Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KISIWA CHAMAUTI -18

Muktasari:

  • ILIPOISHIA: “Mimi narudi kazini. Haitafika saa kumi nitakuwa nimesharudi. Wewe nenda sokoni kanunue unachofikiria kwamba utakipika na tutakula mimi na wewe  nitakaporudi. Sawa?”

ILIPOISHIA

“Mimi narudi kazini. Haitafika saa kumi nitakuwa nimesharudi. Wewe nenda sokoni kanunue unachofikiria kwamba utakipika na tutakula mimi na wewe  nitakaporudi. Sawa?”

“Una maana nitashinda hapa?”

“Ndiyo maana yake. Moyo wangu hautaki nikuache mapema”

“Sawa. Nimekuelewa’

Nikamuonesha Edda jiko lilipo, kabati la vyombo na vitu vingine ambavyo angehitaji kuvitumia akiwa hapo nyumbani.

SASA ENDELEA...


Baada ya hapo nikatoka na kumuacha.

Nilipofika ofisini kwetu nilikuta waandishi wenzangu wakinisubiri kwa hamu.

Nilivyoingia walinilaki na kunipokea kama mgeni wa shani huku wakinipongeza.

Kwa kweli nilifurahi na kufarijika. Waandishi wenzangu walinizunguka wakawa wananihoji maswali kuhusu tukio zima lililonitokea.

Mimi nilikuwa nimekaa, wao walisimama. Nikaaana kuwaeleza tangu nilivyoanza kumfuatilia Makita mpaka meneja wake alivyoniwekea dawa za kulevya na kunilaza katika chumba cha hoteli ambapo asubuhi yake nikakuta ule  mwili wa msichana aliyekufa na kudhani nimemuua mimi.

Niliwaleza hatua kawa hatua kila kilichojiri mpaka nilivyokamatwa na polisi na kuwekwa  ndani pamoja na maelezo aliyoyatoa meneja wa Makita baada ya mimi kukamatwa.

Baada ya maelezo yangu marefu ambayo yalikuwa kama hadithi ya kusisimua, waandishi wenzngu walinipa pole pamoja na pongezi kutokana na jinsi nilivyoukabili kishujaa mkasa huo.

Mhariri wangu naye alitoa maelezzo yake jinsi alivyolishughulikia suala langu baada ya kutoamini maelezo ya polisi kuwa niliua.

“Sasa ndio uamini kuwa kalamu inafanya kazi. Ni baada ya hii habari kutoka ndio polisi waliubaini ukweli” Mhariri akasema.

Aliendelea kueleza kuwa siku zote mti wenye matunda ndio unaochuchwa.

“Tukio hili liwe kipimo chako na likupe muelekeo wa mahali tunakokwenda” akaniambia na kuongeza.

“Siku zote nimekuwa nikusisitiza kuwa makini. Lakini hili suala la umakini hukulielewa Masha. Kama ungekuwa makini usingekubali kukirimiwa kilevi na mtu ambaye tayari umeshayatishia maisha yake”

“Ni kweli mkuu. Lakini naamini baada ya tukio hili nitakuwa makini zaidi” nikamwambia mhariri wangu huku nikitoa tabasamu la aibu.

“Kuna wenzako nimewatuma wafuatilie habari ya yule mwanamke ambaye mwili wa  binti yake umeibiwa na Makita. Kesho tutakuwa na stori nzuri sana kuhusu yule mwanamke”

“Kwa hiyo ile stori ya Makita ndio imekufa”  nikamuuliza mhariri wangu.

“Ile tutaendelea kuifuatilia, hatuwezi kuiacha”

Baada ya mazungumzo marefu niliruhisiwa nirudi nyumbani kupumzika kabla hata ya muda wa kutoka kazini kuwadia. Niliacha pikipiki  nikarudi nyumbani kwangu kwa kutumia daladala.

Nikamkuta Edda alikuwa akikaribia kuivisha pilau ya nyama.

Haukupita muda mrefu pilau ikawa tayari. Tulikula na Edda  na kufurahi.

Edda alikaa kwangu hadi saa mbili usiku nilipomrudisha nyumbani kwake.

