Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya kutisha - Sehemu ya 22

MAUAJI 22 Pict

UTANGULIZI

“Akamfanya nini mwanangu?”

“Sisi tulimkuta  tayari ni marehemu…”

“Una mmaana hao watu wamemuua?”

“Nasikitika kukueleza kwamba ndiyo hivyo”

“Wewe ulikuwa wapi?”

“Yeye Ben aliniambia kuwa anakwenda  msalani. Hao watu aliwakuta huko huko. Mimi sikuwaona”

Mke wa Almasi akaanza kupiga kelele kwenye simu hali iliyomfanya mlinzi huyo kukata mawasilino.

SASA ENDELEA


Akarudi chooni na kumkuta Almasi anapiga simu polisi. Alipiga moja kwa moja kwa Inspekata Amour.

“Amour sasa hutakuwa tena na kazi ya kuwatafuta wale wauaji” akamwambia.

“Kwanini unasema hivyo. Sisi tutaendelea kuwatafuta usiku na mchana. Hatutawaachia” Amour akamjibu kwenye simu bila kumuelewa.

“Kwanini mpaka hivi leo hamjawakamata?’

“Hao watu ni wauaji wazoevu. Lakini serikali ina mkono mrefu. Pengine tumechelewa tu kuwakamata lakini ni lazima  tutawakamata watake wasitake”

“Kazi imekwisha. Mwanangu Benjamn niliyekuwa nikimpigania  asiuawe, ameshauawa sasa hivi”

“Unasemaje?”

“Nakwambia kwamba mwanangu Benjamin  naye ameshachinjwa sasa hivi. Hivi sasa sina mtoto tena. Huhitajiki tena kuwatafuta hao watu”

“Unasema kweli mzee?”

“Sasa mimi na wewe tunataniana? Ninakwambia ukweli mwanangu amelala hapa mbele  yangu. Tena amechinjwa chooni kama kuku masikini!”

“Ilikuwaje?”

“Mimi siwezi kukueleza ilivyokuwa, ngoja nimpe simu aliyekuwa mlinzi wake akueleze…”

Almasi akampa simu mlinzi huyo.

“Hebu mueleze Inspekta kilichotokea” Almasi akamwambia mlinzi huyo ambaye alipokea simu.

“Ndiyo Inspeta. Hapa  unaongea na aliyekuwa mlinzi wa Benjamin. Huyu mtu ameuawa sasa hivi kwa kuchinjwa”

“Nataka unieleze ilikuwaje?’

Mlinzi huyo akamueleza mwanzo mpaka mwisho.

Inspekata Amour aliguna.

“Mmepiga simu katika kituo chochote cha polisi?”

“Ngoja nimpe mzee akujibu”

Almasi akarudishiwa simu.

“Unasemaje?’ Almasi akamuuliza Inspekta huyo kwa sauti ambayo haikuwa tulivu.

“Umewaarifu polisi wa kituo chochote au bado” Amour akamuuliza.

“Kwani nikikupigia wewe si ndio  nimewaarifu polisi?”

“Kabla hujanipigia mimi, hujapiga simu kwenye kituo chochote?’

“Bado sijapiga. Hata ningepiga wangefanya nini wakati mtoto ameshauawa. Nimekupigia wewe ili kukuarifu tu…”

Amour aligundua  kuwa Almasi alikuwa amechanganyikiwa kutokana na hamaki ya mauaji ya mwanawe. Akamwambia.

“Tunakuja sasa hivi”

Almasi akakata simu. Alipokata simu ikaingia simu iliyotoka kwa mke wake. Akaipokea.

“Sasa mume  wangu kama Benjamin ameuawa, hali hii unaitafsiri vipi?” Sauti ya mke wake ikauliza.

“Mimi  sina tafsiri labda polisi wakija watatupa tafsiri”

“Kwani polisi hawajafika bado?”

“Ndiyo nimewaarifu sasa hivi, wameniambia wanakuja”

“Na mimi ninakuja huko huko”

“Hapana, wewe usije. Hutaweza kumtazama  mtoto wako. Tafadhali usije”

“Nisije  kwanini mume wangu wakati mtoto wangu ameuawa?’

