Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya kutisha – Sehemu ya 1

MAUAJI

UTANGULIZI

Kazi ya kuchimba madini imegeuzwa ya kishirikina. Mauaji na makafara ni vitu vya kawaida. Almasi aliimaliza familia yake yote. Na mwisho aliimaliza familia yake yote pamoja na yeye mwenyewe.

SASA ENDELEA...


Aliwasili jijini Dar dakika chache kabla  ya saa nne usiku. Safari ya mchana kutwa kutoka Mwanza ambako aliondoka asubuhi ilimfanya ajisikie kuchoka.

Mara tu aliposhuka  kwenye basi, Frenk alitoka katika stendi ya Mbezi akapanda daladala iliyokuwa inakwenda Kariakoo.

Ilikuwa mara yake ya pili kuwasili katika jiji hilo.  Mara ya kwanza ilikuwa miaka mitano iliyopita. Alikuja kumtafuta kaka yake Amon  Marwa aliyekuwa amehamia Dar miaka mingi iliyopita. Kwa vile hakuwa na anuani ya mahali alipokuwa anaishi, Frenk  alijikuta akichanganywa na jiji hilo.

Aligundua jiji la Dar halikuwa kama lilivyo jiji la  Mwanza ambalo alikuwa amelizoea. Aligundua kuwa Dar es Salaam lilikuwa jiji kubwa na kwa mgeni kama yeye  lilikuwa linatatiza.

Aligundua haikuwa rahisi kumpata mtu anayemtafuta bila kuwa na anuani yake sahihi ya mahali anapoishi, mtaa na namba  ya nyumba. Yeye hakuwa navyo.

Frenk baada ya kuhangaika  kwa siku tatu bila  mafanikio ya kumpata kaka  yake, akaamua kurudi Mwanza.

Miaka mitatu baadaye akapata anuani ya kaka yake. Kuna mtu  ambaye alimwambia kwamba alikutana na  Amon na alimkaribisha nyumbani kwake Ilala jijini Dar.

Alimwambia kwamba Amon alikuwa ameoa mwanamke wa Kirufiji na alikuwa amezaa naye watoto watatu.

Kwa vile alitajiwa mtaa na  namba ya nyumba aliyokuwa anaishi Amon, Frenk alitafuta nauli, alipofanikiwa kuipata akaamua kurudi tena Dar kumfuata kaka yake.

Walikuwa wamepoteana kwa miaka mingi iliyopita tangu wakiwa watoto.  Mara tu wazazi wao ambao walikuwa wakulima walipofariki dunia, Amon akafanikiwa kwenda Dar akamuacha  mdogo wake akilelewa na shangazi yake.

Baada ya kuja Dar,  Amon hakurudi tana Mwanza. Shangazi yao alipofariki, maisha yalizidi kuwa magumu kwa Frenk. Hivyo aliamua kwenda kumtafuta kaka yake ili kama  amefanikiwa kimaisha  amsaidie kupata kazi.

Kulikuwa na watu waliokuwa wakimpa matumaini waliomwambia kwamba kaka yake alikuwa tajiri mkubwa jijini Dar, akifika Dar na kumuulizia tu atapelekwa hadi kwenye geti la nyumba yake.

Daladala  ilipomshusha Kariakoo, aliamua kwenda Ilala kwa miguu. Aliutafuta mtaa aliotajiwa. Alipoupata aliitafuta  nyumba ya Amon ambayo namba yake alikuwa ameikariri. Akaipata.

Alipoiona nyumba aliyokuwa anaitaka alipata furaha iliyochanganyika na mshituko. Alipata furaha kwa  sababu aliiona nyumba aliyokuwa anaitafuta lakini alipata  mshituko kuona  nyumba  yenyewe ilikuwa ni ya kawaida na si ya kifahari  kama alivyoambiwa na baadhi ya watu huko Mwanza.

Alibisha kwenye mlango.  Mlango ukafunguliwa na kijana mmoja ambaye alikuwa akitoka na hamsini  zake.

Frenkk alimsalimia. Baada ya  salamu akamuuliza.

“Sijui  nimemkuta Amon?”

“Amon nani?” Kijana akamuuliza.

“Amon Marwa.”

“Oh! Amon aliondoka kwenda Arusha.”

“Alienda lini?”

“Mh!Muda kidogo, inafika miezi sita sasa.”