Asubihi iliyofuata nilikwenda  kituo kikuu cha polisi kuandikisha maelezo yangu ya ushahidi. Baada ya hapo niliambiwa nitafahamishwa ni lini nitahitajika  mahakamani kutoa ushahidi wangu dhidi ya  Makita na meneja wake.

Nilipotoka kituo  cha polisi nikaenda kazini kwangu.

“Unakumbuka  jana uliambiwa leo asubuhi ufike kituo cha polisi kuandikisha maelezo yako?” Mhariri wangu akaniambia.

“Ndiyo natoka huko”

“Umeshaandikisha  maelezo yako?”

“Tayari”

“Polisi wamekwambia nini?”

“Wameniambia kwamba watanifahamisha siku ambayo nitahitajika kutoa ushahidi”

“Wamekwambia ni lini watawapeleka mahakamani?”

“Hawakuniambia lakini nafikiri itakuwa  ni hivi karibuni”

Zilipita siku nne kutoka ile siku aliyokamatwa Makita na meneja wake ndipo watu hao walipofikishwa mahakamani.

Wote wawili walishitakiwa kwa makosa mawili. Kosa la kwanza lilikuwa kuiba mwili wa binaadamu uliokuwa umehifadhiwa hospitalini.

Kosa la pili lilikuwa kuutumia mwili huo kuwadangaya polisi kuwa ni  mwili wa mfanyakazi wa hoteli ya Makita aliyeuawa na mwandishi wa habari.

Makita na meneja wake walikanusha mashitaka yote mawili.

Kila mmoja alikuwa na  wakili wake aliyekuwa akimtetea.

Kesi ile ilivuta watu wengi na karibu waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari walikuwepo mahakamani.

Mawakili wa washitakiwa waliwaombea dhamana wateja wao lakini upande wa mashitaka ulizuia dhamana kwa madai  kwamba bado wanaendelea na upelelezi na endapo washitakiwa wataachiwa kwa dhamana, wanaweza kuharibu ushahidi.

Hakimu alikubaliana na maelezo ya uapnde wa mashitaka na kutowapa dhamana washitakiwa.

Kesi hiyo iliendelea kuunguruma kwa miezi mitatu kabla ya washitakiwa hao kufanikiwa kupata dhamana.

Usikilizaji wa kesi hiyo ulipoanza, mimi nilikuwa shahidi wa kwanza kutoa ushahidi wangu. Ingawa ushahidi huo ilipingwa vikali na mawakili wa mshitakiwa lakini niliweza kujibu maswali yao bila wasiwasi wowote.

Kwa jumla kulikuwa na mashahidi kumi na wawili walioitwa kutoa ushahidi wakiwemo madaktari, mama wa binti ambaye mwili wake iliibwa hospitalini pamoja na polisi.

Mwisho wa siku hakimu alimwambia Makita na meneja wake kuwa wana kesi ya kujibu hivyo wanatakiwa wajitetee.

Waliandaa mashaidi wao ambao walikwenda mahakamani kutoa ushahidi wa uongo ambao ulipingwa na wanasheria wa upande wa mashitaka.

Baada ya Makita na meneja wake kujitetea ikafuatia hukumu. Wote wawili wakapatikana  na hatia kwa makosa yote mawili waliyoshitakiwa na walihukumiwa kifungo cha jumla ya miaka kumi  na miwili. Kila kosa moja kifungo chake kilikuwa miaka sita.

Nikashukuru kuona wale  watu waliotaka kunidhalilisha wamepata adhabu iliyostahili. Baada ya hapo ndipo nilipopeleka barua ya uchumba kwa kina Edda. Barua yangu ilikubaliwa. Miezi mitatu baadaye nikaona na Edda.

Baada ya kesi hii kumalizika nikawa sina hamu tena na kazi ya uandishi wa habari na pia sikuwa na hamu tena ya kuendelea kuishi Dar. Nikaacha kazi na kurudi kwetu Pemba.

