Yvonne amkana kabisa Adebayor
Yvonne
YVONNE Nelson amedai kuwa magazeti ya Ghana yanapotosha mashabiki na wala si kweli kwamba ana ujauzito wa mshambuliaji wa Totenham Emanuel Adebayor. Wanakaa tu wanapika stori kuhusu mimi, angalia kwa mfano sasa wanasema nina mimba ya Adebayor, wanapata wapi habari kama hizi? Nimewahi kukutana na Adebayor mara moja tu na wala sina uhusiano naye sasa watu wanatoa wapi hizo stori. Ndio maana huwezi kuniona nikifanya mahojiano na mwandishi yoyote, kwavile nikifanya au nisipofanya wataenda kuandika vitu ambavyo sijasema, nimewahi kuzungumza na waandishi wawili tu Ghana. Kuna filamu natengeneza nimeigiza kama mwanamke mjamzito, picha zimeonekana kesho yake wanasema nina mimba,anashangaa Yvonne.