Mke wake akaanza tena  kulia.

Almasi akakata simu.

Wafanyakazi walikuwa wamerudi tena chooni baada ya kutofanikiwa kuwaona  watu watatu waliokuwa wakiwatafuta.

“Polisi wanakuja. Yule kijana aliyewaona wale watu atahitajikakutoa maelezo” Almasi akawambia wafanyakazi hao.

“Mimi nipo hapa” Sauti ya mfanyakazi huyo ikasikika kutoka katika kundi la wafanyakazi.

Baada ya muda wa saa moja hivi Inspekta Amour akiwa na kundi la makachero aliwasili kiwandani hapo kwa kutumia magari mawili.

Waliingizwa katika eneo alilouawa Benjamin na kuushuhudia mwili wake uliolala ukiwa macho wazi.

Amour baada ya kuutazama mwili huo alitikisa kichwa kusikitika. Kilichomsikitisha ni kuona watu wa familia ya Alamsi walikuwa wakiendelea kuuawa  licha  ya kuwepo na juhudi za kuzuia mauaji hayo.

Alikereka kuona kikundi cha watu wasiofahamika walikuwa wanataka kuizidi serikali.

Wakati wote tangu makachero hao walipoingia katika eneno hilo, Almasi alikuwa akimtazama Amour kwa jicho la lawama kama vile yeye ndiye aliyetaka mauaji hayo  yatokee.

Baada ya kuukagua  mwili wa Benjamin Amour aliinuka  nakumshika bega Almasi.

“Kuwa mvumilivu mzee wangu, usifadhaike” alimwambia kisha akawaagiza wale makachero wengine waubebe mwili wa Benjamin  na kuupakia  kwenye gari.

Wakati mwili huo unapelekwa kwenye gari, Amour alimwambia Almasi kwamba wangetaka kupata maelezo jinsi Benjamin  alivyouawa.

“Kuna kijana ambaye aliona kila kitu”  Almasi akamwambia na kulitupia macho lile kundi la wafanyakazi waliokuwa wamesongana mahali hapo kuona kilichokuwa kinaendelea.

Yule kijana ajitokeze hapa” akawambia.

Mfanyakazi aliyewaona watu waliomuua Benjamin akajitokeza mbele.

Almasi akwambia Amour.

“Huyo kijana aliona kila kitu”

“Hebu tueleze nini kilitokea?” Amour akamuuliza.

Mfanyakazi huyo akaeleza alichokiona alipoingia msalani kabla ya Benjamin kuuawa.

Alieleza kuwa aliwaona  watu watatu, wawili walivaa mavazi meupe na mmoja alivaa mavazi meusi.

“Yule aliyevaa mavazi meusi alimuuliza Benjamin…”

:Kwanza kabla ya kuendelea nataka unieleze hao watu  watatu walitokea wapi?”

“Niliwakuta humu humu chooni, sikuweza  kujua waliingiaje”

“Kuna uwezekano wa watu kuingia katika eneo lenu bila kuonekana?”

“Kusema kweli haiwezekani. Pale kwenye geti la kuingilia kuna mlinzi, naye anasema hakuwaona. Na huwezi kufika katika eneo hili la choo bila kuonekana  na wafanyakazi wa humu ndani”

“Sasa mnadhani hao watu waliingia kwa wapi?”

“Haijafahammika hadi sasa”

“Enhe…hebu endelea kueleza”

“Yule aliyekuwa amevaa mavazi meusi alimuuliza marehemu ‘Wewe ni mtoto wa Almasi?’

Benjamin akamjibu ‘Ndiyo’

Akamwambia baba yako alikuweka dhamana lakini umeshindwakutimiza  masharti ya dhamana yako”

“Alimwambia alimuweka dhamana mahali gani?” Amour akamuuliza.

