Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya kutisha - Sehemu ya 21

Picha kwa msaada wa AI

Muktasari:

  • “Sasa nakuhadharisha wewe. Acha matembezi ya usiku na acha kujihusisha na makundi ya marafiki wasioeleweka. Umenielewa mwanangu?”

UTANGULIZI

“Tumeambiwa na daktari kwamba damu ya Alex ilionesha kwamba alikuwa amelewa wakati anauawa. Pengine kama asingelewa angeweza kujihami au pengine kama usiku ule asingekwenda klabu asingekutana na mauti yale.

“Sasa nakuhadharisha wewe. Acha matembezi ya usiku na acha kujihusisha na makundi ya marafiki wasioeleweka. Umenielewa mwanangu?”

“Nimekuelewa mama.  Nyinyi wenyewe mnanijua tangu zamani. Sina marafiki kama alivyokuwa Alex na muda mwingi nakuwa nyumbani tu.” Benjamin aliwaambia.

SASA ENDELEA


“Endelea kuwa hivyo na usiache kwenda kanisani.”

“Sawa mama.”

“Na wewe mke wangu kuwa na moyo wa subira, uone haya yanayotutokea ni mitihani ya Mungu. Tukazane kuomba na kufunga ili uadui huu utuepuke mbali sana. Umenisikia mke wangu?” Almasi akamwambia mke wake.

“Kuomba na kufunga ni tabia yangu tangu zamani. Ninaamini iko siku Mwenyezi Mungu atasikia kilio chetu na huyu adui atakuja  kuangamia. Mimi naona mwisho wake uko karibu sana.”

Mke wa Almasi aliposema hivvyo alimtazama Benjamin.

“Mwanangu ondoa wasiwasi. Tutakuombea sana, na Mungu atakuwa pamojanawe”

“Asante mama kwa kunipa  moyo. Mungu atakuwa pamooja na sisii sote, mimi, wewe mama pamoja na baba”

“Ameen…” Mke wa Almasi alisema kisha Almasi mwenyewe akamalizia.

“Ameen”

**********

Miezi miwili ilikuwa iimepita tangu alipouawa mtoto wa tatu wa Almasi. Benjamin ndiye aliyekuwa akimsaidia baba yake kazi ya uongozi katika kiwanda chao cha maji safi. Baada ya kuuawa kwa Alex, Almasi hakutaka  kuajiri mtu mwingine akaamua kushika yeye nafasi  ya Alex.

Wakati akienda kazini alikuwa akifuatana na mwanawe Benjamin ambaye naye alimpa ofisi ili amsaidie kazi zake.

Alex alikuwa na mlinzi wake ambaye wakati wote alikuwa akifuatana naye. Mlinzi huyo aliyeitwa Pius alikodiwa na Benjamin mwenyewe kutoka katika kampuni moja ya ulinzi.  Alikuwa kijana shupavu na mpiganaji wa karate mwenye mkanda mweusi.

Wakati Alex akiwa ofisini, yeye huwepo nje ya ofisi hadi Alex atakapoondoka. Ulinzi huo ulimpa Alex matumaini ya usalama wake kwani aliamini chochote kitakachomtokea, Pius angekuwa tayari kujitoa mhanga kumuokoa.

Asubuhi moja Alex alikuwa ofisini mwake akimuacha Pius nje ya ofisi. Akajisikia kushikwa na haja ndogo, akainuka ili aende maliwatoni. Alifungua mlango wa ofisi akamwambia mlinzi wake kuwa anakwenda  kujisaidia haja ndogo.

Benjamin alipoingia maliwatoni hakujua  kama kulikuwa na watu watatu wakimsubiri. Chumba chenyewe cha kujisaidia kilikuwa ni kile cha kujisaidia wanaume haja ndogo kwa kusimama. Kilikuwa na urefu wa kukaa vizimba saba vya kusimama.

Alex alikwenda hadi kizmba cha tatu akasimama na kufungua zipu. Ndipo alipowaona watu hao. Wa kwanza alitokea kizimba cha  nne, wa pili alitokea kizimba cha tano na wa tatu alitokea  kizimba cha sita.

