Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya kutisha - Sehemu ya 31

MAUAJI 30 Pict

UTANGULIZI

Baada ya nusu saa tu, magari mawili ya polisi yakawasili nyumbani kwa Almasi. Vile polisi walivyoambiwa kwamba wauaji hao walikuwa wamefungiwa kwenye chumba, walikuja polisi tisa. Watano wakiwa na bunduki. Inspekta Amour, ambaye huvaa kiraia, alikuwa wa kumi.

Almasi aliwakaribisha.

“Hao watu wamo ndani?” Amour akamuuliza akiwa ameshika bastola mkononi.

“Niliwafungia chumbani mwangu na sijafungua mlango hadi sasa.”

SASA ENDELEA


HEBU fungua tuingie ndani. Mazungumzo ni baadaye”

Almasi akafungua mlango.

Polisi hao wakaingia ndani pamoja na  Almasi. Alifngua mlango wa ndani. Akawapeleka kwenye mlango wa chumba chake.

“Mauaji yamefanyika ndani ya chumba hiki. Mke wangu yumo  humu ndani na hao watu niliwafungia humu  humu”

“Sasa fungua huo  malango” Amour akamwambia.

Almasi akatoa fungua na kufungua mlango.

Amour alipojaribu kuusukuma mlango, aligundua kuwa mlango huo  ulifungwa kwa nadani.

“Mlango umefungwa kwa ndani” akasema.

“Basi bado wamo” Almasi akamwambia.

Amour akaanza kugonga mlango. Aliugonga kwa sekunde kadhaa akiwataka watu waliomo ndani ya chumba hicho wafungue mlango na kujisalimisha kwa polisi. Lakini hakukuwa na jibu lolote lililotoka.

“Kama hawakutii amri ya polisi, sasa nalazimikakuvunja mlango” Amour akamwambia Almasi.

“Vunja”

Amour alimwambia polisi  mmojawapo aliyekuwa na bunduki apige risasi zile sehemu za bawaba ili kuung’oa mlango huo. Risasi tatu za SMG zikauondoa mlango huo mahali pake.

Mlango ulipokuwa umevunjwa, Amour alipiga risasi mbili za bastola humo chumbani akilenga chini ya ardhi kabla ya kuruka ndani ya chumba hicho akiwa na bastola yake mkononi. Alipotua chini akiwa katikati ya chumba hicho aliishikilia bastola yake sawasawa na kuielekeza pande zote za chumba hicho kwa haraka  haraka.

Kitendo cha kufyatua  risasi mbili na kisha  kurukia ndani ya chumba hicho kilikuwa ni cha kuwafanya watu waliokuwemo ndani ya chumba hicho,  kama walikuwemo kweli, wagwae na aliruka ili kuwashitukizia.

Lakini alipotupa macho  pande zote za chumba hicho hakuona watu wowote zaidi ya mwili  wa mke wa Almasi uliokuwa umelala chini pembeni mwa kitanda.

“Hebu lete tochi” alisema huku akiinama mvunguni mwa kitanda.

Polisi ambao walikuwa hawajaingia, waliingia na mmojawapo alimpa  tochi Amour.

Amour aliipokea tochi  na kumulika  chini ya mvungu.

“Hakuna kitu” alisema.

Akainuka na kumtazama Almasi.

“Mbona hatuwaoni hao watu?”

“Walikuwemo humu ndani nikawafungia” Almasi alisema huku akitupa  macho yake huku na huku.

“Kama wametoka, wametoka kwa wapi wakati  mlango uliufunga kwa nje?”

Almasi alitikisa kichwa kuonesha mshangao.

“Hapo ndio sielewi”

“Watakuwa ni watu wa miujiza”

“Tangu mwanzo wameonekana kuwa watu wa miujiza”

“Hatuoni sababu ni kwanini wamekuandama wewe peke yako!”