“Mke wake yupo?”

“Alipoondoka alimuacha mke  wake lakini alishindwa kulipa pango ikabidi aende kwao.”

“Kwani Amon alikwenda kufanya nini huko Arusha?”

“Siwezi kujua lakini kuna watu walisema walikuwa wanamkuta kwenye gesti moja jirani na stendi ya mabasi pale Arusha.”

Ndoto ya kumpata kaka yake ikayayuka kichwani mwake kama bonge la barafu lililotiwa kwenye ndoo ya maji.

“Kwani hapa Dar alikuwa akifanya shughuli  gani?” Akamuuliza yule kijana kwa sauti ya kukata tamaa.

“Alikuwa akifanya biashara ya duka lakini alifilisika. Nafikiri labda aliamua akatafute maisha huko Arusha.”

Yule kijana  akaondoka na kumuacha Frenk akiwa ameduwaa kando  ya mlango.

Jirani na hapo palikuwa na gesti. Frenk akajikuta akitembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea katika gesti hiyo ambapo aliamua kupangisha chumba cha kulala baada ya kumkosa kaka yake.

Asubuhi kulipokucha Frenk akapata uamuzi wa kwenda Arusha kuendelea kumtafuta Amon.  Alikuwa na imani kuwa huenda alikuwa amefanikiwa huko Arusha na mahali pa kwanza  pa  kumtafuta ni hapo gesti ambapo aliambiwa alikuwa akionekana.

Alipanda basi la asubuhi sana kwenda Arusha. Karibu safari  nzima alikuwa akimuwazia kaka yake. Alijiambia endapo  atafanikiwa kuonana naye atakuwa ametimiza lengo lake.

Alijua kuwa angeweza kumkuta akiwa na mafanikio au akisaga lapa kama yeye. Lakini kwa vyovyote itakavyokuwa, alijiambia, kule kukutana kwao tu kungeweza kuwa mwanzo wa mafanikio yao.

Alifika Arusha jioni. Aliposhuka kwenye basi alikwenda kuitafuta gesti aliyoambiwa ilikuwa jirani na stendi.  Baada ya kuulizauliza wenyeji alielekezwa gesti hiyo. Akaenda kuonana na mhusika.

Alipomuuliza kaka yake, aliambiwa walikuwa hawamfahamu.

“Alitoka wapi??”  Kijana  wa gesti akamuuliza.

“Alitoka Dar kama miezi sita iliyopita. Niliambiwa alikuwa akionekana katika  gesti hii.”

“Hapa kwetu wanafika watu wengi kutoka Dar, hatuwezi kujua  ni nani mmojawapo.”

“Nimesema anaitwa Amon.”

“Amon wako wengi. Hatuwezi kujua ni  Amon yupi unayemuuliza wewe.”

“Yeye ni Amon Marwa.”

“Yukoje?”

“Tuliachana Mwanza tukiwa wadogo. Sijui umbo lake lilivyo kwa sasa. Wakati huo alikuwa ni mwembamba.”

“Kwa kweli itakuwa ni vigumu kumtambua.”

Baada ya maelezo yake kutosaidia kumtambulisha aliyekuwa anamtafuta, aliamua kukodi chumba hapo  hapo. Akajiambia atamtafuta kaka yake kwa siku  mbili. Endapo  hatafanikiwa kumpata atarudi Mwanza.

Baada ya kupata chumba alioga akabadili nguo alizokuwa maevaa kisha alitoka kwenda katika mkahawa uliokuwa karibu kupata chakula.

Baada ya kula alirudi gesti kulala. Hakukumbuka  ilikuwa saa ngapi alipoamshwa usingizini. Kwanza alidhani alikuwa anaota baada ya kusikia mlango wa chumba alichokuwa amelala ukibishwa.

Baada ya fahamu kumrudia vizuri aligundua kuwa hakuwa akiota bali mlango ulikuwa unabishwa kweli. Akainuka kitandani na kwenda kuufungua.

Alimkuta kijana aliyempangisha chumba hapo gesti akiwa na mtu mmoja ambaye alimwambia alikuwa akimfahamu mtu aliyekuwa akimuulizia.

“Unamfahamu Amon?” Frenk akamuuliza yule mtu kwa mshituko.

