora lipo nje”

Mbasha mwenyewe alikuwa akiwachungulia kupitia kwenye dirisha. Aliposhuku kuwa walikuwa maafisa usalama alichomoa bastola yake aliyokuwa ameificha ndani ya koti. Aliondoka haraka kwenye dirisha na kwenda kuwambia wenzake.

Wenzake hao walitoka mle chumbani wakiwa vifua wazi. Waliwahi kubadili suruali tu.

“Tupambane nao, tuwaue humu humu ndani tuondoke!” Mbasha aliwambia.

Maafisa usalama hao walikuwa wamemshika mke wa Mbasha wakielekea naye mle ndani. Ghafla waliona risasi zikiwamiminikia.

Walimuacha mke wa Mbasha wakasambaratika!. Kila mmoja aliruka upande wake. Maafisa usalama wawili walianguka hapo hapo, mmoja alilengwa kwenye kichwa mwenzake kwenye kifua.

Mbasha na wenzake waliendelea kumimina risasi kupitia wenye dirisha na kwenye mlango. Maafisa usalama hao walikimbilia pembeni mwa nyumba ambako kina Mbasha hawakuweza kuwaona, wakawa wananyata pole pole kuelekea kwenye mlango.

Mke wa Mbasha alipoona ameachiwa alikimbilia kwenye mlango ili aingie ndani. Afisa mmoja aliwahi kumdaka kabla mwanamke huyo kuingia ndani. Akamtia kabari na kumuweka mbele yake kama kinga kisha akaingia naye ndani.

Kitendo hicho kiliwafadhaisha Mbasha na wenzake wakasitisha kufyatua risasi na hivyo kuwapa mwanya maafisa usalama kuwashambulia kwa risasi kupitia kwenye dirisha Mwanajeshi mmoja aliuawa hapo hapo na mwingine alijibu mashambulizi kwa kuwafyatulia risasi maafisa hao ambao walilazimika kuinama chini ya dirisha kukwepa risasi.

“Mikono juu nyote!” Afisa aliyemshika mke wa Mbasha alimwambia Mbasha na mwenzake akiwa amewaelekezea bastola yake.

Mbasha alikuwa ameshika bastola lakini alishindwa kufyatua risasi kwa kuhofia kumpiga mke wake aliyewekwa mbele ya afisa huyo ama kinga. Kadhalika mwanajeshi aliyekuwa naye hakuweza pia kufyatua risasi akawa anarudi kinyume nyume huku mdomo wa bunduki ameuelekeza kwa afisa aliyemshika mke wa Mbasha.

Hatari iliyokuwa hapo ni kuwa kama afisa usalama angefyatua risasi, mwanajeshi naye angefyatua kwa kutumia SMG aliyokuwa nayo.

Na kama mwanajeshi angetangulia kufyatua kulikuwa na hatari ya risasi kumpata mke wa Mbasha. Hivyo alioona arudi kinyumenyume ili atokomee kwa mlango wa nyuma.

Wakati mwanajeshi huyo ameielekeza bunduki yake kwa afisa usalama, Mbasha aliielekeza bastola yake kwenye dirisha ambako maafisa usalama wengine walikuwa wameinama chini ya dirisha hilo kwa nje. Alikuwa akisubiri atakayeinua kichwa amdungue! Na yeye alirudi kinyumenyume kumfuata mwenziwe.

Kumbe huko nje baadhi ya maafisa hao walizungukia mlango wa nyuma kuwazunguka Mbasha na mwenzake.

Mwanajeshi alimuweka Mbasha nyuma yake ili afungue mlango wa nyuma. Mbasha alifungua mlango. Alipofungua tu alipigwa risasi ya kifua akaanguka chini. Mwenzake akageuka haraka. Hapo hapo afisa aliyemshika mke wa Mbasha alimpiga risasi ya mgongo. Mwanajeshi huyo akaanguka chini.

Mke wa Mbasha alipoona mume wake amepigwa risasi aliminyana na afisa aliyemshika akitaka aachiwe. Afisa huyo alimuachia. Mwanamke huyo alimkimbilia Mbasha aliyeuwa amelala chini katikati ya mlango.

“Mume wangu umeuawa!” Mwanamke huyo alipiga kelele huku akijaribu kumuinua mume wake aliyekuwa akitokwa na damu kifuani.

Mbasha alikuwa hajakufa. Alikuwa amefumba macho na akipumua kwa nguvu. Aliposikia sauti ya mkewe alifumbua macho na kutazamana naye.

“Buriani mume wangu…”

Mbasha alijitahidi na aliweza kusema.

“Freemason… freemason wamenipoteza!”

Hapo hapo Mbasha alikata roho.

                                       ****************

Ilikuwa saa sita mchana, mkurugenzi wa usalama wa taifa alipotaka kuonana na rais. Wasaidizi wa rais walipomruhusu aliingia ofisini kwa rais.

“Karibu” Rais alimwambia. “Una lipi la kunieleza?”

Mkurugenzi huyo aliketi na kumwambia rais.

“Kanali Mbasha ameuawa”

Rais akashituka. Lakini ulikuwa mshituko wa faraja.

“Ameuawa wapi?”

“Kwenye nyumba moja ambayo inasemekana aliipangisha wakati anaandaa mpango wa kufanya uasi”

“Ameuawaje?”

