Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili iliyokufa - 44

HADITHI - 44 Pict

ILIPOISHIA

Hapo ndipo nilipokumbuka. Wakati ule nilipokuwa nakwenda  kwake kufuatia  dawa ya  mume wangu akanichukua  hadi mahali hapo ambapo alikwenda  kuniingiliakimwili akajidaiananifanyia dawa, kumbe  alikuwa  akinizuga mimi. Na kutoka siku ile sikutamani  tenakurudi kwa mume wangu.

Sasa  kilichomshinda mganga huyokukieleza wazi ni kuniambiakwamba mahali hapo ni pale tulipokwenda akaniingiliakimwili.

“Nimeshapakumbuka”nikamwambia.

SASA ENDELEA...



ILIPOISHIA

“Siku zako za kuishi zinaisha leo. Mimi  ni Kashkash,jini mnywa damu za watu kila mwaka mara tatu…mimi  ndiye niliyekuchagua uolewe na kiti wangu ili muda ukifika ninywe damu yako. Sasa muda huo umeshafika, tulia nilekaramu yangu…!”

Mikono yake ikanivamia ghafla. Nilipiga ukulele mmoja tu kisha sauti yangu ikapotea. Niliendelea kupiga kelele lakini sauti ilikuwa haisikiki. Nilikuwa kama ninayepiga kelele kimoyomoyo au kwenye ndoto.

SASA ENDELEA...


Nikaona meno ya yule mganga yakisogea kwenye shingo  yangu na kuning’ata kwenye mshipa wa shingo.

Nilisikia maumivu makali kisha damu ikaanza kunitoka. Nikaendelea kupiga kelele zisizosikika.

“Jamani…  nakufa…jamani nakufa…!”

Mganga huyo aliyekuwa amebadilika  na kuwa jini alianza kunifyonza damu kwenye shingo.

Nguvu zilikuwa zikiniishia na sikuweza hata kujisogeza. Nilichoweza kufanya ni kuendelea kupiga kelele za  kimoyomoyo.

“Jamani nakufa…jamani nakufa…!”

Ghafla nikasikia mlio wa risasi ya bunduki huko nje halafu nikasikia mlio wa mabuti yakienda huku na huko.

Nikasikia risasi nyingine ikipiga ndani ya kile chumba. Jinsi  ule mlio ulivyovuma masikioni mwangu nilihisi kama ilipigwa kwa karibu na nilipigwa mimi. Yule mganga aliniachia akageuka nyuma.

Nilivyoachiwa nilijiona ninaanguka chini. Kabla sijafika chini nikadakwa. Sikuweza kujua nilidakwa na  nani.

“Wewe ni nani na unamfanya nini huyu mwanamke?” nikasikia  sauti ya amri ikiuliza.

“Mama inuka!” nikasikia sauti nyingine ikiniambia huku nikiwa nimeshikwa mkono.

Nikaunuka.

Sasa nikaweza  kuangaza macho yangu vizuri. Niliona wale watu walikuwa polisi. Walikuwa polisi watatu mmoja wao akiwa mwanamke. Wote walishika bunduki.

“Wewe nani?” ile sauti iliyokuwa ikimuuliza yule mganga ilirudia kumuuliza.

“Mimi…mimi…unaniuliza mimi nani katika nyumba yangu, kwani wewe nani?” Mganga akaunguruma.

“Sisi ni polisi” sauti ikamjibu.

“Mnataka nini?”

“Wewe ndiye mganga tapeli unayetorosha wake za watu halafu…”

“Hebu mtoe nje tumuone  vizuri…”

“Mbona kama ana meno marefu na macho  yake hayana mboni kisha  anatoka  damu mdomoni….?” Ilikuwa sauti ya yule  polisi  mwanamke.

Yule  mganga alivutwa na kutolewa nje  kama jambazi. Tulipotoka huko nje niliuona uso wake ulikuwa wa kawaida. Haukuwa na macho meupe wala meno marefu.

Sikujua alibadilikaje ghafla.

