Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ahadi ya Shakira kwa Ghetto Kids

SHAKIRA Pict

Muktasari:

  • Ahadi hiyo aliitoa kwenye tamasha lake la siku mbili lililofanyikwa Brooklyn’s Barclays Center, New York Marekani ikiwa siku chache tu tangu alipopafomu kwenye Halftime Show ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

HAIKUWA tu usiku wa muziki, bali pia wa hisia. Baada ya mwanamuziki kutoka Colombia, Shakira kumaliza tamasha lake la siku mbili lililofanyika jijini New York, aliwaahidi kundi la Ghetto Kids kutoka Uganda kwamba watazidi kuwa marafiki.

Ahadi hiyo aliitoa kwenye tamasha lake la siku mbili lililofanyikwa Brooklyn’s Barclays Center, New York Marekani ikiwa siku chache tu tangu alipopafomu kwenye Halftime Show ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

Nyota huyo aliyewahi kutwaa tuzo nne za Grammy na zaidi ya tuzo 15 za Latin Grammy, amewaambia watoto hao kuwa watabaki kuwa sehemu ya maisha yake hata baada ya kila mmoja kurejea kwao.

SHAKI 03

"Msihuzunike, tutakuwa marafiki milele naahidi. Nitawapigia simu nitakapokuwa Uganda, na Milan pamoja na Sasha pia watawasiliana nanyi," amesema Shakira huku akiwakumbatia watoto hao akitokwa na machozi baada ya onyesho hilo.

Kauli hiyo imewagusa wengi waliokuwa nyuma ya jukwaa, ikionyesha upande mwingine wa msanii huyo wa ukaribu wake na watoto kupitia shughuli mbalimbali za kijamii na elimu anazozifanya kupitia taasisi yake ya Pies Descalzos Foundation.

SHAKI 02

Katika maonyesho hayo, Ghetto Kids walionyesha umahiri wao wa kucheza, huku Shakira akiendelea kuthibitisha kwa nini amebaki kuwa mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa duniani baada ya zaidi ya miongo mitatu kwenye muziki.

Shakira alianza safari yake ya muziki akiwa na umri wa miaka 13 kabla ya kung'ara kimataifa mwaka 2001 kupitia albamu ya Laundry Service, iliyobeba nyimbo maarufu kama 'Whenever, Wherever' na 'Underneath Your Clothes'. 

Tangu wakati huo, ameuza zaidi ya nakala milioni 95 za albamu duniani, na kuwa mmoja wa wasanii wa Kilatino waliouza kazi nyingi zaidi katika historia ya muziki.

SHAKI 01

Mbali na mafanikio hayo, Shakira ameandika historia kwa kuimba kwenye matukio makubwa ya soka duniani, ikiwemo wimbo wa Kombe la Dunia 2010, 'Waka Waka (This Time for Africa)', ambao umeendelea kuwa miongoni mwa nyimbo za michezo zinazotazamwa zaidi duniani.

Kwa upande wa Ghetto Kids, safari yao ilianzia mitaa ya Kampala nchini Uganda chini ya mwanzilishi wao Dauda Kavuma maarufu kama Uncle Dauda. Kundi hilo lilijizolea umaarufu kupitia video za dansi zilizokuwa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, kabla ya kupata mwaliko wa kushiriki vipindi na maonyesho makubwa ya kimataifa.

Mwaka 2023, Ghetto Kids walipata umaarufu dunia walipofika katika fainali za Britain's Got Talent, wakimaliza katika nafasi ya sita baada ya kuwashangaza majaji na watazamaji kwa mchanganyiko wa dansi, sarakasi na simulizi za maisha yao.

Mbali na hilo, kundi hilo limewahi kushiriki kwenye mashindano ya America's Got Talent.