Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya kutisha - Sehemu ya 23

AKAD 01

UTANGULIZI

“Mimi sikuwaona”

“Itakuwa ni miujiza kwamba watu watatu wameingia hunu na kuua mtu bila kuonekana!”

“Lakini Inspekta kitu gani kinakushangaza?’ Almasi akamuuliza Amour.

“Ninashangaa kuona kwamba mnaye mlinzi anayelinda kwenye geti lenu na humu ndani kuna wafanyakazi lakini watu wasiotakiwa wameweza kuingia na kufanya mauaji!”

SASA ENDELEA


“Kwani hii ni mara ya kwanza kwa watoto wangu kuuawa? Hii si mara ya kwanza. Huu ni mfululizo  wa mauaji ya kimiujiza ya muda mrefu. Mwanangu John aliingiliwa nyumbani kwake na kulikuwa na mlinzi!”

“Sikiliza mzee Almasi sisi tunatathmini kila tukio linalotokea na kujiuliza lilifanyika katika mazingira yapi. Hatupendi kulinganisha matukio. Kama  tunayalinganisha ni kwa sababu za kiuchunguzi tu”

“Nimekuelewa Inspekta endelea na maswali yako”

Inspekta alinyamza kwanza kutuliza taharuki. Alijua kuwa Almas alikuwa hayuko sawa na hivyo hakutaka kumchukulia.

Alikumbuka kwamba aliwahi kuambiwa na Almasi kwamba mwanawe Benjamin aliajiri mlinzi ambaye atakuwa yuko naye wakati wote.

“Nakumbuka kwamba uliwahi kuniambia kwamba uliajiri mlinzi  kwa ajili ya usalama wa mwanao?”

“Ndiyo. Lakini pia hakusaidia kitu”

“Wakati tukio hili linatokea alikuwa wapi?”

“Labda umuulize mwenyewe, yuko hapa”

“Yuko  wapi?”

Mlinzi huyo aliyekuwa yupo hapo karibu akajitokeza.

“Ni mimi”

Inspekta Amour alimntazama kijana huyo kwa makini kabla ya kumuuliza.

“Wewe ndiye uliyekuwa mlinzi  wa Benjamin?”

“Ndiye mimi”

“Ulikuwa ukifahamu majukumu yako ni nini?”

“Nilikuwa nafahamu”

“Niambie majukumu yako yalikuwa  ni nini?”

“Kumlinda Benjamin”

“Ulikuwa unamlinda Benjamin?”

“Ndiyo”

“Ulikuwa unamlinda dhidi ya kina  nani?”

“Nilikuwa namlinda dhidi ya mtu yeyote ambaye atakuwa na nia ya kumdhuru Benjamin”

“Ulikuwa unaifanya kazi hiyo kwa weledi?”

“Ndiyo

“Na marehemu alikuamini kuwa unamlinda?”

“Natumaini aliniamini”

“Sasa leo Benjamin ameuawa, utatueleza  nini?”

“Aliuawa kwa bahati  mbaya”

“Unataka uniambie kuna mauaji ya bahati nzuri?”

“Hakuna. Lakini Benjamin aliuawa kwa bahati mbaya”

“Ni kwa sababu hukutimiza jukumu lako la kumlinda”

“Benjamin alipouawa sikuwa naye karibu. Aliniambia anakwenda msalani. Nikamuacha aende msalani. Waliomuua walimuua akiwa msalani kama mwili wake ulivyokutwa”

“Hukuona kuwa kumuacha peke yake ulikuwa unawapa  mwanya wauaji?”

“Hilo sikulitegemea kwa sababu tangu nianze kazi hii sijawahi kumfuata msalani hata siku moja. Hakuna aliyetarajia  kuwa wauaji wangemfuata msalani”

“Na wewe wakati wote ukiwa na Benjamin hukuwahi kunusanusa na kugundua kuwa wauaji walikuwa wanamfuatilia?’