Benjamin alipowaona alishituka. Haja ndogo aliyokuwa akiisikia ikampotea. Akabaki ameduwaa akiwatazama watu hao ambao hawakuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Mtu wa kwanza alikuwa amevaa mavazi meupe, wa pili alivaa mavazi meusi na wa tatu alivaa mavazi meupe.  Aliyevaa mavazi meusi alikuwa katikati. Kilichomshitua zaidi Benjamin ni kuwa yule mtu aliyevaa mavazi meusi shingo yake ilikuwa imechinjwa na kichwa chake kilikuwa kinaning’inia!

Benjamin akayakumbuka mauaji ya kaka zake! Watu waliowaua kaka zake walielezwa kuwa na mavazi kama hayo na mmojawao akiwa na kichwa kama hicho.

Kulikuwa na mfannya kazi mmoja naye alikuwa akienda kujisaidia. Alipoingia tu kwenye mlango alishituka na kusita alipomuona mtu aliyekuwa amevaa mavazi meusi akimuuliza  Benjamin

“Wewe ni mtoto wa Almasi?”

“Ndiyo mimi” Benjamin alimjibu kwa  kubabaika.

“Baba yako alikuweka kama dhamana  lakini wewe umeshindwa kutimiza  masharti ya dhamna” sauti ya yule mtu ikaendelea kusikika.

“Dhamana gani?” Benjamin akamuuliza.

“Unadhani utakuwa na muda wa kupata maelezo wakati muda wako wa kuishi umeshamalizika?”

Benjamin alifungua  mdomo ili apige kelele lakini  hakuwahi, sime ikapita kwenye koo  lake kama umeme.

Mtu aliyekuwa akiwachungulia alitoka mbio huku akipiga kelele.

“Jamani kuna watu wamemkata panga Benjamin…!”

Mtu huyo aliendelea kupiga kelele huku akikimbilia kwenye ofisi ya Almasi. Mlinzi wa Benjamin aliposikia kelele hizo aliungana na  wafanyakazi wengine kukimbilia maliwatoni ili kuwaona hao watu.

Walipoingia maliwatoni walikuta  michirizi ya damu iliyosambaa pande zote huku mwili wa Benjamin uliokuwa  umechinjwa ukiwa umelala chini. Pius alishituka  na kutaharuki.  Wafanyakazi wote wakashituka na kutaharuki.

Huko ofisini kwa Almasi, mfanyakazi aliyeingia ofisini humo alimshitua Almasi alipomwambia.

“Mzee kuna watu nimewaona kule  chooni wakimsulubu Benjamin!”

“Watu gani?”

“Watu watatu, wawili wamevaa mavazi meupe, mmoja amevaa mavazi meusina huyo alikuwa ameshika upanga…!”

“Mlinzi wake yuko wapi?” Almasi akamuuliza.

“Sijui”

“Ndio hizo kelele ninazozisikia…?”

“Watu wanakwenda kuwaangalia”

Almasi alikuwa ameshainuka kwenye kiti, akaenda kwenye mlango na kuufunngua. Alitoka mbio hadi maliwatoni.

Choo kilikuwa kimejaa wafanyakazi waliokuwa  wakiminyana ili wamuone Benjamin aliyekuwa ameshachinjwa.

Almasi baada ya kupishwa aliuona mwili wa mwanawe. Macho ya Benjamin yalikuwa wazi yaliyokuwa yakitazama bila  kuona chochote! Hao watu watatu hawakuwepo tena!

“Haah…Benjamin na wewe umeuawa!” Almasi alimaka baada ya kuuona mwili wa Benjamin uliolala  chini. Alikishika kichwa chake kwa mikono miwili, akajisemea.

“Sasa nashukuru Mungu”

Yulemfanyakazi aliyeliona tukio hilo alikuwa akiendelea kuwaeleza wafanyakazi wenzake alichokiona.

“Nilipokuwa naingia niliona watu watatu. Wawili walivaa mavazi meupe, mmoja alivaa mavazi meusi. Yule aliyevaa mavazi meusi alimuuliza Benjamin. “Wewe ni mtoto wa Almasi?”

Benjamin akajibu. “Ndiyo mimi”

“Yule mtu akamwambia. “Baba yako alikuweka kama dhamana na wewe umeshindwa kutimiza masharti ya dhamana yako. Benjamini akamuuliza. “Masharti gani?”