“Baada ya kuilipua helikopta ya jeshi iliyokuwa inawafuatilia walipora gari la raia mmoja na kwenda nalo kwenye hiyo nyumba. Gari hilo lilionekana huko na tuliarifiwa nikatuma vijana kumi kulifuatilia. Walipofika waliliuta nje ya hiyo nyumba…”

Mkurugenzi wa usalama aliendelea kumueleza rais kilichotokea ndani ya nyumba hiyo hadi Mbasha na wenzake wakauawa.

“Mke wake tunamshikilia kwa ajili ya mahojiano”

“Kuna chochote ambacho mke wake amekieleza?”

“Ndiyo anaendelea kuhojiwa, baadaye nitapata taarifa zake. Lakini kuna kitu ambacho Mbasha alikitamka kabla ya kukata roho…”

“Alitamka kitu gani?’

“Alitamka… freemaso wamempoteza”

Shanga alishituka tena aliposikia neon hilo.

“Tamshi hilo linamaanisha nini?”

“Hatujaelewa, tunaendelea na uchunguzi. Tutakupatia taarifa kamili baada ya uchunguzi wetu”

“Sawa. Asante sana”

Mara tu baada ya kuzungumza na mkurugenzi wake wa usalama, Shanga alimpigia simu waziri wake wa mambo ya ndani na kumuuliza kama freemaso walihusika na uasi uliotokea.

“Siwezi kujibu swali hilo, inabidi kwanza nimuulize Osaka” Waziri alimjibu.

“Muulize halafu unipe jibu”

Dakika chache baadaye Osaka akampigia simu Rais Shanga.

“Napenda kukujibu kuwa tunahusika moja kwa moja na uasi uliotokea. Kanali Mbasha ni mwanachama wetu” Osaka alimwambia Rais Shanga kwenye simu.

“Unaweza kunieleza sababu za kuhusika kwenu na uasi huu?”

“Sababu ni kwamba tulikuweka katika madaraka na baadaye ulitugeuka. Sasa tunaipa misukosuko serikali yako mpaka pale utakapotii kile ambacho sisi tunataka”

“Nyinyi hamkuniweka mimi kwenye madaraka, nimewekwa na wananchi. Unaelewa?”

“Sisi tunajua tumekuweka sisi. Na unaweza kuukataa ukweli huo kwa kuona umeshapata. Lakini tunataka ujue kuwa ili uweze kuongoza nchi ni lazima ukae vyema na sisi”

“Mimi kama rais wa nchi hii  sitakuwa tayari kuendeshwa na mtu yeyote yule wala taasisi yoyote ile. Nitaongoza nchi hii kwa mujibu wa ilani iliyomo kwenye chama changu na si vinginevyo”

“Mheshimiwa usisahau ahadi uliyoitoa kwetu….”

Ahadi gani! Kama mtajaribu kuwa na kauli za kuhatarisha amani na kufanya vitendo vya kuyumbisha utawala wangu, sitasita kuwachukulia hatua”

“Huwezi kututisha kwa sababu tuna ahadi na wewe”

Shanga akakata simu. Akionesha wazi kukasirika alimpigia simu waziri mkuu wake na kumuita ofisini kwake.

Baada ya nusu saa tu waziri mkuu aliingia ofisini kwa Rais Shanga.

“Nimefika mheshimiwa rais” Waziri mkuu alisema baada ya kuketi.

“Unajua kuwa hapa nchini kwetu kuna watu wanaojiita freemaso?” Rais Shanga akamuuliza

“Ninachojua ni kwamba wamesajiliwa kama taasisi ya kiraia”

“Futa usajili wao. Na upige marufuku shughuli zao zote hapa nchini kwetu. Hatuwahitaji tena!”

Waziri mkuu alikuwa kama aliyetaka kuuliza swali lakini alisita akasema.

“Sawa mheshimiwa, kuna jingine?”

“Hilo tu”

Waziri mkuu akatoka ofisini.

                                        *************

Wakati serikali ya Shanga inafuta usajili wa kundi hilo na kupiga marufuku shugjuli zao zote, Rais Shanga alimfukuza kazi waziri wake wa mambo ya ndani na kuteua waziri mwingine kushika nafasi yake.

Baada ya hatua hizo Osaka alimpigia simu Rais Shanga.

“Tunakwambia asante sana kwa hatua ulizochukua”

“Nimesikitishwa sana na hatua ya kundi lenu kutaka kuleta machafuko hapa nchini” Rais Shanga akamwambia Osaka na kuongeza.

“Serikali ndiyo imewasajili nyinyi lakini nyinyi hamkuiweka serikali. Sasa tumefuta usajili wenu”

“Pamoja na hatua ulizochukua nataka kukufahamisha kuwa kuwepo kwetu kunatambulika kimataifa na tupo dunia nzima”.

Osaka aliposema hivyo alikata simu.

Baada ya kupita wiki moja taarifa za kikachero ziliifikia ikulu zikidai kuwa kundi hilo lililopigwa marufuku lilikuwa likiendelea na shughuli zake kama kawaida

Taarifa hiyo ilimchukiza Rais Shanga akampigia simu waziri mkuu na kumuita ofisini kwake.

Dakika chache baadaye, waziri mkuu alipowasili ofisini kwake Shanga alimuulizia kuhusu agizo lake la kupiga marufuku shughuli za freemaso.

“Unakumbuka nilikuagiza nini?” Shanga alimuuliza.

“Nilitekeleza agizo lako mheshimiwa Nimehakikisha kuwa usajili wa kundi hilo umefutwa na niliwapelekea barua kuwajulisha kuwa usajili wao umefutwa na shughuli zao haziruhusiwi nchini mwetu.”