“Sikuwa na taarifa kama hizo, nisingemuacha aende msalani peke yake”

“Maana ya kukuajiri wewe ni kuwa alijiona alikuwa katika  hatari. Wewe kama mlinzi wake ulipaswa kuwa na mwajiri wako wakati wote na mahali popote?”

“Hata msalani pia?”

“Wewe si umesema kama ungejua usingemuacha aende msalani peke yake? Sasa unashangaa nini?”

Kijana  huyo akanyamza kimya.

“Unaonaje kama tutakukamata wewe kwa kusababisha  Benjamin auawe?”

“Mimi sikusababisha  Benjamin auawe”

“Wewe ndiye uliyechukua  jukumu la kumlinda na umeshindwa kutimiza jukumu lako. Ameuawa hapakazini kwenu na wewe ukiwepo?”

Amour alipomuona kijana huyo amenyamaza kimya, aliwageukia polisi aliokuwa amefuatana nao na kuwambia.

“Mchukueni huyu kijana na mlinzi wa geti pamoja na yule mfanyakazi aliyeshuhudia Benjamin akiuawa ili waisaidie polisi katika uchunguzi”

Vijana hao walikamatwa na kuingizwa kwenye gari lapolisi.

Wakati wote amour alipokuwa akimhoji mlinzi wa marehemu Benjamin hadi kuwaamuru polisi wamchukue yeye, mlinzi wa geti pamoja na mfanyakazi wao aliyeshuhudia wakati Benjaminakiuawa, Almasi alikuwa akimtazama kwa jicho la dharau. Alikuwa akijiuliza ni kwanini kachero huyo afikirie kuwachukua vijana hao badala ya kuwajibika polisi wenyewe.

“Inspekta nakukumbusha kwamba matukio ya mauaji hayakuanza leo. Yalinza tangu hao vijana mliowachukua siwajui” Almasi akamwambia Amour.

“Kwanini unaniambia  hivyo?” Amour akamuuliza.

“Nakukumbusha tu Inspekta”

Amour alitulia kidogo akayatafakari yale maneno kisha akamwambia Almasi.

“Sawa. Nimekuelewa. Nitakuhitaji ofisini kwangu utakapopata nafasi kuja”

“Nitafika”

“Sisi tunaondoka”

“Sawa Inspekta”

Wakati Amour akiendesha gari kuelekea kituo kikuu cha polisi, alijiuliza ni kwanini Almasi alimwambia akumbuke kuwa mauaji ya wanawe hayakuanza leo?

Ana maana kwamba hatuamini? Au ana maana kwamba vijana waliowachukua walikuwa wanawaonea?

Amour akatikisa  kicwa peke yake kusikitika alipowaza kwamba Almasi alikuwa amekiuka mipaka ya shutuma.

Lakini tutamfanya nini wakati kuna ukweli kwamba  ana uchungu wa kuuliwa watoto wake kwa mfululizo? Akajiambia. Anaweza kusema  lolote analojisikia kulisema aukuwaza lolote linaloingiakichwani mwake. Lakini hatowaza hata siku moja kwamba huenda matatizo haya  yanatokana na yeye mwenyewe. Amour aliwaza.

“Kuna umuhimu sasa wa kuanza kumchunguza huyu mzee” akajiambia.

Walipofika kituo kikuu cha polisi,vijana waliokamatwa wakatakiwa watoemaelezo yao.

Alianza mfanyakazi aliyeshuhudia Benjamin akiuawa.

Baada ya kuandikisha maelezo yake, Amour alimwambia.

“Hebu rudia yale maneno. Yule mtu aliyemchinja Benjamin alimuuliza nini?”

Alimuuliza Benjamin kama ni mtoto wa Almasi?”

“Benjamin akamjibu nini?”

“Alimjibu ‘Ndiyo”

“Halafu huyo mtu alimwambia nini tena?”

“Alimwambia baba yako alikuweka kama dhamana na wewe umeshindwa kutimiza masharti ya dhamana yako. Benjamin akamuuliza aliniweka dhamana wapi? Yule mtu akamwambia asingeweza kumueleza kitu  kwa sababu muda wa Benjamin ulikuwa  umeisha”

“Ndipo alipotoa  sime na kumchinja?”

