Wema afunguka mashabiki wake ‘walivyomchana’
Muktasari:
- Wema alisema miaka ya nyuma aliwahi kufanya hivyo na mashabiki zake kumjia juu na baadhi walimytukana huku wengine wakimchana hapendizi na mkorogo.
MSANII wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka alichokigundua ni mashabiki wake hawapendi atumie mkorogo.
Wema alisema miaka ya nyuma aliwahi kufanya hivyo na mashabiki zake kumjia juu na baadhi walimytukana huku wengine wakimchana hapendizi na mkorogo.
“Mimi hakuna kitu napenda kama kuwasikiliza mashabiki zangu wa kweli ambao huwa wananisapoti kwenye kazi zangu na hata jambo langu, hivyo kipindi cha nyuma nilijuta kuichezea ngozi yangu kwa kutumia mkorogo, ila niliona bora niache kufanya hivyo na hii ni kutokana na mashabiki kunishambulia sana mitandaoni kila nilipokuwa napojaribu, yaani mashabiki zangu hawakuwa wanataka kabisa nitumie.”
“Na niliona wako sahihi wala sikuchukizwa nao, maana kutumia mkorogo hatima yake ni kupoteza urembo wako wa asili uliokuwa nao mwanzo kabla ya kuanza kujichubua,” alisema Wema.