Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili iliyokufa - 47

HADITHI - 47 Pict

ILIPOISHIA

Sasa baada ya mkuu wa kituo kusema kwamba mimi ndiye niliyemripoti mganga huyo polisi ndipo walipoinua uso na kunitazama.

Bila shaka  walikuwa wakinilaani. Na kwa upande wa yule mganga alikuwa  akijiuliza nilivyopata akili hadi nikaweza kwenda kituo cha polsi  wakati  mwenyewe akiamini kuwa alikuwa ameniroga.

“Mnamtazama? Mkuu wa kituo akawauliza na kuwambia.

“Hata mkimtazama hamuwezi kumfanya  chochote.”

SASA ENDELEA...


Mkuu huyo wa kituo akaondoka kwenye meza aliyokuwa ameegesha tako lake, akaanza kurandaranda mle ofisini huku akiwa ameshika kifimbo chake mkononi.

“Huyu mwanamke naye mkamuweke ndani,” akawaambia polisi wawili wanawake waliokuwa wamesimama pembeni.

Mwanamke huyo akaambiwa ainuke. Alipoinuka, polisi hao wakaondoka naye.

Akabaki mganga peke yake.

Mkuu wa kituo hicho akamsogelea karibu yake, kisha akachutama na kumuuliza.

“Kumbe unapowapa huduma wake za watu huwa unawatongoza?”

“Hapana. Mimi ninawahudumia tu.”

“Wewe umeoa wanawake wangapi?”

“Nina wake wawili.”

“Ni nani na nani?”

“Mke wangu wa kwanza ni huyu aliyepelekwa ndani muda huu, na wa pili ni yule aliyepelekwa ndani mara ya kwanza.”

“Na huyu hapa ni nani wako?”

Mkuu wa kituo alinionyesha mimi.

“Huyo ni mteja tu aliyefuata huduma.”

“Sasa kwa nini ulikuwa unaishi naye nyumbani kwako?”

“Sikuwa naishi naye.”

“Tuliwakuta mko pamoja naye, tena wewe ndiye uliyekuwa naye chumbani. Au ndiyo ulikuwa unampa huduma?”

Mganga akanyamaza kimya.

“Yeye ameshasema kwamba nilikuwa nataka kumfyonza damu, wakati si kweli,” mganga akasema.

“Sasa tueleze wewe ukweli. Kule chumbani mlikuwa mnafanya nini?”

“Yeye aliniambia alikuwa haelewani na mume wake. Nilikuwa ninamfanyia dawa waende wakaelewane.”

“Ulimfanyia hiyo dawa kwa siku ngapi?”

“Alikuwa akija mara kwa mara.”

“Alikuwa haishi pale nyumbani kwako?”

Mganga akatikisa kichwa chake, lakini uso wake ulikuwa umeinamia chini.

“Mimi huwa silazi watu pale nyumbani. Nikishawahudumia wanaondoka.”

“Sawa. Sasa taarifa tulizonazo sisi ni kwamba huyu msichana alikuja kwako kwa mara ya kwanza wiki kadhaa zilizopita, na wewe ukaharibu akili yake akajikuta anabaki kwako na kukuona wewe kama mume wake. Lakini kumbe ulikuwa na mpango wa kumtoa kafara kwa majini yako; yaani ulitaka umuue kwa kumfyonza damu...”

“Si kweli... si kweli...”

Jinsi mganga huyo alivyokuwa mnafiki si kwamba alikataa tu kwa kusema si kweli, bali alitoa tabasamu la uongo, akathubutu kunitazama na kuniuliza,

“Mbona unataka kunizushia uongo? Nimekukosea nini?”

“Sijakuzushia uongo, kaka. Nilikuja kwako kwa shida zangu, lakini ukanigeuzia kibao... sijui mwenyewe ulivyofanya, nimejikuta tu naishi kwako, mume wangu nimemsahau....”

“Wewe uliishi kwangu? Si kweli. Labda kama uliishi kwa mtu mwingine, lakini si kwangu. Mimi siwezi kuishi na mke wa mtu. Kwanza mimi nina wake zangu wawili, na mmewaona,” mganga alinikatiza.

“Kama hukuwahi kuishi naye, mbona tulimkuta nyumbani kwako ukiwa pamoja naye?” Mkuu wa kituo akamuuliza.

“Si alikuja kwa shida zake.”

“Alikuja lini?”

“Leo ndiyo alikuja kwangu.”

“Sasa kama alikuja kwako leo, kule mlikokutwa mlikwenda kufanya nini?”

“Kule... kule....”

Mganga alikuwa amepata kigugumizi, lakini macho yake yalionyesha alikuwa akiwaza kwa haraka uongo wa kusema.

“Kule ndiyo!”

“Kule tulikwenda kufanya huo uganga wake.”

“Wewe ulikutwa umemshikilia unataka kumfyonza damu. Huo ndiyo uganga?”

Mganga alithubutu kutoa kicheko cha uongo.

“Sikutaka kumfyonza damu. Hii habari ya kufyonza damu si ya kweli.”

“Wake zako walithibitisha hapa kuwa unafyonza watu damu.”

“Sasa nyinyi mnawasikiliza wale. Wale si waongo tu!”

“Unasema wake zako ni waongo, wewe ndiye mkweli?”

“Ndiyo, mimi nasema ukweli. Kwa nini nidanganye?”

“Sasa mimi nakwambia ulimteka huyu msichana, ukaishi naye nyumbani kwako kama mke wako, na mwisho wa siku ukaenda naye huko unakokuita mzimuni. Na polisi wamekukuta unataka kumfyonza damu. Wake zako ni mashahidi.”

Mganga akatikisa kichwa.

“Si kweli... si kweli. Wake zangu wanaropoka tu.”

