Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya kutisha – Sehemu ya 2

MAUAJI 2 Pict

UTANGULIZI

Mtu aliyekuwa karibu yake aligeuka ghafla na kumpiga kwa kitu kizito  kichwani. Frenk alipiga yowe akaanguka hapo hapo akiwa amepotewa na fahamu.

Mtu aliyempiga aliinama akamshika mikono na kumburuza kwenye kichaka kilichokuwa pembeni mwa njia. Alimuingiza ndani ya kichaka hicho akamlaza chini.

Wenzake walimfuata. Yule aliyekuwa akiendesha gari alikuwa ameshika begi ambalo aliliweka chini.

Alitoa simu kutoka mfukoni mwake akaipiga. Baada ya muda kidogo simu yake ilipokelewa..

SASA ENDELEA...


““TUMESHAMPATA yule mtu na tuko naye hapa njia panda ya kuja Marerani. Sasa njoo mara moja tumshughulikie,” akasema kwenye simu.

“Ni kijana?” Sauti ikauliza kutoka kwenye simu.

“Bado ni kijana sana na ana umbile lililotakiwa.”

“Mmemfunga sawasawa?”

“Samueli amempiga kichwani kwa kitako cha bastola, amezirai.”

“Sasa mmemfunga? Akizinduka anaweza kuleta usumbufu.”

“Sawa, tutamfunga kamba mikononi na miguuni.”

“Mkishamfunga mnisubiri hapo hapo.”

“Sawa.”

Yule mtu aliirudisha simu yake mfukoni akachutama na kufungua lile begi.  Alitoa furushi la kamba akawapa wenzake.

“Mfungeni kamba miguuni na mikononi. Jamaa anakuja sasa hivi.”

Watu hao walilifungua lile furushi la kamba na kulichakua. Zilikuwa kamba  nyingi ambazo zilikuwa vipande vipande.

Walichukua vipande hivyo vya kamba wakamfunga Frenk  mikononi na miguuni.

“Sasa tusubiri hapa hapa.” Yule aliyekuwa akiendesha gari aliwambia wenzake.

Alitazama saa yake kisha akatoa sigara na kujiwashia.

Baada ya kupita kama  nusu saa hivi, simu yake ikaita. Aliitoa mfukoni na kuipokea.

“Sasa mpakieni kwenye gari, muje naye chimboni. Mganga amesema kafara lake ni lazima lifanyike kwenye chimbo na huu ndio muda muafaka.” Sauti ikasikika kwenye simu..

“Sawa.”

Mtu huyo aliirudisha simu mfukoni akawambia wenzake wambebe yule kijana na kumpakia kwenye gari.

“Kwanini?” Mmoja akamuuliza.

“Amesema kafara lake linatakiwa lifanyike chimboni.”

“Yaani tutakwenda naye huko huko?”

“Hakuna  tatizo. Hivi sasa ni saa nane usiku, kila  mtu amelala. Nani atatuona?”

Walimbeba Frenk wakampakia katika siti ya nyuma ya gari hilo.  Mtu mmoja alikaa naye kwenye siti. Mwingine alikaa siti ya mbele pamoja na aliyekuwa akiendesha gari hilo.

Gari likawashwa moto na kuondoka. Baada ya mwendo wa dakika  kadhaa gari hilo likaingia katika viunga vya eneo la Marerani.

Lilisimama karibu na chimbo moja lililokuwa karibu na kibanda kimoja kilichojengwa kwa miti.

Aliyekuwa akiendesha alishuka na kwenda kwenye kile kibanda ambako kulikuwa na  watu wawili waliokuwa wamekaa.

“Tumekuja naye.” Mtu huyo aliwambia watu hao.

“Amezinduka?” Mmoja kati ya wale watu wawili waliokuwa wamekaa, akauliza.

“Hajazinduka  na tumemfunga kamba.”

“Sasa mtoeni kwenye gari. Mumburuze hadi pale kwenye chimbo. Fanyeni haraka. Hivi sasa watu wengi wamelala.”