“Ndiyo”

Amour akamgeukia  kachero mwenzake ambaye walikuwa wakiandikisha yale maelezo pamoja.

“Unaona, chanzo kinaweza kuwa ni kwa baba mtu. Huyu mtu alimuuliza wewe ni mtoto wa Almasi. Akamwambia baba yako alikuweka dhamana na wewe umeshindwa  kutimiza masharti ya dhamana. Si unaona chanzo kipo kwa baba mtu?” Amour alimwambia kachero mwenzake.

“Inawezekana kabisa kwamba tatizo limetokana na baba mtu”

“Huyu mzee anahitaji kuhojiwa na kuchunguzwa. Hapa kuna kitu, si bure. Haiwezekani watoto  wake wauawe bure kila siku”

“Kule Pakistan kuna mchezo mmoja. Unaweza kumuweka mtu dhamna ukapewa kokeni ukauze lakiniukishindwa kutimiza masharti ya dhamna, mtu wako anauawa!?”

“Umetoa mfano sahihi sana. Unahisi kuna kitu kama hicho?”

“Kinawezekana. Kwani yule mzee utajiri wake aliupata wapi?”

“Ndiyo maana nikasema ni lazima tumhoji na  kumchunguza, isije kuwa yeye ndiye anayewasababishia vifo watoto wake”

“Hebu tuwe wazi. Unashuku kwamba anajishughulisha  na biashara ya madawa ya kulevya?”

“Majibu tutayapata baada ya uchunguzi wetu”

“Sawa. Naona hivi sasa tuingie kazini kumchunguza yeye”

“Nimemwambia aje ofiisini kwangu. Nitakualikaili tumhoji maswali”

“Sawa afande. Akifika utanijulisha”

Kijana aliyekuwa akitoa maelezo akaambiwa na Inspekta Amour kwamba atawekwa ndani.

Kijana huyo akashituka.

“Niwekwe ndani kwa kosa gani?’ akauliza kwa taharuki.

“Ni kwa sababu kwa taratibu zetu wewe pia ni mtuhumiwa!”

“Kwanini?’

“Kwa sababu wakati Benjamin anauawa ni nyinyi wawili mliokuwa msalani. Unadhani tutamkamata  nani?’

“Lakini nimeshaeleza kwamba  mimi sikuhusika”

“Sasa acha tuendelee na uchunguzi wetu. Tukijiridhisha kuwa hukuhusika tutakuachia”

Licha ya mfanyakazi huyo kuanza kulalamika, Amour alimuamuru polisi aliyekuwepo hapo amchukue na kwenda kumuweka ndani.

Mtu wa pili aliyeitwa kutoa maelezo alikuwa mlinzi wa geti la kiwanda.

Baada ya kutoa maelzo yake na kukana kuwaona watu waliomuua Benjamin wakiingia katika kiwanda hicho, Amour alimwambia na yeye atawekwa ndani.

“Kwanini niwekwe ndani?” Mtu huyo akang’aka.

“Tutajuaje kama wewe ulikula njama na hao wauaji?” Polisi mmoja akamwambia mlinzi huyo.

“Mimi nile njama na wauaji?” Mlinzi huyo akang’aka tena.

“Kama wewe ulikuwa mlinzi wa Benjamin, sasa kwanini Benjamin ameuawa?”

“Ameuawa katika mazingira yanayofahamika lakini si kweli kwamba mimi nilikula njama  na wauaji”

“Jukumu lilikuwa mikononi mwako. Itabidi utupe maelezo ya kina ni kwanini Benjamin ameuawa”

“Niwape maelezo gani tena?”

“Huna budi kuisaidia polisi. Utakuwa mikononi mwetu hadi uchunguzi wetu utakapokamilika”

“Lakini hii si haki jamani!”

“Haki ni ipi?”

Inspekta Amour akaingilia kati.