Yule mtu akamwambia. “Unadhani utakuwa  na muda wa kupata maelezo wakati  muda wako wa kuishi umeshamalizika. Palepale akamkata panga la shingo. Miimi nikatoka mbio kwenda kuwajulisha  watu…”

“Pale ulipowaona  hao watu ungekuja kusema  haraka, pengine tungewawahi lakini ulingoja mpaka alipomkata  mwanangu…” Almasi akamwambia yule mtu  kwa  uchungu.

“Sikujua kama walikuwa na dhamiri ya kumkata. Nilijua walikuwa wakimuulizamaswali tu. Na ndiyo nilisubiri kuwasikiliza” Mfanyakazi huyo akajitetetea.

“Wale ni wauaji. Ndio wamekuwa wakiwafuata  watoto wangu  na kuwaua…huyu ni wa mwisho…”

“Sasa  kama walikuwemo humu, swali la kujiuliza waliingiaje na walitokaje bila kuonekana  wakati tukio limetokea muda huu  huu?” Mlinzi wa Benjamin akauliza.

“Hilo ni swali ambalo litajibiwa na mlinzi wetu aliyeko kwenye geti. Yuko hapa?” Mfanyakazi mwingine akauliza.

“Nipo”  mlinzi huyo akajibu

“Uliwaona hao watu walipoingia?” Aliyeuliza alikuwamlinzi wa Benjamin.

“Sikuona watu hao”

“Je walipotoka?”

“Pia sikuwaona”

“Waliingiaje humu ndani bilakupitia kwenye geti?”

Hakukuwa na aliyejibu.

“Tujaribu kuwatafuta.Labda wamejificha mahali”

Wafanyakazi hao wakaanza kupekua katika vile vyoo vingine. Wakatoka nje ya choo hicho na kuwatafuta watu hao  katika  majengo yaliyokuwa karibu na choo kwa imani kuwa watakuwa wamejificha humo lakini hawakuwaona.

Almasi aliachwa chooni akiwa peke yake. Mtu wa kwanza aliyempigia simu alikuwa mke wake.

“Mke wangu, Benjamin naye amerudi kwa Mungu!” akamwambia mwanamke huyo  kwenye simu.

“Unasemaje mume wangu?” Sauti ya mwanamke huyo ikauliza kwa taharuki.

“Jikaze sana. Nakwambia kwamba Benjamin hatuko naye”

“Amefanya nini?”

“Ameuawa”

“Unanieleza nini mume wangu?”

“Sijui nitumie lugha gani kukueleza mke wangu….”

Almasi alianza kulia. Mke wake alisikia sauti nzito ya mume wake iliyojaa machungu ikiunguruma kwenye simu. Simu ikakatika.

Mke wake akampigia mlinzi wa Benjamin.

“Mko wapi?” akamuuliza kwa ukali.

“Tuko  kazini mama…”

“Nini kimetokea huko?”

“Kwani mzee hajakufahamisha bado?”

“Amenipigia simu lakini naona analia tu. Nini kimetokea?”

“Kuna matatizo. Benjamin alikuwa amekwenda msalani kujisaidia. Baadaye kidogo tukaona mfanyakazi mmoja wa kiwanda hiki anakuja mbio na kutoa taarifa  kwamba ameona watu watatu chooni ambao walimuuliza maswali Benjamin…”

“Walimuuliza  maswali gani?”

“Kwamba yeye ni mtoto wa Mzee Almasi na kwamba alikuwa amekiuka dhamana, hatujui ni dhamana gani kisha yule mmojawao aka…”

“Akamfanya nini mwanangu?”

“Sisi tulimkuta  tayari ni marehemu…”

“Una mmaana hao watu wamemuua?”

“Nasikitika kukueleza kwamba ndiyo hivyo”

“Wewe ulikuwa wapi?”

“Yeye Ben aliniambia kuwa anakwenda  msalani. Hao watu aliwakuta huko huko. Mimi sikuwaona”

Mke wa Almasi akaanza kupiga kelele kwenye simu hali iliyomfanya mlinzi huyo kukata mawasiliano.