“Na mimi najiuliza swali hilo kila siku”

“Ni lazima jibu lipatikane. Hatuwezi kushuhudia hali hii ikijitokeza mara kwa mara”

“Nimeshajitolea sadaka. Kama kuna aliyebaki kufa ni mimi mwenyewe. Sihitaji tena kuwasumbua polisi. Nimewaita tu kwa sababu ndio utaratibu wa kisheria kuwafahamisha polisi linapotokea tukio kama hili la mauaji”

“Sisi hutusumbui, tunatekeleza jukumu letu. Na vile vile hupaswi kusema kuwa umejitolea sadaka. Ni lazima polisi tutimize wajibu wetu wa kukulinda wewe”

Almasi hakusema kitu tena kwa vile alishajua sababu ya kuuawa kwa wanawe na mke wake.

Polisi wakaanza kushughulika. Hatimaye mwili wa mke wa  Allmasi ulitolewa ukapakiwa kwennye gari na kupelekwa hospitali. Almasi alitakiwa afike kituo cha polisi kuandikisha maelezo yake.

Wakati Almasi anatoka, mdogo wa mke wake pamoja na kaka  zake wawili wakafika.

Walikutana kwenye geti.

“Shemeji unakwenda wapi?” mmoja wa kaka wa mke wake aliyeitwa Samson akamuuliza baada ya kushuka kwenye gari.

“Nakwenda kituo cha polisi”

“Tumepata taarifa sasa hivi kutoka kwa mdogo wetu Maria kuwa mke wako ameuawa, ni kweli?”

“Ni kweli, ndio  ninakwenda kituo cha polisi kuandikisha maelezo”

“Mwili wake umo ndani?”

“Umechukuliwa na polisi sasa hivi”

“Unaweza kutueleza sababu ya kuuawa  kwa dada yetu na  kututajia watu waliomuua?”

“Mbona mnauliza kama vile kuna ugomvi. Hili suala liko mikononi mwa polisi…”

“Kuna maneno ambayo umemueleza Maria, yametupa taharuki”

“Maneno gani?”

“Yale ambayo ulimueleza kwenye gari na baadaye ukamfukuza kwenye gari lako na kumuacha atembee kwa  miguu  usiku huu”

Almasi akajifanya anatikisa kichwa kusikitika.

“Jamani mmekuja kwenye msiba au mmekuja kwenye kesi?”

“Tumekuja kwa vyote kwa sababu si uungwana kumfukuza shemeji yako kwenye gari usiku huu baada ya kukueleza kuwa umemuua dada yake!”

“Sasa ni kwanini yeye aniambie kuwa nimemuua mke wangu?”

“Kutokana na maelezouliyomueleza wewe mwenyewe kwamba ulimtoa kafara yeye na watoto wako”

Almasi akatikisa kichwakukataa.

“Sijamwambia kuwa nimemtoa kafara mke wangu na watoto  wangu. Mimi si kichaa. Inaonekana huyu mdogo wenu si muelewa”

“Sasa tueleze wewe ni nani aliyemuua mke wako na kwanini alimuua?”

“Mimi sijui ni kwanini aliuawa ila najua kuwa aliuawa huu usiku. Hii kesi iko mikononi mwa polisi. Labda watakapomaliza uchunguzi wao watatueleza”

“Wewe si umenieleza kuwa umeambiwa  na mganga kwamba uliweka masharti kwa maganga wako ambayo hukuyatimiza na hivyo kusababisha watoto wako na mke wako wauawe na wewe ulikubali?” Maria akamwambia Almasi.