“Mnasemaje… mnaseje?” mganga huyo akauliza kama vile alikuwa  hajui lililotokea. Sauti  yake sasa ilikuwa ya kawaida. Haikuwa ile ya kukoroma.

Joho lake lilikuwa limejaa matone ya damu yangu na mimi damu ilikuwa ikinitiririka kwenye shingo.

Kulikuwa na polisi wengine wawili waliokuwa huko nje pamoja na mume wangu. Walikuwa wamewashikilia wale wake wawili wa mganga, mke mkubwa na mke mdogo ambaye sikuweza kujua alifikajepale kwa maana hakuwepo kwenye msafara wetu.

Polisi waliiona ile damu iliyokuwa ikivuja kwenye shingo yangu.

“Na hii damu inatoka wapi?” Yule polisi mwanamke akauliza kwa mshangao huku akiitazama  damu hiyo kwenye shingo yangu na kwenye lile joho la mganga.

“Alikuwa amening’ata na kuniifyonza damu” nikawambia polisi.

Nilivyotamka hivyo yule polisi mwanamke alimpiga kibao yule  mganga. Kilikuwa kibao kikali kwani alipopigwa aliguna akajishika shavu.

“Unamfyonza damu binaadamu mwenzako kwa maana gani?” akamuuliza.

Mganga akanyamaza kimya. Sasa alikuwa amenywea. Huwezikuamini kwamba ndiye yule aliyekuwa akiniambia “Siku zako za kuishi zinaisha leo…mimi ni Kashkash…”

“Alikuwa anataka kuniua. Aliniambia siku zangu za kuishi zinaisha leo…” nikaendelea kuwambia wale polisi huku nikijipapasa ile  sehemu niliyokuwa ninatoka damu.

“Siku zake yeye za kutapeli watu na kutorosha wake za watu ili awaue ndio zinaisha leo. Mshenzi mkubwa!” Polisi  mmoja akamwambia.

“Na hawa wake zake ndio vibaraka wake. Wanajua kila kitu. Wote  tutawafungulia mashitaka”

“Mimi simo. Mwenyewe nilikuwa nimelalanyumbani, sijisikii vizuri” yule mke mdogo akajitetea.

“Nyote nyinyi mnahusika” Polisi mwanamke akawambia.

“Sogeza gari” Polisi mwingine akasema.

Nikaona gari la polisi linakuja mbele ya ile nyumba.

Yule mganga pamoja  na wake zake wawili wakapakiwa kwenye gari hilo.

“Hebu tuingie humu ndani tufanye upekuzi” Polisi mmoja akasema.

Yeye na polisi wenzake wawili wakaingia ndani ya ile nyumba.

Baada ya muda wa kama robo saa hivi walitoka wakiwa wameshika sanduku la mbao. Wakaliweka chini.

“Huyu mtu alikuwa mnyama kweli” Mmoja wa polisi hao akasema kisha akaongeza.

“Humu ndani ya sanduku mna vichwa vitayu vya binaadamu”

Alilifungua lile sanduku. Tulipotupa macho yetu tukaviona vichwa hivyo vilivyokuwa vimekaushwa. Kichwa kimoja kilinifanya nigutuke.

Kilikuwa na sura ya mwanamke ambaye nilikuwa nikimuona nyumbani kwa yulemganga siku za mwanzo mwanzo halafu baadaye nikawa simuoni  tena. Lakini katika akili yangu nilikuwa namhisi kama alikuwa mmoja wa wake zake, yaani mke wake wa tatu kabla yangu.

Nikakisia kwamba mwanamke huyo atakuwa amefyonzwa damu na kuchinjwa na kisha kichwa chake kuhifadhiwa katika lile sanduku. Kwa hiyo hata vile  vichwa vingine vilikuwa vya watu waliofyonzwa damu na kuchinjwa.

Pale niligunudua kwamba yule mganga hakuniroga nikae kwake kwa kunipenda bali alitaka anitoe mhanga kwa majini wake kama alivyomtoa mhanga yule mwanamke wake mwingine.

Loh! Kama  si juhudi ya wifi yangu kuja kwa  mganga huyu na kufanyiwa ule uganga uliorudisha akili yangu, siku ile ningefyonzwa damu  na kuchinjwa  bila mume wangu kujua.

