Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zari: Huu sasa ndio umri wangu halisi

ZARI Pict

Muktasari:

  • Zari alitimiza miaka hiyo Septemba 23, mwaka huu na katika mahojiano mapya ameeleza mkanganyiko kuhusu umri wake umetokana na changamoto ya upatikanaji wa nyaraka zake za kuzaliwa.

MFANYABIASHARA maarufu, Zari Hassan ‘The Boss Lady’, amefichua ana miaka 46, huku akisisitiza amezaliwa mwaka 1980, baada ya suala la umri wake kuwa gumzo kwa miaka kadhaa.

Zari alitimiza miaka hiyo Septemba 23, mwaka huu na katika mahojiano mapya ameeleza mkanganyiko kuhusu umri wake umetokana na changamoto ya upatikanaji wa nyaraka zake za kuzaliwa.

“Nimezaliwa mwaka 1980. Kliniki ilikuwa imefungwa, hivyo nilikuja Kampala kutafuta nyaraka zangu, lakini hawakunipata kwenye mfumo,” amesema Zari.

ZAR 01

Kauli hiyo imekuja wakati baadhi ya watu wakimhoji kuhusu umri wake kutokana na kuwa na watoto ambao tayari ni wakubwa. Zari amesema hana sababu ya kusema uongo kuhusu umri wake kwa sababu tu ana watoto wakubwa na alianza kupata watoto akiwa bado mdogo.

“Jamani, sina sababu ya kusema uongo kuhusu umri wangu kwa sababu tu nina watoto wakubwa. Nilipata watoto nilipokuwa mdogo, na nimekuwa nikikua pamoja nao,” amesema.

Hata hivyo, suala la umri wa Zari si jipya. Mjadala huo uliwahi kuwa gumzo zaidi mwaka 2018, wakati akiwa kwenye uhusiano na mwanamuziki wa Tanzania, Diamond Platnumz. Wakati huo Zari amesema alikuwa akielekea kutimiza miaka 38 mwezi Septemba, jambo lililoendana na mwaka wa kuzaliwa 1980.

Mwaka 2019, mjadala huo ulirudi tena baada ya hati ya kusafiria iliyodaiwa kuwa ya Zari kusambaa na kuonyesha mwaka wa kuzaliwa 1978. Zari alikanusha taarifa hiyo na kusisitiza kuwa alizaliwa Septemba 23, 1980.

Mwaka 2023, suala hilo liliibuka tena baada ya taarifa za hati yake kusambaa mtandaoni. Zari alirudia msimamo wake wa kuzaliwa mwaka 1980, akisema familia yake, ndugu zake na watu aliokwenda nao shule wanafahamu mwaka huo.

ZAR 02

Sasa, mwaka 2026, Zari amerudi tena kwenye suala hilo akiwa ametimiza miaka 46, akisisitiza 1980 ndiyo mwaka wake wa kuzaliwa na  hana tatizo na umri wake na hana sababu ya kuuficha.

Kwa upande wa familia, Zari ni mama wa watoto watano. Watatu aliwapata katika uhusiano wake na marehemu Ivan Ssemwanga, huku wawili, Tiffah na Prince Nillan, akiwa nao katika uhusiano wake wa zamani na Diamond Platnumz.

Baada ya uhusiano wake na Diamond kuvunjika mwaka 2018, Zari aliendelea na maisha yake na baadaye kuingia kwenye uhusiano na Shakib Cham Lutaaya. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2023, huku Shakib akiwa tayari ana watoto wawili wa kiume kutoka uhusiano wake wa awali.

Hivyo, kwa upande wa familia, Zari na Shakib wanahusishwa na jumla ya watoto saba.