“Benjamin aliuliza hilo swali akajibiwa na yule  mtu kwamba muda wake wa kuishi ulikuwa umekwisha ndipo alipotoa panga na kumkata shingo”

“Muda wote huo wewe ulikuwa  wapi?”

“Nilikuwa nimesimama kando ya mlango”

“Hao watu watatu hawakukuona?”

“Walikuwa wameshughulika na marehemu”

“Mpaka  hapo wanamkata panga  ulikuwa umesimama unawaona?”

“Ndiyo”

“Kwanini hukupiga kelele kuita wafanyakazi wenzako ili wawakamate wale watu?’

“Kusema kweli kwanza sikujua kama wangemkata panga. Nilipoona lile panga linatolewa ndipo nilipozinduka na kupiga kelele”

“Baada ya kupiga kelele nini kilitokea?”

“Yaani wakati  napiga kelele ndio nilitoka  mbio  kwenda kuita watu”

“Lakini wakati huo walikuwa wameshamkata?”

Mfanyakazi huyo akanyamza kimya kwa kuona huenda alikuwa amefanya kosa kusubiri hadi Benjamin alipouawa.

Amour alipoona mfanyakazi hiyo amenyamaza alimuuliza.

“Unashindwa kujibu kwa sababu umegundua kosa lako, si ndiyo?”

“Muda ule nilipigwa na butwaa kwa sababu hata yule mtu aliyetoa panga hakuwa wa kawaida”

“Alikuwaje?”

“Kichwa chake kilikuwa kinaning’inia kama vile shingo yake ilikuwa imechinjwa”

“Hivyo ndivyo  alivyokuwa?’

“Ndiyo”

“Na wale watu wengine walikuwaje?”

“Wale wengine walikuwa watu wa  kawaida tu isipokuwa

walikuwa weupe sana”

“Kwa  hiyo baada ya wewe kutoka, kupiga kelele na kuita watu, nini kilitokea?”

“Tulikuja  humu chooni tukakuta Benjamin ameshachinjwa”

“Na wale watu waliishia wapi?”

“Hatukuwaona. Tuliwatafuta kila mahali. Wafanyakazi walikuwa na hasira walitaka kuwapiga lakini  hatukuwaona  tena”

“Walitoka kwa wapi?”

“Haijulikani”

Amour akamtazama Almasi.

“Mzee umesikia huyu mfanyakazi wako anaeleza kuwa huyo mtu aliyekuwa amevaa mavazi meusi alimsikia akimwambia marehemu kwamba wewe  ulimuweka dhamana. Je ulimuweka dhamna wapi?”

Almasi alibetua mabega yake

“Ni maneno ya kiwendawazimu! Nimemuweka dhamana wapi! Mimi sijui!”

“Nafikiri kuna kitu amekusudia. Sidhani kama alimwambia hivyo bure tu”

“Kama kitu gani Inspekta?”

“Mimi siwezi kujua ndio sababu ninahoji”

“Mimi pia siwezi kujua”

“Lakini ni kitu cha ajabu sana kwamba wauaji wameingia katika  eneno lenu bila kuonekana. Ninataka kumuona mlinzi anayekaa kwenye geti”

Mlinzi aliitwa. Akaja mbele ya inspekta Amour.

“Wewe  ndio unalinda geti?”

“Ndio”

“Kuna watu wasiotakiwa wameingia humu na kuua mtu na wewe ndiye mlinzi, utatueleza nini?”

“Mimi sikuwaona hao watu”

“Kuna mlango mwingine wa kuingilia?”

“Mlango ni huu mmoja”

“Sasa hao watu waliingilia kwa wapi kama si kwenye mlango huo?”

“Mimi sikuwaona”

“Itakuwa ni miujiza kwamba watu watatu wameingia hunu na kuua mtu bila kuonekana!”

“Lakini Inspekta kitu gani kinakushangaza?’ Almasi akamuuliza Amour.

“Ninashangaa kuona kwamba mnaye mlinzi anayelinda kwenye geti lenu na humu ndani kuna wafanyakazi lakini watu wasiotakiwa wameweza kuingia na kufanya mauaji!”