“Ndiyo namfahamu. Aliwahi kukaa hapa gesti kwa muda mrefu, hivi sasa yuko wilaya ya Simanjiro anafanya biashara.”

“Sasa nitampataje?”

“Mimi  naenda  huko huko. Kama unataka twende nitakupeleka mahali aliko.”

“Kweli tutapata usafiri usiku huu?”

“Nina  gari yangu binafsi, tunaweza kwenda tu.”

“Basi subiri nivae twende.”

Frenk akarudi ndani. Alivaa nguo haraka haraka akachukua begi lake na kutoka. Yule mtu alikuwa akimsubiri ukumbini.

“Twenzetu,” akamwambia.

Walitoka nje ya gesti ambapo palikuwa na gari aina ya Noah  iliyoegeshwa.

Ndani ya gari hilo kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa amekaa siti ya nyuma.

Frenk aliambiwa akae siti ya mbele kando ya dereva. Akafungua mlango na kujipakia.

Yule mtu naye alikaa katika siti ya dereva akaliwasha gari na kuanza safari ya kuelekea wilaya ya Simanjiro.

“Mimi naitwa Rafael, je wewe mwenzngu unaitwa nani?” Mtu huyo alimuuliza Frenk baada ya kimya kifupi.

“Mimi naitwa Frenk.”

“Huyo Amon ni nani wako?”

“Ni kaka yangu. Tuliachana zamani sana  huko Mwanza.”

“Alikuja hapa  Arusha miezi sita iliyopita. Hivi sasa anaishi Simanjiro na amefanikiwa sana kimaisha.”

“Nitafurahi sana kumuona  kaka yangu. Uliniambia kuwa  mnafahamiana?”

“Tunafahamiana na tunaihsi jirani. Wewe hujawahi kufika  hapa Arusha?”

“Sijawahi kufika.”

“Na huko Simanjiro ndiyo hukujui kabisa?”

“Kwa kweli huko sikujui.”

“Basi leo utakujua.”

“Nitafurahi.”

Safari ikaendelea. Gari hilo liliwasili Simanjiro saa nane usiku. Lilisimama mbele ya nyumba moja ambapo aliyekuwa akiendesha alishuka akaenda kubisha mlango.

Baada ya muda kidogo mlango ulifunguliwa, mtu huyo akaingia  ndani.

Haikupita muda mrefu akatoka akiwa na mwenzake aliyekuwa ameshika begi. Mwenzake alijipakia katika siti ya nyuma. Akakaa na Frenk.

“Vipi bwana?” Akamuuliza frenk.

“Salama tu.”

Gari likawashwa moto na kuendelea na safari.

“Hivi sasa tunakwenda nyumbani kwa Amon,” aliyekuwa akiendesha alimwambia  Frenk.

“Ni mbali sana kutoka hapa?”

“Hapana. Ni karibu tu.”

Baada ya mwendo mfupi walivuka daraja, wakaingia katika barabara za vichochoro. Walitokea katika eneo ambalo lilikuwa na pori. Baada ya kulipita pori hilo,  gari likasimama ghafla karibu na kichaka.

Aliyekuwa akiendesha alisonya kisha akafungua mlango.

“ Hili gari limeshaanza matatizo. Limezima  ghafla,” alijisemea kabla  ya kushuka na kwenda mbele ya gari hilo ambapo alifungua  boneti la mbele.

Wenzake waliokuwa katika siti ya nyuma nao walishuka  na kumfuata.

Frenki alipoona amebaki peke yake ndani ya gari naye alishuka. Alikwenda  mbele  ya gari hilo kulikokuwa na wenzake waliokuwa wakilikorokocha gari hilo.

“Lina  tatizo gani?” Frenk  akauliza.

Mtu aliyekuwa karibu yake aligeuka ghafla na kumpiga kwa kitu kizito  kichwani. Frenk alipiga yowe akaanguka hapo hapo akiwa amepotewa na fahamu.

Mtu aliyempiga aliinama akamshika mikono na kumburuza kwenye kichaka kilichokuwa pembeni mwa njia. Alimuingiza ndani ya kichaka hicho akamlaza chini.

Wenzake walimfuata. Yule aliyekuwa akiendesha gari alikuwa ameshika begi ambalo aliliweka chini.

Alitoa simu kutoka mfukoni mwake akaipiga. Baada ya muda kidogo simu yake ilipokelewa.