Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sitaki tena Urais – Sehemu ya 05

RAIS 05 Pict

UTANGULIZI

Walimwambia kwamba wanahitaji kuwa na rais wa nchi atakayetambua harakati zao.

Osaka akamwambia Shanga kuwa watu hao aliowakuta hapo ndio nguzo za freemaso ncini mwao na hukutana kila siku usiku na kujadili mambo mbalimbali ya kifreemaso.

“Wako wengine wengi tu, unaweza kukutana nao muda mwingine,” Osaka aliendelea kumwambia.

“Lakini kuna kitu kimoja, zingatia sana ushirikiano na wenzako. Sisi ni wajenzi huru. Ushirikiano wetu ndio utakaotuwezesha kuijenga dunia hii.”

SASA ENDELEA


Akaendelea kumueleza. “Si kwa matakwa ya urais, si kwa matakwa ya utajiri bali ni kwa matakwa ya kuwa na dunia huru, dunia ya amani na yenye utii….”

“Tunayo maktaba yetu katika jengo hili. Utakuwa unajisomea vitabu vyetu mbalimbali ili uweze kutambua maadili yetu na malengo yetu. Ujue wapi tunataka na wapi tunaelekea. Vilevile utakuwa unahudhuria kwenye mafundisho yetu siku za jumanne na jumamosi.

“Sisi kama freemaso hatukuanza leo, tuna historia. Kumbukumbu zinaonesha kuwa freemaso wamekuwepo kwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita. Mafanikio yetu makubwa ni kuwa tumekuwa na wanachama marais wa mataifa makubwa tangu muda huo. Hivi sasa tunataka kuwa na wanachama marais katika nchi za Afrika na wewe utakuwa mmojawapo.

“Najua kuna mengi unayotaka kuyajua lakini acha haraka. Endelea kuhudhuria katika mafundisho yetu, utajua mengi…”

Osaka alimaliza kumueleza Shanga. Wakarudisha glasi . Osaka akamtaka Shanga kuagana na wanachama wenzake kisha akaondoka naye.

Walikwenda katika chumba kimoja kilichokuwa na maktaba ya vitabu, magazeti na CD za freemaso. Kwenye kuta za chumba hicho kulibandikwa picha za wanachama mbalimbali maarufu wa freemason duniani.

Osaka alimuonesha Shanga vitabu mbalimbali vyenye habari za freemaso.

“Wakati ukipata nafasi unaweza kuja kujisomea na kuangalia CD mbalimbali” Osaka alimwambia Shanga.

Baada ya hapo walitoka katika chumba hicho. Wakati wanapanda ngazi Osaka alimwambia Shanga kuwa anatakiwa kuhudhuria kwenye mafunzo ya kila siku kwa muda wa siku saba.

“Yanakuwa saa ngapi?”

“Yanakuwa saa kumi hadi saa kumi na mbili jioni”

“Nakumbuka umeniambia mafundisho ni siku ya jumanne na jumamosi”

“Jumanne na jumamosi ni mafundisho kwa wote, yanaanza saa mbili usiku hadi saa nne. Wewe utakuwa na mafunzo ya peke yako kila siku kwa muda wa siku saba”

“Kuna tofauti kati ya mafunzo na mafundisho?”

“Utakapoanza kuja kwenye mafunzo yetu ya kila siku na kwenye mafundisho ya jumanne na jumamosi, utagundua kuwa ipo tofauti”

“Kwa hiyo ninatakiwa nifike hapa kila siku saa kumi kwa siku saba?”

“Ni muhimu sana. Huwezi kusema unaendesha gari wakati hujui kuendesha. Na huwezi kujua bila kupata mafunzo”

“Sawa nimekuelewa”

Walipomaliza kupanda ngazi walitoka nje ya jengo hilo, walisimama karibu na mlango. Osaka akamwambia Shanga.

“Nafikiri tumemaliza shughuli yetu ya leo. Sasa unaweza kwenda isipokuwa kumbuka kwamba kesho tutakuhitaji kuanzia saa kumi”

“Asante sana” Shanga alimshukuru Osaka.

Wakati wanapeana mikono ya kuagana Osaka alimwambia Shanga.

“Bosco anakusubiri kwenye gari akurudishe”

“Acha niende, tutakutana hapo kesho”

Wakati Shanga akiwa kando ya Bosco akirudishwa nyumbani, maswali mengi yalikuwa yanapita kichwani mwake. Alijiuliza ni kwanini fomu aliyojaza alitakiwa kueleza idadi ya watoto wake, ndugu zake na pia kuandika majina ya majirani zake na marafiki zake wa karibu.

Wao wanahusika na nini wakati aliyetaka uanachama ni yeye? Alijiuliza. Pia alijiuliza kama kweli ataupata urais kama alivyoahidiwa.

Alijiambia kama atashindwa kwenye uchaguzi huo atajitoa kwenye jumuia hiyo hata bila kutoa taarifa kwani alishawishiwa kujiunga ili apate urais.

Baada ya kimya cha dakika kadhaa Bosco alimuuliza Shanga.

“Ni kitu gani ambacho umeona hakikukupendeza?”

Kwa vile alikuwa katika mawazo Shanga aligutuka kidogo na kumtazama Shanga.

“Kitu ambacho hakikunipendeza?” Na yeye akamuuliza Shanga kama vile hakuwa amemsikia vizuri.

“Ndiyo”

“Kwa kweli sikuona kitu ambacho hakikunipendeza”

“Je kwa upande wa uanachama wako, umeona utaweza kuendelea kushirikiana na sisi?”

“Lengo langu kubwa ni kuwa rais. Kwa hiyo ni lazima tutashirikiana kwa lile litakalowezekana”

“Unaposema ‘kwa lile litakalowezekana una maana gani?”