Mtu huyo alirudi tena kwenye gari akawambia wenzake wamtoe Frenk na kumburuza kwenye chimbo. Wakati watu hao wakifanya hivyo, mtu aliyetoa agizo hilo  alimuacha mwenzake amekaa, akaenda kwenye chimbo akiwa ameshika mfuko.

Alipofika  kwenye chimbo hilo  aliuweka chini ule mfuko akatoa pembe mbili zilizofungwa kwa vitambaa vyeusi na vyekundu.

Pia alitoa  tunguri mbili alizoziweka karibu na mlango wa chimbo hilo. Frenk aliletwa mahali hapo kwa kuburuzwa chini ambapo isingekuwa rahisi kwa  mtu aliyekuwa mbali kumuona usiku huo kutokana na kutokuwepo kwa mwanga wa taa.

Frenk alilazwa kichalichali  karibu na mlango wa chimbo. Yule  mtu aliyetoa pembe na tunguri alichukua pembe moja na kumzunguka Frenk huku akimmwagia mavumba. Alimzunguka mara saba.

Alipomaliza aliziweka zile pembe akachukua tunguri na kuzunguka nazo mara saba huku akitabana maneno ya kichawi.

Alipomaliza alivua nguo zake zote akafanya mauzauza kabla ya kuwambia wale watu kwamba wamchinje kijana huyo. Mtu mmoja akamshika Frenk ili asifurukute na mwingine alitoa kisu na kukishika kichwa cha Frenk. Hapo hapo Frenk akazinduka.

“Kitu gani?” Akauliza kwa mshangao. Hakukuwa  na aliyemjibu.

“Niko wapi hapa na kwanini nimeshikwa hivi na kufungwa?” Akaendelea kuuliza.

Aliyekuwa amemshika alimshika vizuri. Yule aliyeshika kisu akaanza kumchinja harakaraka huku yule aliyevua nguo akisaidia kumshikilia asifurukute.

Kisu kilipoanza  kukata koo, Frenk alianza kukoroma. Alijaribu kufurukuta lakini waliomshika walikuwa wamemdhibiti sawasawa.

Damu ikaanza kumwagika. Dakika tatu tu baadaye kichwa kilikuwa kimetenganishwa na kiwiliwili!

Ile damu iliunda mchirizi na kuchirizikia kwenye mlango wa chimbo.

Mwili wa Frenk uliendelea kushikiliwa mpaka ulipotulia kabisa. Ndipo yule mtu aliyekuwa amekaa kwenye kile kibanda alipoinuka na kwenda mahali hapo.

“Tayari?” Akauliza.

“Tayari.” Mtu mmoja akamjibu.

“Sasa mrudisheni kwenye gari mwende mkamzike.” Yule mtu aliyevua nguo alisema huku akivaa suruaIi yake.

Watu hao walishika miguu ya Frenk wakamburuza hadi kwenye gari. Wakafungua boneti la nyuma na kuutia  mwili huo. Mmoja alirudi kufuatia kichwa cha frenk ambacho pia alikitia ndani ya boneti.

Aliyekuwa akiendesha gari hilo alikuwa amesimama akizungumza na yule mtu waliyemkuta hapo pamoja na yule mganga.

“Mtamzika mahali mbali na hapa. Mtakwenda kuchimba shimo refu ili mwilli wake usifukuliwe na fisi. Si mmesema hafahamiki?” Mtu huyo alimuuliza yule aliyekuwa akiendesha gari.

“Hafahamiki.Tumeambiwa kwamba alifika leo pale gesti, anamtafuta ndugu yake.”

“Alitokea wapi?”

“Alitokea Dar es Salaam.”

“Atakuwa ni mgeni. Hakuna anayemfahamu.  Sasa nendeni mkachimbe kaburi mumzike. Tukutane asubuhi.”

“Sawa,” aliyekuwa akiendesha gari alisema kisha akaondoka kuelekea lilikokuwa gari hilo. Alifungua mlango akajipakia na kuliondoa gari.

Mganga alikuwa akiitia michanga ile damu ya Frenk ili isionekane. Alipomaliza alimsogelea yule  mtu aliyekuwa naye ambaye alikuwa amesimama kando yake.