“Usifikiri unaposema si kweli tutakuachia. Unakabiliwa na kosa kubwa la mauaji. Umeua watu watatu!”

Mganga akanyamaza kimya.

“Na tutataka kuwajua ndugu wa wale marehemu waliofukuliwa ili tuwape taarifa za ndugu zao.”

“Kwanza ndugu zao hawana taarifa zozote.”

“Uliwaambia ndugu zao wamekwenda wapi?”

Mganga hakusema. Alinyamaza kimya.

“Au nao uliwateka kama ulivyomteka huyu mke wa watu?”

Mganga hakujibu.

Mkuu wa kituo, ambaye alikuwa ameonyesha kuadhirika, alimtazama mmoja wa polisi waliokuwapo pale.

“Koplo Hamisi, nenda kamuweke ndani. Tutaandaa mashitaka yake apelekwe mahakamani.”

Polisi mmoja akamshika ukosi mganga huyo na kumkokota. Tukabaki mimi, mume wangu, mkuu wa kituo na polisi wawili.

“Sasa nyinyi mtakwenda zenu. Kesho asubuhi nyote wawili mtatakiwa mfike hapa kituoni muandikishe maelezo yenu ili yatumike kama ushahidi. Mmenielewa?” Mkuu wa kituo alituambia.

“Tumekuelewa,” mume wangu akajibu.

“Basi mnaweza kwenda.”

Tukawaaga wale polisi na kutoka. Tukiwa nje ya kituo, wifi yangu alilipiwa na kaka yake pesa ya kupanda bajaji impeleke alikokuwa anaishi. Sisi tukaenda kwenye kituo cha daladala. Tukasubiri kwa dakika chache, daladala ikapita na kutupakia.

Tuliporudi nyumbani, mume wangu alinipa pole kutokana na misukosuko niliyoipata kutoka kwa yule mganga.

“Ukweli umedhihirika kwamba yule mganga alikuzuga,” akaniambia.

“Alinizuga na nilikuwa sijielewi. Siku ambayo nilijielewa ni ile niliyorudi.”

“Lakini kuna kitu kimoja unakificha, hujakifafanua.”

Hapo nikashtuka kidogo.

“Kitu gani nilichokificha?”

“Kama yule mganga alikufanya kama mke wake, ni kwamba mlikuwa mnafanya mapenzi,” mume wangu akaniambia.

“Sikuwahi kufanya naye,” nikambishia.

Niliogopa kukiri jambo hilo. Mume wangu angeweza kunichukia au pia kuamua kunipa talaka.

“Si kweli. Lazima mlikuwa mnafanya mapenzi, lakini siwezi kukulaumu kwa sababu ulikuwa hujielewi.”

Nikanyamaza kimya. Sikutaka kuendelea kubishana naye wakati ilikuwa kweli nilifanya mapenzi na mganga huyo.

“Lakini itabidi twende tukapime afya zetu, isije kuwa amekuambukiza balaa.”

Hapo nikamuuliza mume wangu,

“Tutakwenda kupima lini?”

“Hata kesho.”

“Sawa, twende tu.”

Mwanaume huyo huyo aliyeniambia twende tukapime, baadaye alijisahau. Wakati wa kulala nikaona mkono ukianza kunipapasa shingoni. Muda si muda tukajikuta tumeingia katika mahaba mazito. Kama niliambukizwa virusi na yule mganga, na yeye (mume wangu) alivipata.

Asubuhi yake tukaenda kituo cha polisi. Mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kuandika maelezo yangu. Nilitakiwa nieleze tangu siku ya kwanza niliyokwenda kwa yule mganga hadi yakatokea yaliyotokea. Nikaeleza hatua kwa hatua.

Baada ya kuandika maelezo yangu, mume wangu naye akatakiwa kuandika maelezo yake kama mume wangu ambaye nilimtoroka. Baada ya sisi sote kuandika maelezo yaliyotakiwa, tukaacha namba zetu za simu.

Tuliambiwa kwamba tutafahamishwa siku ambayo kesi ile itapelekwa mahakamani, kisha tukaruhusiwa kuondoka.

Tulipotoka kituo cha polisi nikamkumbusha mume wangu kwenda kupima. Kwanza alisita, kisha akaniambia,

“Haya, twende.”

Tukaenda katika kituo kimoja cha kupima virusi vya UKIMWI na kutoa ushauri nasaha ambacho kilikuwa Barabara ya Kumi na Nne.

Tulipofika, tukajieleza kwamba tulikuwa wanandoa ambao tulikuwa tunataka kupima afya zetu.

“Ni uamuzi mzuri,” mhudumu tuliyekutana naye akatuambia.

Akaendelea kutueleza kwamba watu wengi hawajajua umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara.

“Mara nyingi watu wanaokuja hapa ni wale wanaotaka kuoana. Wanapooana ndiyo hatuwaoni tena. Maambukizi ya UKIMWI yanaweza kupatikana hata ndani ya ndoa. Ni vizuri wanandoa pia wanakuja kupima afya zao na kupata ushauri nasaha kama mlivyoamua nyinyi.”

Baada ya kutupa maelezo marefu, akatuambia tuwe tayari kwa matokeo yoyote yatakayopatikana na kwamba tutapata ushauri nasaha, hivyo hata kama mmoja wetu au sisi sote tutagundulika kuwa na virusi, tutafundishwa jinsi ya kuishi navyo na maisha yakaendelea kama kawaida.

Aliyeanza kutolewa damu alikuwa mume wangu, kisha nikatolewa mimi.

Tukaambiwa tusubiri majibu wakati wateja wengine wakipewa ushauri nasaha.

Tulisubiri kwa karibu saa moja kasorobo. Majibu yetu yaliwekwa katika bahasha, kila mmoja bahasha yake.