Nikatikisa kichwa changu kusikitika. Kumbe hawa waganga wana mengi, tunawapenda sana lakini wana hila. Wewe unakwenda akushughulikie tatizo lako kumbe yeye ana lake jambo!

Wale polisi wengine walipoviona vichwa hivyo walishituka.

“Hivi vichwa ni vya nani?” Mmoja wa wale polisi aliyetoka nalile  sanduku akamuuliza mganga huyo aliyekuwa kwenye gari.

Mganga akavitazama  kisha akabetua mabega.

“Sijui ni vichwa vya nani” akasema.

Yule polisi alimsogelea na kumtandika bonge la bao!

“Unasema hujui ni vichwa vya nani? Wewe si ndiye uliyewachinja hawa! Miili yao iko wapi?”

Mganga akanyamaza kimya. Akatandikwa bao jingine.

“Usiposema leo tunakuua hapa hapa mpumbavu wewe!. Tunajua hawa watu umewaua  wewe, miili yao iko wapi?”

Mganga alipoanza kujitafuna tafuna, polisi huyo alimkwida kwa hasira akamuinua juu na kumshusha kwenye gari.

Kile kitendo cha kukwidwa ghfla na kushushwa kwenye gari kama mzigo kilimfanya mganga agwae na kuhisi kitakachofuata baada ya hapo ni kipigo mwizi!

“Iko wapi miili yao?”Polisi huyo akamuuliza kwa sauti ya ukali akiwa bado amemshikilia kwenye ukosi.

“Niliizika…” Mganga akasema kwa sauti iliypfifia.

“Umeizika wapi, hebu tuoneshe?”

Mganga huyo alinyoosha mkono kuonesha kwenye ule mzimu wake.

“Wapi…tuoneshe…!” Polisi huyo akaendelea kumuuliza.

“Kwenye ule mzimu”

“Mzimu uko wapi?”

“Huu hapa”

Mganga aliuonesha ule mzimu wake.

“Hebu njoo unioneshe” Polisi aliendelea kumkazania.

Akiwa bado amekwidwa, mganga alimpeleka polisi huyo kwenye ule mzimu.

“Nimewazika humu ndani” akamwambia.

“Twende humo ndani”

Wakaingia. Mimi na mume wangu pamoja na polisi wawili tukawafuata.

“Hebu mulika tochi” Polisi aliyemshikilia mganga akamwambia polisi aliyekuwa na tochi ambaye alikuwa nyuma yake.

Polisi huyo akamulika tochi mbele na kukiondoa kiza kilichokuwa kimetanda.

Walipoingia katika lile eneo, mganga aliwaonesha kaburi lililokuwa chini ya kile kichanja chake ambacho siku ile alinipandisha hapo na kunibaka.

Polisi aliyekuwa amemshika ukosi mganga huyo  alimuachia na kumuuliza.

“Hebu tuoneshe vizuri umewazika wapi?”

“Nimewazika  hapa”

Mganga alionesha  chini ya kile kichanja.

“Umewazika hapa?”

“Ndiyo”

“Nani ni kwanini umewazika hapa?’

“Ndiyo mizimu ilivyotaka”

“Sasa ondoa hicho kichanja tulione hilo kaburi”

Mganga hakukataa. Akaanza kukisogeza kile kichanja.

“Na  hicho kichanja ni cha nini?”

“Nicha wenyewe” Mganga alijibu huku akiendelea kuburutana na kichanja hicho.

“Wenyewe kina  nani?”

“Wenye huu mzimu”

“Maneno  ya kijinga sana.  Hebu kiondoe haraka.

Wakati mganga  anakiburuta kichanja hicho kukiweka pembeni, polisi huyo alikisukuma  kwa nguvu  na kukipindua. Polisi mwingine akasaidia kukisukuma hadi pembeni mwa  mzimu huo.

Mchanga wa mahali kilipoondoka kichanja hicho ulikuwa umetitia.

“Hapa ndipo ulipoizika hiyo miili?” Polisi akamuuliza mganga huyo.