“Naona kazi imekwisha. Sasa zingatia vile nilivyokueleza. Asiingie mtu kwenye chimbo hili mpaka baada ya siku tatu. Wataingia watu watatu tu wakiwa uchi. Umenielewa?”

“Nimekuelewa vizuri.”

“Hawatafukua umbali mrefu watakuta mwamba ambao watautoboa. Huo mwamba una mali za majini ambazo huwezi kuzipata mpaka ufanye kafara la roho kama tulilolifanya hapa. Wakishapata hizo mali watatoka wakiwa uchi. Watavaa nguo watakapotoka.  Sijui kama  unanielewa vizuri?”

“Nakuelewa vizuri.”

“Mali watakayopata itatosha kukupa utajiri katika maisha yako yote na hutakiwi kurudia mara ya pili. Ukishapata hiyo mali nenda katafute biashara nyingine ufanye, ukirudia mara ya pili utakufa.”

“Sawa mzee.”

“Kingine ninachotaka kukukumbusha ni kuwa katika utajiri wako kila mwaka ukazamishe baharini fedha za mapato yako ambazo ni sawa na theluthi moja ya mapato yako. Hiyo ni zaka ya majini waliokupa mali.”

“Kama kweli nitafanikiwa nitafanya hivyo. Lakini ningependa kujua hizo fedha niziweke kwenye nini kabla  ya kuzizamisha baharini?”

“Swali zuri sana. Hizo  pesa utazitia kwenye mfuko mweupe. Utashona mfuko mweupe. Utaweka na jiwe ili ziweze kuzama chini. Unaweza kukodisha boti ikupeleke mbali kidogo.”

“Sawa. Nimekuelewa.”


************

Miaka kumi na mitano baada ya kuuawa Frenk. Martin Almasi aliuondoa mkoba wake wa kiofisa kutoka katika kaunta ya benki baada ya kuzipanga noti alizozitoa hapo benki.

Akiwa ameushika mkoba huo  kimadhubuti aligeuka na kuelekea katika mlango wa kutokea benki.

Aliusukuma mlango wa benki akatoka nje na kulifuata gari lake alilokuwa ameliegesha katika eneo la  maegesho.

Kila mwezi alikuwa akienda mwenyewe benki kutoa  pesa  za  mishahara ya wafanyakazi wao. Siku ile alikuwa amekwenda kuchukua  pesa za mishahara.

Alipofika kunako gari lake la kifahari, Martin alijipakia na kuliwasha gari hilo, akatia gea na kuliondoa.

Huku akiendesha kwa mwendo wa kasi kidogo, Martin alijiona alikuwa mmoja wa vijana waliofanikiwa katika jjiji la  Dar. Alikuwa ameshaoa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja aliyekuwa akimpenda sana.

Alimuoa mwanachuo mwenzake wa chuo cha  uhasibu ambaye alipendana naye tangu wakiwa wanasoma.

Baada ya kuanza kazi kwa baba yake ndipo alipofunga uchumba na Hilda ambaye kwa wakati huo alikuwa ameajiriwa serikalini.

Miezi michache baadaye Hilda alipata ujauzito ambapo alikuja kujifungua mtoto wa kiume waliyempa jina la Almasi  ambalo ni jina la babu yake.

Almasi mwenyewe ndiye aliyetoa jina hilo kumpa mjuu wake. Alipofahamishwa kuwa mkwe wake alikuwa amejifungua alikwenda hospitalini alikokuwa amelazwa Hilda.

Pamoja na mambo mengine, alimpa  pole na  hongera mkwe wake. Akakishika kichanga kilichozaliwa na kukiambia.

“Wewe ni Almasi”

Tangu hapo mtoto huyo akaanza kuitwa Almasi wakijua kuwa babu yake alikuwa ameshampa jina hilo..

Kuzaliwa kwa Almasi kulimfurahisha Martin na kumpa  hisia kwamba alikuwa ametoka katika kundi la utoto na kuingia katika kundi la utu uzima kwani si muuda mrefu atakuwa akitwa  baba.