“Sasa  mimi siwezi kushika maelezo ya mganga. Huko kwa mganga ulinipeleka wewe na wala siamiiini kile nilichoambiwa. Cha msingi hapa  ni kuendelea na msiba. Baada ya kumzika marehemu tutaweka kikao tuongelee mambo mengine lakini simu muda huu. Mimi nahitajika polisi”

“Kaka tumsusie huyu marehemu, azike mwenyewe. Huyu shemeji ni mshirikina sana. Huyu ndiye amemuua dada. Ameniambia yeye mwenyewe. Hivi sasa amewaona nyinyi anabadilisha maneno”

“Sasa unasikia shemeji, sisi tumeamua kukuachia huyu marehemu kwa sababu hutaki kutupa maelezo ya kuridhisha ni kwanini ameuawa na nani amemuua. Tunaamini kama anavyotueleza Maria umemuua wewe!”

“Sasa hiyo ni akili gani? Mnashika maneno yaMaria! Mnasusia maiti ya dada yenu kwa kushika maneno ya Maria? Nimeshawambia uchunguzi unafanywa na polisi. Kama mnataka maelzo zaidi, nendeni mkawaone polisi watawaeleza”

Almasi alipowambia hivyo shemeji zake hao waliingia kwenye gari walilokwenda nalo na kuondoka bila kuaga.

“Potelea mbali. Kama ni kumzika maremehu nitamzika mwenywe. Nendeni” Almasi akajisemea peke yake. Na yeye akaingia kwenye gari lake na kuondoka.

Alipofika kituo cha polisi akalikuta gari la shemeji zake likiwa nje ya kituo.

Alipoingia ndani ya kituo hicho akakutana na watu hao wakizungumza  na Inspekta Amour.

Walipomuona akiingia walikatisha mazungumzo. Amour akamwambia Almasi.

“Nimepokea mashitaka yako”

“Mashitaka gani?”

“Kwamba watoto wako pamoja na  mke wako wameuawa kwa sababu za kishirikina”

“Sasa ushirikina upi nilioufanya?’

“Ni ushirikina ambao uliufanya kwenye madini miaka iliyopita. Shemeji zako wanadai kuwa hukutimiza mashrti ya waganga na hivyo kusababisha watoto wako pamoja na mke wakokuuawa na majini”

Almasi akatikisa kichwa.

“Si kweli. Mimi nawaomba polisi muendelee na upelelezi wenu. Habari hizi za kishirikina muachane nazo”

“Ni kweli kwamba hatuchunguzi kadhia zenye mtazamo huo na wala madai hayo hayawezikutufanya tukufungulie kesi lakini mazingira ya yale mauaji yanatisha. Kwa mfano wale watu waliomuua mke wako uliwafungia ndani lakini tulipovunja mlango hawakuwemo ndani!”

Maria alliposikia  hivyo akachachamaa.

“Sasa ulikataa nini wakati hata polisi wammeona jinsi hao watu walivyotoweka. Bado utasema si ushirikina wako uliomuuua dada yangu?’

Kaka zake nao wakaingilia.

Ikawa mzozo ndani ya kituo cha polisi, ikabidi Inspekta Amour aingilie kati kuwasuluhisha nakuwaweka sawa mpaka wakakubalina kwamba washirkiane kumzika marehemu na baada ya hapo waweke kikao kuzungumzia tatizo lililotokea lakini wazingatie ripoti ya uchunguzi itakayotolewa na polisi.

Baada ya muafaka huo, shemeji zake Almasi waliondoka na kumuacha Almasi akiandikisha maelezo yake. Baada ya hapo akaondoka.  Aliporudi nyumbani kwake aliwapigia simu jamaa zake na rafiki zake na kuwajjulisha kuhusu msiba wa mke wake.

Lengo lake lilikuwa  kupata  watu wa kulala naye pale nyumbani. Alikuwa ameingia uoga wa kulala pake yake. Alihisi kama vile  wauaji hao watamfuata usiku na kummaliza na yeye kama alivyoambiwa na mganga kwamba ilibaki roho yake kutoka. Saa chache baadaye, jamaa na marafiki aliowapigia simu wakaanza kufika nyumbani kwake na kumfariji.

Alipata watu ambao alilala nao hadi asubuhi lakini shemeji zake hawakufika.