“Nina maana kwamba nitatekeleza kila nitakachoambiwa ambacho nitaweza kukifanya”

“Bwana Shanga hakuna kisichowezekana kama kweli una nia thabiti ya kuwa mwanachama mwenzetu na kuwa rais wa nchi hii”

“Mpaka sasa sijaelezwa chochote kigumu ninachotakiwa nifanye, kwa hiyo siwezi kuzungumzia chochote”

Bosco akanyamaza na Shanga hakutaka tena kuendelea kumsemeha.

Ukimya huo ulimrudisha tena Shanga katika mawazo. Alijiambia kama Bosco angemuuliza ni kitu gani kimemshitua kwa siku ile angemjibu kuwa ni kuwaona wale watu wawili ambao walifika ofisini kwake mchana na kumuonya kuhusu freemaso.

Kitandawili cha watu hao ambao aliwakuta ndani ya kundi hilo ndicho kilichokuwa ndani ya akili yake hadi muda ule.

Kutokana na kuwakuta ndani ya jengo lile na kutokana na mavazi waliyokuwa wamevaa ilikuwa ni wazi kwamba walikuwa ni wenzao.

Akajiuliza ni kwanini walimfuata na kumuonya kuhusu freemaso wakati na wao wamo?

Gari lilipofunga breki mbele ya geti la nyumba yake ndio alipozinduka na kugundua kuwa alikuwa ameshafika nyumbani.

“Asante bwana Bosco, kwaheri” alimwambia Bosco huku akifungua mlango.

“Asante. Usiku mwema” Bosco akamjibu.

“Usiku mwema na kwako” Shanga alimwambia akiwa nje ya gari. Aliufunga mlango wa gari na gari hilo likaondoka kwa kasi.

Alipoingia ndani ya nyumba yake hakumueleza mke wake kuhusu kujiunga kwake na freemaso. Alijua kama atamueleza mke wake angeshituka na kumuonya. Pengine angekimbilia kanisani kudai talaka.

“Mmemaliza mkutano wenu?” mke wake alimuuliza mara tu alipketi sebuleni.

“Tumemaliza, wafadhili wamekubali kutusaidia kwa mashati” akamdanganya mke wake,

“Masharti yapi?”

“Tuwe na uhakika wa kushinda kwa asilimia 80 ili pesa zao zisipotee bure”

“Anayeshindana yeyote anatarajia kushinda”

“Tumewambia kwamba tuna uhakika wa kupata urais na wabunge wa kutosha”

“Watawapatia kiasi gani?”

“Kiasi kitajulikana baadaye lakini wao watagharamikia mahitaji yetu mbalimbali ya kampeni mpaka kampeni itakapokwisha.”

“Safi sana.”

“Kesho tutaanza kuwapa bajeti yetu ya wiki moja. Tutakuwa tunawapa bajeti ya kila wiki.”

“Jitahidi mume wangu tuingie ikulu”

“Hakuna shaka mke wangu, ikulu ni yetu”

Shanga alipotoka nyumbani kwake asubuhi alikwenda ofisini kwake. Shughuli kubwa iliyomkabili siku ile ilikuwa ni kupokea vifaa mbalimbali vya kampeni, fulana za chama chao zenye picha za wagombea wa chama hicho kuanzia mgombea urais, wabunge na madiwani. Fulana hizo zilitengezwa nchini humo humo.

Pia walipokea picha za kampeni za kupachika kwenye mitaa. Picha hizo zilikuwa za mgombea urais na ubunge wa chama hicho. Zilikuwepo bendera, vipeperushi na vitu vingine mbalimbali ambavyo viligharamiwa na mfanyabiashara  Jacob Niwako.

Wakati wa mchana Shanga alirudi nyumbani kwake kula chakula. Alitoka tena saa tisa na nusu na kuelekea Useriver kwa gari lake.

Alipolisimamisha gari mbele ya jumba la freemaso, askari alimfungulia geti akaliingiza gari hilo bila kuulizwa chochote. Aliliegesha kwenye banda la magari. Wakati analizima moto alimuona Osaka akitokea kwenye mlango wa jumba hilo na kumsubiri.

Alifungua mlango akashuka na kutembea kuelekea kunako mlango wa jumba hilo.

“Karibu sana Bwana Shanga, una uhakika wa ahadi!” Osaka alimwambia Shanga huku akimtolea mkono wasalimiane.

“Habari yako  Bwana?” akamsalimia wakati wakipeana mikono.

“Nzuri Bwana Osaka, za hapa”

“Hapa ni kwema tu, karibu ndani”

Waliingia ndani. Safari hii hawakupanda wala kushuka ngazi. Walikwenda moja kwa moja hadi mwisho wa ukumbi ambako kulikuwa na milango kadhaa. Osaka alifungua mlango wa chumba kimoja akaingia. Shanga alimfuata.

Waliingia katika chumba kilichokuwa kama darasa. Upande mmoja kulikuwa na viti na meza zipatazo saba. Upande mwingine kulikuwa na ubao mweusi uliopachikwa kwenye ukuta. Mbele ya ubao huo kulikuwa na meza kama ya mwalimu ambapo kulikuwa na mtu akiandika.

“Karibuni” Mtu huyo alisema alipowaona Osaka na Shanga wakiingia.

“Huyu ni mkufunzi wetu anaitwa Charly” Osaka alimwambia Shanga wakiwa mbele ya meza.

“Na  Bwana Charly huyu ni Bwana Shanga, mwanachama wetu mpya tuliyekuwa tunamsubiri kwa ajili ya mafunzo” Osaka aliendelea kumtambulisha Shanga.

Baada ya utambulisho huo Shanga na Charly kila mmoja alisema amefurahi kumtambua mwenzake, wakapeana mikono na kuulizana hali.