Baada ya miezi michache ya kuishi Pemba mke wangu akafariki. Tukaurudisha mwili wake Dar na baada ya msiba kumalizika nikarudi tena Pemba. Kwa vile niliona kazi ya uvuvi inalipa nikajiunga na wenzangu sita waliokuwa na boti ya uvuvi nikaanza kazi ya uvuvi wa samaki.

Miezi sita baadaye nikapata mualiko wa kwenda Comoro kuhudhuria harusi ya binti wa raisi wa Comoro aliyeitwa Yasmin binti Sharif Abdilatif aliyekuwa akiolewa na mwana wa mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Comoro Abubakar Mustafa Al-Shiraz aliyekuwa akiishi Ufaransa.

Sisi tuliokuwa tunatoka Zanzibar tulialikwa na mke wa mkuu wa majeshi ya Comoro Kulthum ambaye alikuwa Mzanzibar tena Mkojani wa Pemba ambaye alialika ndugu zake walioko Zanzibar, mimi nilikuwa mmojawapo.

Ndege tuliyosafiri nayo ilifika Comoro saa kumi jioni. Ndoa ilikuwa inafungwa saa mbili usiku baada ya swala ya isha katika msikiti wa Riadha, msikiti mkuu wa ijumaa nchini humo. Nyumbani kwa bwana harusi kulikuwa kumejaa shamra shamra. Kadhalika nyumbani kwa Rais Sharif Abdulatif nako kulikuwa hakutoshi.

Kulikuwa na hoteli mbili kubwa zilizokodishwa siku ile kwa ajili ya sherehe za harusi. Na kulikuwa na hoteli nyingine kadhaa zilizokodiwa kwa ajili ya wageni walioalikwa kutoka nchi mbalimbali.

Sisi tulifikia katika hoteli ya Zaharani. Jina la hoteli hiyo lilifanana na jina langu. Jina langu ni Zaharani Shazume. Hoteli hiyo ilikuwa jirani na msikiti wa Riadha mahali ambapo ndoa ya Yasmin na Abubakar ingefungwa usiku ule.

Kwa kawaida msikiti wa ijumaa hujaa watu siku za ijumaa lakini siku ile kwa mara ya kwanza ulijaa watu katika swala ya isha.

Kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi na maafisa usalama waliokuwa na kazi ya kuhakikisha usalama unakuwepo katika eneo hilo.

Nilijitahidi sana nipate safu ya mbele lakini sikuweza. Safu hiyo ilikuwa imejaa masheikh na maafisa usalama. Nilibahatika kupata safu ya tatu yake.

Baadaya swala ya isha Rais wa Comoro Sharif Abdulatif alitakiwa kutoa idhini ya kumuozesha mwanawe.

Wakati anatoa idhini alipokea simu hapo hapo iliyomtambulisha kuwa binti yake Yasmin alikuwa ameanguka nyumbani na alikuwa akitokwa na povu mdomoni.

Shughuli ya ufungishaji ndoa ikasimama. Hapo hapo Rais Abdulatif na wasaidizi wake pamoja na maafisa usalama walitoka kwenda nyumbani.

Habari iliyopatikana baadaye ilieleza kuwa Yasmini alikuwa ameanguka na kupoteza fahamu huku akitokwa na povu midomoni. Baba yake alipofika na kumuona aliamrisha apelekwe hospitali harka.

Gari la hospitali lilikuwa limeshafika. Yasmin alipakiwa na kukimbizwa hospitali. Gari hilo la hospitali lilifuatana na gari la maafisa usalama na gari la rais mwenyewe.

Lakini gari alilopakiwa Yasmin likapata ajali kabla ya kufika hospitali. Tairi lake la mbele la upande wa kulia lilipasuka na kusababisha gari hilo kuyumba na kuligonga gari jingine kabla ya kupindukia kwenye mtaro uliokuwa kando ya barabara.

Heka heka ikawa kubwa! Magari ya maafisa usalama yakasimama. Maafisa hao wakashuka na kukimbilia kutoa msaada.

Dereva wa gari la hospitali alipotolewa alikutwa akiwa ameshakufa. Yasmin mwenyewe hakuonekana. Wauguzi wawili waliokuwa naye walikutwa wamezirai. Tukio hilo lilizua taharuki kubwa.