Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasanii na watengeneza maudhui 21 wasamehewa makosa ya jinai

Muktasari:

  • Katambi ameyasema hayo leo Septemba 2, 2026, alipokutana na wasanii hao ambao aliwaita kufika katika ofisi za wizara hiyo kwa ajili ya kutoa maelezo na kupewa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema wasanii 21 waliokutana na wizara hiyo wamepewa msamaha wa makosa yao ya awali ya jinai yaliyohusishwa na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Katambi ameyasema hayo leo Septemba 2, 2026, alipokutana na wasanii hao ambao aliwaita kufika katika ofisi za wizara hiyo kwa ajili ya kutoa maelezo na kupewa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

Amesema wasanii hao wanapaswa kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya mitandao, akisisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba kauli, matendo na mienendo inayotolewa mitandaoni inapaswa kuzingatia utu na maadili ya jamii.

Kwa upande wa mwakilishi wa wasanii na watengeneza maudhui wa mitandao, Mwemba Burton maarufu Karma Mwijaku amesema wasanii wanapaswa kufuata sheria na kutotumia majina yao vibaya, huku akiwataka kutumia nafasi zao kuelimisha na kujenga jamii.

Katambi amesema baadhi ya wasanii hawakufika katika kikao hicho kutokana na sababu mbalimbali, huku wale waliohudhuria wakitakiwa kuwa mabalozi wa kuwafikishia ujumbe wenzao ambao hawakufika.