Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wema achoshwa na tetesi za ujauzito, afunguka mabadiliko ya Whozu

Muktasari:

  • Hivi karibuni kumekuwa na mijadala mingi katika mitandao ya kijamii kuhusu mwonekano wa Whozu na mashabiki wamebaini ameongezeka uzito ghafla na kubadilika kimwili tofauti na awali, huku kila mmoja akiwa na maoni tofauti juu ya chanzo cha mabadiliko hayo.

MSANII wa Bongo Movie amesema mabadiliko katika maisha yake na mpenzi wake, msanii Whozu yamekuwa mjadala mkubwa mitandaoni, hasa kutokana na mionekano yao ya mwili ikiwamo ishu ya kuwa mjamzito.

Hivi karibuni kumekuwa na mijadala mingi katika mitandao ya kijamii kuhusu mwonekano wa Whozu na mashabiki wamebaini ameongezeka uzito ghafla na kubadilika kimwili tofauti na awali, huku kila mmoja akiwa na maoni tofauti juu ya chanzo cha mabadiliko hayo.

Baadhi ya watu wamekuwa wakifanya utani kuhusu ukaribu wa Whozu na maisha ya Wema, wakihusisha mabadiliko hayo na maneno ya kejeli kuhusu mbwa 'Manunu alikuwa anamnyima raha', ambaye alikufa mwezi Mei.

Hata hivyo, akizungumza na Mwanaspoti, Wema anasema kuhusu mabadiliko ya Whozu ni matunzo tu na kuelewana vizuri zaidi kuliko awali na  sasa wanaishi kwa utulivu zaidi, wakizingatia zaidi maisha yao na namna ya kujitunza kuliko presha na mitazamo ya nje.

ISHU YA UJAUZITO

Wema anaeleza kuchoshwa na kuendelea kuhusishwa na habari za ujauzito kila mara anapoposti au kuonekana mitandaoni. Anasema baadhi ya watu husubiri tu aweke picha mpya ili waanze kujadili jambo hilo bila uthibitisho wowote.

Anaongeza anajua Watanzania wengi wanatamani kumwona akiwa na mtoto, lakini si sahihi kila wakati kila picha au posti kutafsiriwa kama ujauzito.

"Siri kubwa ya mabadiliko haya ni matunzo na kuelewana vizuri. Kwa sasa tunaishi kwa utulivu zaidi na tumebadilisha kabisa namna ya maisha yetu ya kila siku. Tumejifunza kuchagua watu wanaotuzunguka, kwa sababu kulikuwa na baadhi ya marafiki ambao hawakuwa na nia njema na walikuwa chanzo cha kukwaruzana, ingawa sitaki kuwataja majina yao. Pia tumebadili ratiba ya chakula na namna ya kujitunza, na hilo linaonekana hata kwenye muonekano wa Whozu. Kuhusu mitandao, watu wamekuwa wakinihusisha kila mara na ujauzito, kila nikiposti au kuonekana tu, jambo ambalo linakuwa la kurudiarudia bila uthibitisho. Najua watu wanatamani hilo, lakini si kila kitu kinachozungumzwa ni kweli, na nimepunguza sana kuposti picha na video nyingi Instagram ili kupunguza attention isiyo ya lazima."

KUPUNGUZA KUPOSTI, MARAFIKI WANAFIKI

Wema anasema amepunguza sana kuposti picha na video kwenye Instagram yake na sasa anaposti zaidi matukio na kazi badala ya muonekano wake wa kila siku.

Anasema sababu kubwa ni kuona watu wamekuwa wakifuatilia kila anachoposti na kuanza kuchambua maisha yake binafsi, hivyo ameamua kupunguza 'attention' ya aina hiyo.

Wema pia anaeleza moja ya changamoto waliwahi kupitia ni kuwepo kwa baadhi ya marafiki ambao hawakuwa na nia njema na walikuwa chanzo cha kukwaruzana na Whozu katika maisha yao ya karibu.

Ingawa hakutaja majina, amesisitiza watu hao walikuwepo kwenye maisha yao, lakini kwa sasa wamepunguza mzunguko wa watu wanaowazunguka ili kulinda utulivu wao.

Ukaribu wa wawili hao ulianza kutokana na matukio ya burudani na mitandao ya kijamii na walionekana mara kadhaa wakishiriki pamoja kwenye shughuli mbalimbali za kijamii na muziki.